Nyani Ngabu Mjengoni! Interview: Mapenzi, Utajiri&Mali, Marafiki na Maisha ya ugenini.

Nyani Ngabu Mjengoni! Interview: Mapenzi, Utajiri&Mali, Marafiki na Maisha ya ugenini.

JF ya sasa hivi imekosa utulivu. Hususan utulivu wa michango yenye hoja zenye mashiko na za kuvutia.

Lakini hilo ni jambo la kutegemewa, kwa mtazamo wangu.

Kadri udadi ya wanachama inavyozidi kuongezeka na kadri majukwaa yanavyozidi kuongezeka ndo vurugu nazo zinavyozidi kuongezeka.

Zamani jukwaa kuu lilikuwa la siasa tu na mada zilikuwa za kiutu uzima zaidi.

Siku hizi kuna kila aina ya watu na kila aina ya takataka.

Imagine watu wanajiaminisha kuwa wanakujua wewe Daby ilhali hata kukuona hawajawahi, hawajui unaitwa nani, hawajui unaishi wapi, hawajui unafanya nini, kisa tu eti wanakusoma humu JF.

So penye wengi pana mengi.

Hata zamani Dar haikuwa chafu kama ilivyo sasa na haikuwa na uhalifu kama uliopo sasa. Hata dada poa hawakuwepo.

Kwa hiyo hata haya mabadiliko ya JF ni mambo ya kawaida tu. Kadri JF inavyozidi kukua na kadri idadi ya wanachama inavyoongezeka na yenyewe [JF] inabadilika kwa mazuri na mabaya.
Asante saana NN, JF imebadilika saana ni kweli.

Mara nyingi nimekuwa msomaji saana jukwaa la siasa sio mchangiaji kivile lakini nimekunona mnavyorushiana maneno na baadhi ya member n.k.

je Yanaishia hapo au kuna hatrage zaidi ikitegemea xxx alishalalamika kufuatwa pm na kutukanwa.
 
Hahahahah
Hivi Nyani Ngabu katika kuishi kwako kote huko ughaibuni, kuanzia college hadi kazini,
ulishawahi kukutana na wazungu wenye tabia za kiswazi /kiswahili?
Mfano wanawake kutupiana maneno ya mafumbo n.k...
Hebi nijibu hili please

Ngoja nikwambie kitu kimoja...tabia haina rangi ya ngozi.

Tabia zote unazoziona uswazi hata kwa wazungu zipo.

Ona hao

 
Unajua kuna baadhi ya majibu yeye anayaona yako sawa kwa upande wake, ila kwa upande mwingine yanaweza sababisha ukosefu wa utulivu wa nafsi kwa baadhi ha member.
Kabisa.
Ila naamini moyo wa madame B hautikisiki kwa mirindimo ya majibu ya hivyo.
 
Asante saana NN, JF imebadilika saana ni kweli.

Mara nyingi nimekuwa msomaji saana jukwaa la siasa sio mchangiaji kivile lakini nimekunona mnavyorushiana maneno na BAK n.k.

je Yanaishia hapo au kuna hatrage zaidi ikitegemea BAK alishalalamika kufuatwa pm na kutukanwa.

Hapana.

Hayo maneno kwa upande wangu yaliishia na huwa yanaishia hapa hapa.

Mimi huyo jamaa hata simjui kabisa.

Kama aliwahi kufuatwa na kutukanwa na mtu PM basi mtu huyo hakuwa mimi.

Kama yeye alidhani mimi ndiye niliyemfuata huko PM na kumtukana basi alidhani kimakosa.

Na uzuri ni kwamba angeweza tu kuwaambia mods kuwa katukanwa huko PM na mods wana uwezo wa kuangalia IP address ya mtu na nina uhakika wa 100% kuwa kama waliangalia ili kuona nani ndiye kamtukana hayo matusi huko PM basi waligundua kuwa haikuwa mimi.

As simple as that.
 
Unajua kuna baadhi ya majibu yeye anayaona yako sawa kwa upande wake, ila kwa upande mwingine yanaweza sababisha ukosefu wa utulivu wa nafsi kwa baadhi ha member.

Kivipi yakoseshe ukosefu wa utulivu wa nafsi kwa baadhi ya member?

Kwani kuna mtu nimemtaja humu au kumfunulia faragha yake?

Hebu dadavua kidogo hapo, tafadhali kama hutajali...
 
nimecheka hapa [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Oh yeah...mara nyingi tu.



Kutokuwa huru. Wakati mwingine huwezi kujua kama unachokifanya kinawapendeza au kuwachukiza wenyeji wako mwisho unaishia kuhisi hisi tu na kuanza kujistukia. I hate that.

Usafi wa hiyo sehemu hususan wa bafu, choo, jiko, na vyombo vya mezani kama vijiko, bilauri [sipendi kabisa kunywea maji bilauri za watu]. Nipo radhi nitumie paper plates na vijiko au uma wa plastiki kuliko silverware zao.



Kuwasha tivii na kuangalia nipendacho.

Kufungua jokofu muda wowote na kuchukua chochote kilichomo.

Kuoga navyotaka mimi. Nikiwa hapa kwangu naweza hata kumaliza dakika 45 naoga bafuni.

Kwa watu huwezi kufanya hivyo.

Kufua nako pia. Hapa muda wowote tu naweka nguo kwenye washer na dryer bila hofu yoyote ile.

Kujilaza popote pale...iwe sakafuni..kwenye kochi...kwenye futon....ukiwa kwa watu huwezi kujiachia hivyo.

Hata kwenda haja kubwa nako inabidi uende kwa kuwalia watu timing....sipendi kabisa aisee.

Hapa kwangu nikisikia tu mzigo unagonga hodi naenda bla hofu yoyote ile.

Imagine uko kwa watu halafu unabanwa mavi na choo kiko ndani ya nyumba karibu na jikoni....

Unaingia chooni halafu unashusha mzigo tena ule unaoambatana na makelele...noma sana yaani.

Halafu ukimaliza na kutoka unaanza kuombea asiingie mtu mwingine kabla harufu haijaisha...man...I hate that.
 
Kabisa.
Ila naamini moyo wa madame B hautikisiki kwa mirindimo ya majibu ya hivyo.
Gari bovu linavutwa na gari zima.....siku zote gari bovu halikokoti bovu mwenzie.
Hahahha....kwakweli wala hautikisiki aisee.
 
Kivipi yakoseshe ukosefu wa utulivu wa nafsi kwa baadhi ya member?

Kwani kuna mtu nimemtaja humu au kumfunulia faragha yake?

Hebu dadavua kidogo hapo, tafadhali kama hutajali...
Nikuulize swalii?
 
Back
Top Bottom