Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Nyani Ngabu Ulishawahi kuaibika?
Hahaaa yeah...nakumbuka wakati nipo college...siku moja hivi Ijumaa jioni nikitoka darasani naenda dorm...kuna hallway moja hivi ilikuwa na milango ya vio.
Sasa mimi akili yangu hata sijui ilikuwa wapi siku hiyo...nilipofika hapo kwenye milango mimi nikatembea tu utadhani hakuna milango na matokeo yake nikajibamiza uso hahahaa. Uzuri hakukuwepo na watu wengi ila alikuwepo mchuchu mmoja wa kizungu aliyeniona. Alinicheka sana aisee.
Au ulishawahi kuwa mshamba on something?
Oh yeah...niko mshamba kwenye mambo mengi tu.
Kwa mfano, mwaka juzi tu ndo nimeanza kuwa na smartphone.
Imagine mpaka mwaka 2015 nilikuwa natumia simu kama kitochi....