BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Kaka yangu Lazaro Nyalandu kama wajumbe walikua 30, Lissu akapata 24 ilikuaje ukamgaragaza? Hizi hesabu zako mbona hazifuati formula ya MAGAZIJUTO? Kama Lissu alipata 24 kati ya 30 it means wewe uliipata kura 6. Kwahiyo unataka kutuambia ulimgaragaza kwa kura 6?
Halafu kwa maoni yangu nadhani uache kuongelea haya mambo ya Chadema, wewe jenga chama chako. Chadema ilikupokea na ikakupa heshima ya nafasi mbalimbali za uongozi. Kwakua umeamua kuondoka sidhani kama ni sahihi kuanza kuisema vibaya.
Najua unatafuta "remedy" huko CCM ili uaminike tena. Lakini usitafute remedy kwa kuisema vibaya Chadema. Hii itakuharibia zaidi kuliko kukujenga. Kumbuka ulivyojiunga Chadema uliisema vibaya CCM, na sasa umerudi CCM unaisema vibaya Chadema. CCM watakuwa wajinga sana kama wakikuamini kwa sababu unatoa siri za Chadema, wakati wanajua ulitoa pia siri za CCM ulipoenda Chadema.
Yani hapa umejijenga ukuta wa kutokuaminika pande zote mbili. Unavyoendelea kuiponda Chadema CCM wanakuona "snitch" kwa sababu wanajua uliiponda pia CCM ulipokua Chadema. Ukiachana na mwanamke akaenda kwa mwanaume mwingine, ikatokea akarudi kwako halafu akaanza kumponda yule mwanaume mwingine, basi ujue hata wewe alikua anakuponda alipokua kwa huyo mwingine. Simple logic. USIMUAMINI TENA.!
Unavyoendelea kuikandia Chadema unawapa CCM sababu nyingi zaidi za kutokukuamini, kuliko ungekaa kimya.
Njia nzuri ya kuaminika ndani ya CCM ni kutulia na kujenga chama chako. Msaidie Mwenyekiti wenu mpya kufanya reforms za mifumo. Mmepata Katibu Mkuu bora sana, msaidieni kukujenga upya chama chenu. CCM imepoteza ushawishi sana kwa vijana, jiulizeni tatizo ni nini ili mfanyie kazi mapungufu.
Hizi porojo za kwamba ulipata kura 6 kamati kuu halafu ukamgaragaza Lissu aliyepata 24, hazikusaidii sana wala hazisaidii chama chako.!
GJ Malisa