PreGE2025 Nyamuhokya: Mwaka huu Tucta hatuna madai kwa Rais labda yeye kama mama akiona ana cha kufanya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tatizo la kuchagua machawa kuwa viongozi wa TUCTA ndiyo hili.

Ktk nchi ambayo wafanyakazi wanalipwa ujira (na siyo mishahara), boss wa TUCTA anasema hana cha kudai??

95% ya wafanyakazi Tanzania wanalipwa chini ya 1.5M kwa mwezi. Huu ni ujira siyo mshahara.
 
Sijui mimi ndo nimemwelewa huyo Katibu kwa mtazamo mwingine?

Mimi namtazama Tumaini Nyamuhokya kama mtu aliyekata tamaa kudeal na chura kiziwi, maana kila analomwambia kuhusu Wafanyakazi wa nchi hii hajali kabisa.

Ukitaka kujua msimamo wa Katibu wa TUCTA rejea kauli mbivu ya Mei Mosi, 2025. Ni bango dhidi ya Utawala uliopo madarakani.
 
Ahsante sana!!!!!
Nilikuwa tu napitia comments za watu hapo juu kabla ya kuikuta hii Yako, nikiri nimesikitika sana......watu wameoza na akili za kisiasa maji taka basi muda wote wanawaza hasi tu. Wamekurupuka kumtukana baba wa watu wakiwa hata hawajui kaongea katika muktadha gani. Kuna watu, nakuapia, wakishika hii nchi siku Moja tu tunachapana. Mungu anajua sana!!
 
Daaaaa kweli tunachezewa sana....TUCTA CWT Woote mapandikizi......tangu kina Mkoba walipopiga deals miaka ile sina hamu na mapandikizi.....Bank Walimu inaendekeaje??
 
Na kwa nini mshiriki hata hayo maandamano yao kama tayari ana majibu? Why usijilalie tu na kupiga biere zako maskani mambo yaishe tu? 😀
 
Huko TUKTA na CWT wanaweka makada wa CCM na hii njia wamefanikiwa sana ukizingatoa pia na Wafanyakazi wengi ni vilaza wajinga.

Vyama vya wafanyakazi viko Kenya, tu kwa EAC nzima.
 
Hili punga linaongea utumbo , mwaka jana walikuwa ya nyongeza ya mshahara, Samia akawapiga chenga akamtuma Dr. Mpango awaambie kuwa mtasikia kitu toka kwa Rais hivi karibuni lakini hadi leo Rais hajazungumzia kuhusu nyongeza za mishahara halafu junya linaropoka wafanyakazi hawamdai, pumbavu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…