Nyerere Against Islam in Zanzibar and Tanganyika

Mimi kila nilichoandika kuhusu Nyerere nina ushahidi.
Una ushahidi kwa mujibu wa nani?
Kitabu changu "The Life and Times of Abdulwahid Sykes..." kimechapwa London mwaka 1998.
Kwa mtu anayechunguza mambo, kitabu si tatizo facts are. Suala kuu ni ukweli wa kinachozungumziwa.
Nyerere yu hai na alikisoma.
Sikusuburi afe ndiyo nizungumze habari zake.
Ningefurahi ukaweka na feedback au response yake kuhusiana na tuhuma zako.
Nadhani ushaelewa kuwa uoga si sifa yangu.
Acha sifa zako zionekane na zisemwe na wengine, sio na wewe mwenewe kwa kujipigia chapuo.
Lete jingine kama lipo.

Yapo mengi, ila tuanze na haya/
 

Kwa kawaida mtu mwenye kutukana huwa sijadilinae chochote.
Lakini hii post ya pili imekuja na adabu.

Kuhusu niache wengine wanisemee hili halitowezekana kwa kuwa uleinitukana kuwa mimi ni...ni wewe kwa hiyo siwezi kusubiri mtu mwingine anijibie. Ndiyo nikakujibu uongo si sifa yangu na ndiyo maana hata hapa JF natumia jina langu halisi sijajificha.

Ushahidi ninao kwa kila nilichosema nimeweka ushahidi katika kitabu. Ikiwa wewe unataka ushahidi wa kimahakama katika tafiti ya kisomi hilo sijui tutalifanyaje lakini kama unaweza kuniongoza kwa kunifunza tufanyeje ili upatikane ushahidi kama wa mahakamani kama unavyoainishwa na ''law of evedence'' mimi Insha Allah niko tayari kutoa ushirikiano.
 
Mjadala wa watu waliofilisika mawazo. Siwezi kujadili hisia za mtu!
 
Ningeshangaa kama Mohamed Said asingetia mguu ndani ya hii thread ha ha ha ha ha ha.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said, kwa vile kila siku tunapata ufahamu mpya kuhusu yaliyojiri Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla, ningekuuliza maswali haya mawili:
1. Je, bado unaamini kuwa Okello alitumwa na Wakristo kwenda kufanya mapinduzi ZNZ
2. Je,Nyerere ndiye chanzo cha mapinduzi ya ZNZ

Ningependa unijibu kwa maoni yako na wala si nukuu za kitabu au vitabu kwasababu ninazo na nimezisoma sana.
 
Ningeshangaa kama Mohamed Said asingetia mguu ndani ya hii thread ha ha ha ha ha ha.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Said vipi umekimbia mnakasha? Tunahitaji darsa!!!
 
Mzee Said vipi umekimbia mnakasha? Tunahitaji darsa!!!

Sijakimbia mnakasha ndugu yangu. Tatizo ni kuwa mie siwezi kutukanana sasa inapofika hali ya kejeli na matusi basi huvunjika nguvu.

Insha Allah mimi nipo na hii ilm ni amana na kwa kuwa nyie wenye amana mmekuja kudai amana yenu ni wajibu wangu nirejeshe amana hiyo kwenu.

Insha Allah tutaendelea na darsa kadri Allah atakavyotuwezesha.
 

Umeniuliza swali nami nimelipokea ila sijui kwa nini uaniwekea masharti jinsi ya kujibu.
Inaelekea unaniamini sana kiasi cha kutaka fikra zangu pasi na kufanya rejea za vitabu vya wasomi.

Insha Allah nitajitahidi kujibu.

Okello.

Kwanza hebu ngoja tumuweke pembeni Insha Allah wakati wake utakapofika tutamzungumza.

Ningependa tuanze na watu, sehemu na matokeo muhimu katika mapinduzi ya Zanzibar.

Kulikuwa na kambi Kipumbwi iliyokuwa imewekwa rasmi kwa kuwafunza mamluki wa Kimakonde kutoka shamba la mkonge la Sakura na kwengineko kwenda kuivamia Zanzibar.

Hawa Wamakonde walikuwa wakifanya kazi ya manamba katika mashamba ya mkonge Tanga.

