Uchaguzi 2020 Nyehunge: Dkt. Magufuli amuamrisha Mfugale atangaze ujenzi barabara ya Sengerema-Nyehunge (KM 46) kisha amuulize hela za kujengea

Ipo haja ya kupima akili wagombea wetu wa ngazi ya ubunge na urais, la sivyo nchi itakuja kuingizwa kwenye matatizo makubwa kuliko ambayo yameshatokea
Unajua sasa ni muda gani? Amka sasa kumekucha mkuu maana ndoto zako ni za hatari kwako!
 
Sasa kwaakili za kawaida (usifikiri kiccm) unaona kuna uwanja sawa wa kushindana na vyama vingine vya siasa?
Unayefikiri kuna usawa pole sana, Lissu mwenyewe anajua usawa hakuna kikatiba, na kwa hiyo kampeni za Lissu ni za kutimiza mkakati wa kivuli cha demokrasia nchini na kwa kujua hilo Lissu anapungua gharama za kampeni kwa kuwachangisha michango wananchi!

Siasa ni maisha ya watu, siasa ni biashara za watu na usipojua mchezo huo utaumia sana na huenda ukapoteza maisha halafu wanasiasa wakaendelea kula bata pamoja!
 
Hasikii
 

RUSHWA HADI KWENYE BARABARA. SIKU ZOTE ALIKUWA WAPI? JE ANGEKUWA MGOMBEA MWINGINE AMEAHIDI AU KATOA MABATI YA KUJENGA SHULE, NA KATOA FEDHA ZA UJENZI WAKATI HUU WAKAMPENI ANGECHUKULIWAJE NA HAO TAKUKURU/TUME VIBARAKA WA CCM?
 
Anaendelea kwa mujibu wa nani?Sanduku la kura ndio mwamuzi!
Tunachosema hapa,hilo hitaji la barabara alishaliona ndio maana wakati anaongea akasema wameshafanya feasibility study na vitu kama hivyo!Sasa hiyo kufanya jukwaani ni rushwa,inamaana anawaambia msiponichagua barabara haitajengwa maana pesa najua mimi nitakapozitoa!
Hii ni rushwa ya wazi wazi na haikubaliki kwenye jamii ya wastaarabu!Hatukuwahi kuona mambi haya kipindi cha Mkapa wala kikwete!
 
Hivi Mheshimiwa anajua nini maana ya kampeni za uchaguzi wa Rais? Na pia anatambua nini kinachopaswa kufanyika wakati wa shughuli za kampeni? Na kweli alisoma kwa kina na kuzielewa kanuni na maadili ya wagombea kutokana na tume ya uchaguzi?
Huyo alishasema kuwa yeye ni jiwe na jiwe tangu lini likayumbishwa kwa makelele ya watu?

Mwenye nacho ataongezewa asiekuwa nacho atazidi kunyanganywa.
 
Hivi Mheshimiwa anajua nini maana ya kampeni za uchaguzi wa Rais? Na pia anatambua nini kinachopaswa kufanyika wakati wa shughuli za kampeni? Na kweli alisoma kwa kina na kuzielewa kanuni na maadili ya wagombea kutokana na tume ya uchaguzi?
Hujuw kwamba magufuri ni Rais?? Unakwama wap

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Tumwogope mungu kupinga had maendelei

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Mwenyewe anajiita KICHAA unategemea nini Mkuu? Tume huru wangempiga stop kuhusu uhuni anaoufanya wakutoa ahadi wakati wa kampeni na kuzungumza kisukuma lakini tumeccm HAWATHUBUTU.

Nchi inaendeshwa kama kuku aliyekatwa shingo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…