Uchaguzi 2020 Nyehunge: Dkt. Magufuli amuamrisha Mfugale atangaze ujenzi barabara ya Sengerema-Nyehunge (KM 46) kisha amuulize hela za kujengea

Uchaguzi 2020 Nyehunge: Dkt. Magufuli amuamrisha Mfugale atangaze ujenzi barabara ya Sengerema-Nyehunge (KM 46) kisha amuulize hela za kujengea

Ipo haja ya kupima akili wagombea wetu wa ngazi ya ubunge na urais, la sivyo nchi itakuja kuingizwa kwenye matatizo makubwa kuliko ambayo yameshatokea
Unajua sasa ni muda gani? Amka sasa kumekucha mkuu maana ndoto zako ni za hatari kwako!
 
Sasa kwaakili za kawaida (usifikiri kiccm) unaona kuna uwanja sawa wa kushindana na vyama vingine vya siasa?
Unayefikiri kuna usawa pole sana, Lissu mwenyewe anajua usawa hakuna kikatiba, na kwa hiyo kampeni za Lissu ni za kutimiza mkakati wa kivuli cha demokrasia nchini na kwa kujua hilo Lissu anapungua gharama za kampeni kwa kuwachangisha michango wananchi!

Siasa ni maisha ya watu, siasa ni biashara za watu na usipojua mchezo huo utaumia sana na huenda ukapoteza maisha halafu wanasiasa wakaendelea kula bata pamoja!
 
Hapa ndipo umuhimu wa katiba mpya unapoonekana, kuwa Rais wa nchi halafu hapo hapo kuwa mwenyekiti wa chama cha siasa ni tatizo.

Hapo Magufuli anaamua kutumia kofia yake ya Urais kujinufaisha kisiasa kwenye kampeni zake, hiIi sio sawa.

Hizi bajeti siku zote zinatakiwa kupitishwa na bunge, sio mtu mmoja anajiamulia tu, hii nchi ina sheria na taratibu zake Magufuli akumbushwe kuzifuata.
Hasikii
 
DKT. Magufuli akiwa anaendelea na kampeni za uchaguzi 2020, amepita kijiji cha Nyehunge akiwa anaelekea Geita ambapo kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46. Alisimama kuongea na wananchi waliokuwa wakimsubiri barabarani, wakati anaielezea barabara hiyo ghafla aliomba simu yake na kumpigia mtu ambae baadae alijulikana ni mkurugenzi mkuu wa TANROADS, Injinia Mfugale na mazungumzo yao yalikuwa hivi.

Magufuli: Hallo, Chief executive

Mfugale: Naam mheshimiwa Rais

Magufuli: Hujambo

Mfugale: Sijambo mheshimiwa

Magufuli: Uko wapi?

Mfugale: Niko Dar es Salaam TANESCO tunazungumzia habari ya Nyerere dam.

Magufuli: Haya, sasa mimi niko Nyehunge, kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46, hii barabara tumeshaifanyizia feasibility study na detail design, nimesimama hapa na wananchi, nataka hii barabara, mimi si ndio Rais?

Mfugale: Ndio mheshimiwa(Wananchi kicheko cha furaha)

Magufuli: Nyehunge Oyee, Unanielewa Chief? Basi hii barabara uitangaze kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Huu ni mwezi wa ngapi? (Mfugale: Mwezi wa tisa). Haya uandae document zote kabla ya mwezi wa 12 haujafika na kandarasi apatikane, niulize hela nitazitoa wapi. Sawa Mfugale?

Mfugale: Nimekuelewa mheshimiwa Rais

Magufuli: Umenielewa, mueleze na Waziri kwamba hayo ni maagizo yangu wala yasibadilike, Asante sana.

MWISHO WA MAONGEZI

RUSHWA HADI KWENYE BARABARA. SIKU ZOTE ALIKUWA WAPI? JE ANGEKUWA MGOMBEA MWINGINE AMEAHIDI AU KATOA MABATI YA KUJENGA SHULE, NA KATOA FEDHA ZA UJENZI WAKATI HUU WAKAMPENI ANGECHUKULIWAJE NA HAO TAKUKURU/TUME VIBARAKA WA CCM?
 
Mhh mkuu mwananchi yeye anataka barabara, hajalishi ni uchaguzi au hapana.
Sisi wananchi tunataka haki ya kuwa na barabara na sio sheria ya kuwa na barabara wakati usio wa uchaguzi.Afterall yanini kutumia hesabu mbovu wakati fika yule Magu ataendelea,tunamdanya nani.
Anaendelea kwa mujibu wa nani?Sanduku la kura ndio mwamuzi!
Tunachosema hapa,hilo hitaji la barabara alishaliona ndio maana wakati anaongea akasema wameshafanya feasibility study na vitu kama hivyo!Sasa hiyo kufanya jukwaani ni rushwa,inamaana anawaambia msiponichagua barabara haitajengwa maana pesa najua mimi nitakapozitoa!
Hii ni rushwa ya wazi wazi na haikubaliki kwenye jamii ya wastaarabu!Hatukuwahi kuona mambi haya kipindi cha Mkapa wala kikwete!
 
Hivi Mheshimiwa anajua nini maana ya kampeni za uchaguzi wa Rais? Na pia anatambua nini kinachopaswa kufanyika wakati wa shughuli za kampeni? Na kweli alisoma kwa kina na kuzielewa kanuni na maadili ya wagombea kutokana na tume ya uchaguzi?
Huyo alishasema kuwa yeye ni jiwe na jiwe tangu lini likayumbishwa kwa makelele ya watu?

Mwenye nacho ataongezewa asiekuwa nacho atazidi kunyanganywa.
 
Hivi Mheshimiwa anajua nini maana ya kampeni za uchaguzi wa Rais? Na pia anatambua nini kinachopaswa kufanyika wakati wa shughuli za kampeni? Na kweli alisoma kwa kina na kuzielewa kanuni na maadili ya wagombea kutokana na tume ya uchaguzi?
Hujuw kwamba magufuri ni Rais?? Unakwama wap

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Hapo watahamisha mafungu kutekeleza hilo agizo haramu huku wakiathiri mipango mingine.

Swali la kujiuliza ni je, kama anaagiza hivi hadharani, nyuma ya pazia huwa anaagiza mangapi?

Ni wazi hata Chato Airport imejengwa kwa style hii.

Jambo lingeni la hatari ni kuwa,yeye ana kinga, ila anaowapa maagizo hawana kinga, hivyo wawe makini kwani tawala zinabadilika.
Tumwogope mungu kupinga had maendelei

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Mwenyewe anajiita KICHAA unategemea nini Mkuu? Tume huru wangempiga stop kuhusu uhuni anaoufanya wakutoa ahadi wakati wa kampeni na kuzungumza kisukuma lakini tumeccm HAWATHUBUTU.

Nchi inaendeshwa kama kuku aliyekatwa shingo.
 
Kazi kwelikweli
IMG_20200906_120039.jpg
 
Back
Top Bottom