Hawa Wamakonde kutoka Kipumbwi ndiyo waliovushwa kwenda Zanzibar mwaka 1961 kuipigia kura ASP na mwaka 1964 kwenda kupindua serikali ya Mohamed Shamte ambayo ilikuwa ni muungano wa vyama viwili ZPPP na ZNP.

Walioshughulika na kambi hii upande wa Tanganyika walikuwa Jumanne Abdallah aliyekuwa RC wa Tanga, Victor Mkello aliyekuwa kiongozi wa chama cha wakata mkonge na Mohamed Omari Mkwawa kijana wa mjini Tanga aliyepewa kazi ya kuwatia Wamakonde katika kambi na kuwavusha.

Jimmy Ringo mwanachama wa ASP alikuwa Tanga mjini ofisi ya TANU Br. 14 akiratibu operasheni hii yote.
Jimmy Ringo alikuja kuuawa baada ya mapinduzi.

Mauaji mengi sana ya Waarabu siku ya mapinduzi yalifanywa na hawa Wamakonde kutoka Kipumbwi wakiwa na John Okello.

Asikuambie mtu ati mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na ASP na Umma Party ya Abdulrahman Babu.

Swali la kujiuliza ni nani aliruhusu kuwekwa kwa kambi hii hapo Kipumbwi?
 
Sijakuwekea masharti ya kujibu, nisichokitpendelea katika mjadala ni nukuu za maandishi yako ambayo tayari nimeyasoma mara nyingi sana, na nimesoma maandiko ya wanazuoni wengine mara nyingi sana.

Mzee Said, ukiangalia maswali niliyokuuliza bado hujajibu, ulichofanya ni kuzunguka. Maswali yapo wazi kabisa.

1. Je,bado unaamini Okello alitumwa kwenda kufanya mapinduzi Zanzibar

2. Je, Nyerere ndiye chanzo cha mapinduzi (Umeongelea wakata mkonge na wamakonde, ningependa utufahamishe endapo Nyerere aliwatuma au walitumwa na mtu mwingine). Nasema hivi ili mbele ya safari tujue tunamjadili nani na siyo kuzunguka zunguka porini kwa kutaja makundi.
 

sidhani kama wewe ni kati ya author ambao nyerere alikuwa akiwasoma, hii itakuwa ni kashfa kwa nyerere how can such a genius read fools writings such as yours, disgusting.
 
Mohamed Said,
Nadhani unafahamu wazi kuwa unachokieleza kina walakini ndio maana hujibu maswali.
Unafaham kuwa mapinduzi hayakufanywa na Nyerere wala Okello hakutumwa kama unavyowaaminisha watu.

Unafahamu kuwa unahitaji kitu cha ziada kuunganisha ukristo na Nyerere katika hali ya kisiasa iliyopo sasa.
Unafahamu kuwa wanazuoni WZN wamekupinga kwa hoja hizi.

Nimekuuliza maswali very basic na umegundua kuwa mbele ya safari utakwama, kama kawaida umeahirisha mnakasha ili nyuzi nyingine ianzishwe.

Mada hii ni nzuri sana na nilidhani tungekuwa na mnakasha mzuri sana, sidhani kama litatokea hilo.
 
Wanajamvi, kabla ya kueleza jambo nililokusudia nimeiweka makala hii iliyotoka katika gazeti la Rai Mwema tole 227 la tarehe 22 feb 2012 makusudi kabisa.
Mwandishi wa Makala hii ni Ahmed Rajab ambaye hana tatizo la kidini na Mohamed Said litakalo kwaza mjadala.
Mohamed Said atufahamishe haya yafuatayo

1. Je, naye alifanya mahojiano na Wna mapinduzi kama alivyodai mwenzake Ahmed Rajab
2. Je, anaikubali au kuikataa makala hii kwa ukweli au uongo wake?

Kwanza naanza kwa kumnukuu
Mohamed Said; Asikuambie mtu ati mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na ASP na Umma Party ya Abdulrahman Babu


Ni kwa msingi wa maandishi haya Mohamed Said anaweza kutusaidia kubainisha kwa kuyakubali au kuyakanusha.
Mambo mengi aliyosema kuhusu Nyerere na Tanganyika, mwandishi mwenzake Ahmed Rajab ambaye hana ''doa'' ameyakanusha.

