Mzungu.
Mapenzi.Makaratasi?
Ebu tupe UZOEFU kidogo....Ndiyo.
Nakumbuka wakati bado niko dogo rafiki yangu mmoja na mdogo wake walinichangia bana.
Siku hiyo nilienda kwao kucheza halafu tukaishia kukorofishana nikaanza kupigana na kaka mtu halafu mdogo mtu naye akaingilia.
Licha ya kwamba walikuwa kwao na wao kunichangia, niliwachakaza wote.
Walipoona wamezidiwa wakaenda kumfungulia mbwa wao na kunisakizia.
Ile wanaenda bandani kumfungulia bobbi wao mi tayari nishaacha vumbi nyuma yao.
Enzi nikiwa dogo nilikuwa na mbio sana.
Marafiki wa huku uraiani:
Kusema ukweli mimi niko 'picky' sana na pia niko 'mfikiriaji' sana.
Huwa siruhusu kirahisi watu wanijue kiundani hadi niwe nawaamini.
Na hadi nije nimwamini mtu hunichukua muda mrefu sana.
Kwa msingi huo, marafiki wa karibu nilionao huku uraiani ni wale niliosoma nao kuanzia chekechea mpaka shule ya upili.
Kwa bahati nzuri sana nilibahatika kusoma nao shule moja...kuanzia chekechea, msingi, hadi upili.
Hivyo hao nimejuana nao tokea utotoni. Nimecheza nao, nimepigana nao, nimewinda nao ndege, nimefuga nao njiwa, na mengineyo mengi.
Idadi yao hao haizidi vidole vya kiganja kimoja!
Wa mtandaoni:
Kusema ukweli, mtandaoni sijawahi kupata rafiki wa kweli.
Ambao ninao ni washikaji tu.
Siwajui kivile na wao hawanijui hata robo.
Huku kwenye mitandao huwa nipo makini sana kuliko hata umakini wenyewe.
JF ya sasa ikoje kwani?That time JF was JF. Na ilikuwa kama familia.
Mambo yamebadilika inabidi uende tu na aina ya mdundo wa sasa.
Naweza kusema wanachama wamekuwa wengi wa kila aina hasa teenagers kuheshimiana kumekwisha.JF ya sasa ikoje kwani?
Maana kila nikiingia najiona kama mgeni watu siwatambui, naishia kusepa tu...
1. Ulimwambia nini au ulimuudhi nini mpaka akakupiga?Mwenyewe alijistukia akaomba samahani yakaisha.
Kikofi chenyewe wala hakikuuma😀
Unaonaje Mahondaw ikifuata intervew yako..!!
Tehtehteh Nitakimbiaje hio interview heeeeeeeee hamtaamini kwa hio speed [emoji125] [emoji125] [emoji125]Unaonaje Mahondaw ikifuata intervew yako..!!
Nina mengi sana nataka kujua juu yako na mimi nitakuwa miongoni mwa/wa watakao uliza maswali...
Ngoja nijaribu kuwasiliana na RALLY KING jr (Stunter)...
Kumbuka nina maswali mengi ya UFUKUNYUKU .......unatakiwa unipange
Dogo janja na mimi nataka intavyuu.Hahahahahaha!!
Dah kweli kabisa, hata mimi siyafurahi maisha ya ugenini
Hahahahaaaaaaa mkuu umenikumbusha Yule jamaa aliyeenda ukweni akaumwa na Tumbo la kuharisha .Oh yeah...mara nyingi tu.
Kutokuwa huru. Wakati mwingine huwezi kujua kama unachokifanya kinawapendeza au kuwachukiza wenyeji wako mwisho unaishia kuhisi hisi tu na kuanza kujistukia. I hate that.
Usafi wa hiyo sehemu hususan wa bafu, choo, jiko, na vyombo vya mezani kama vijiko, bilauri [sipendi kabisa kunywea maji bilauri za watu]. Nipo radhi nitumie paper plates na vijiko au uma wa plastiki kuliko silverware zao.
Kuwasha tivii na kuangalia nipendacho.
Kufungua jokofu muda wowote na kuchukua chochote kilichomo.
Kuoga navyotaka mimi. Nikiwa hapa kwangu naweza hata kumaliza dakika 45 naoga bafuni.
Kwa watu huwezi kufanya hivyo.
Kufua nako pia. Hapa muda wowote tu naweka nguo kwenye washer na dryer bila hofu yoyote ile.
Kujilaza popote pale...iwe sakafuni..kwenye kochi...kwenye futon....ukiwa kwa watu huwezi kujiachia hivyo.
Hata kwenda haja kubwa nako inabidi uende kwa kuwalia watu timing....sipendi kabisa aisee.
Hapa kwangu nikisikia tu mzigo unagonga hodi naenda bla hofu yoyote ile.
Imagine uko kwa watu halafu unabanwa mavi na choo kiko ndani ya nyumba karibu na jikoni....
Unaingia chooni halafu unashusha mzigo tena ule unaoambatana na makelele...noma sana yaani.
Halafu ukimaliza na kutoka unaanza kuombea asiingie mtu mwingine kabla harufu haijaisha...man...I hate that.
Ila kale ka movie ka 'Coming to America' nako kalikupa mshawasha wa kwenda US Kwingwa....HahaaaaaUzuri wangu ni kwamba tokea nikiwa mdogo kabisa nilipata fursa ya kutembelea nchi mbalimbali za Ulaya.
Pia, nikiwa mdogo niliwahi kuishi Uingereza kwa miaka kadhaa.
Mshua wangu alisomea Marekani...shahada zake zote. Nyumbani tulikuwa tunaletewa majarida kibao ya Kimarekani kama vile Reader's Digest na Time Magazine, almanac ya CIA World Fact Book, World Book Encyclopedia, na kadhalika.
Kwa hiyo, ukijumlisha mimi kusafiri nikiwa mdogo, kuishi Uingereza, na kusikiliza stori za mshua kuhusu Marekani, kusoma hayo majarida na hivyo vitabu,picha ya Marekani niliyokuwa nayo kabla sijaenda ndo hiyo hiyo niliyoiona nilipofika. to Hakukuwa na surprise yoyote kabisa.
Halafu majirani zetu tulipokuwa tunaishi walikuwa Wamarekani. Kwa hiyo sikupata culture shock yoyote ile.
So I took to the USA like a duck to water🙂.
Mwanzoni kusema ukweli nilikuwa homesick sana.
Kumbukua, nilienda USA nikiwa mdogo kwa kweli.
Kwa hiyo huo udogo, umbali, na ukizingatia kwamba mimi sina kaka wala dada, kuna nyakati nilikuwa najikuta napakumbuka sana nyumbani.
Sawa, baba na mama nilikuwa nao na ningeweza kuchukua tu simu na kuwapigia ili kuongea nao, lakini bado mazungumzo ya mtoto na wazazi wake ni tofauti na mazungumzo ambayo mtu unaweza kufanya na kaka au dada zako au hata marafiki zako.
Hivyo homesickness ndo ilinisumbua sana hapo mwanzoni mwanzoni.