Hapa hakuna bias kwasababu wote ni waislam, na wana hulka ya kuishambulia Tanganyika na Nyerere.
Kwanini jambo hili wametofautiana kiasi cha kutiana madole machoni?

Kuna data zaidi zinakuja.
 

Ndugu yangu ni maswali yapi ambayo mimi sijayajibu?
Tafadhali hebu niwekee tena moja baada ya jingine.

Insha Allah nitajitahidi kujibu kama ninayo majibu yake.
 

Ndugu yangu kuhusu kufanya mahojiano na wanamapinduzi wengine kama alivyofanya Ahmed Rajab mimi nimezungumza na baadhi kama alivyofanya Ahmed Rajab.

Siyakanushi maandishi ya Ahmed Rajab ila ninalosema ni kuwa huo ni upande anojua yeye.
Uko upande mwingine ambao yeye huenda haujui kabisa na kwa kweli si wengi wenye kuujua.

Hadi leo ukiwatajia huo upande mwingine wa mwezi watakanusha.
Mimi naelewa kwa nini wanakanusha.

Ni hulka ya binadamu kuiogopa fedheha au kuikubali aibu ya kusutwa.

Upande huu mwingine ulitakiwa usijulikane kabisa.

Nitakuwekea hapa kwa mukhtasari.

Kuna ''connection'' ya Wayahudi, silaha kutoka Algeria ambazo zilipokelewa Tanganyika, kuna jeshi la mamluki wa Kimakonde kutoka Kipumbwi katika mapinduzi ya Zanzibar.

Nitakufahamisha kitu kimoja.
Hadi kufika asubuhi serikali ya Jamshid ilikuwa ishaangushwa.

Makomredi waliingia siku ya pili asubuhi si wao waliopiga pigo la kwanza.
Waliingia asubuhi kucheza ngoma uwanjani mwali keshatolewa ndani na keshapekekwa kwa mumewe.

Hii ndiyo sababu hadi leo hakuna comrade hata mmoja aliyethubutu kunyanyua kalamu
kuandika kuhusu historia ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa kumaliza ningependa kusema kuwa naamini hiyo kauli yako ya ''data'' hukukusudia kunitisha na data
bali ni kunogesha maandishi yako.

La ikiwa kusudio ni kuniwekea vitisho vya data ahlan wasaalan.
Mimi naogopa kitu kimoja tu.

Matusi.

Ama kuhusu hilo la Ahmed Rajab kutokuwa na ''doa'' la dini sijui unakusudia nini khasa.
Kuwa hana mapenzi na Uislam au kitu gani?
 
Nianze kwa kuweka sawa msemo ''hana doa''. Hapa nilimaanisha kuwa angeandika mtu mwingine zaidi ya Mwislam basi ingeshakuwa doa ya kuwa anapindisha historia kuwadhulumu waislam. Yeye ni Mwislam kama wengine na wala sikuongelea uumini wake kwasababu nia ya mja anaijua mwenyezi mungu peke yake.

Mohamed, Mzee Nasor Moyo katika mada zake nyingi amekuwa kifanyia reference ''mimi ni mwanapinduzi'' na pale bwawani mwezi oktoba 2012 aliuliza nani anayajua mapinduzi zaidi yake.

Karume alikuwa na kauli za mapinduzi kama ilivyokuwa kwa jumbe, Mwinyi, Salim, Abdul Wakili, Thabiti Kombo Jecha, Aman Karume, Abdallah Natepe n.k.
Swali hapa ni kuwa je, hawa wote walikuwa vibaraka wa Mwalimu Nyerere?
 
ACHA UWONGO na acha miporojo ya kina mikmunisti ya kuuwa dini!
 
Waislamu pambaneni na adui yenu mkubwa (ujinga) a.k.a kutoliona darasa msitafute majibu mepesi kwenye mambo magumu na yamsingi. poor of you!
 
sidhani kama wewe ni kati ya author ambao nyerere alikuwa akiwasoma, hii itakuwa ni kashfa kwa nyerere how can such a genius read fools writings such as yours, disgusting.

Nadhani ''fools writings'' umekusudia ''fool's writings.''

Juu ya kuwa yanaweza kuwa maandishi yangu ni ya ''mwandishi mjinga'' genius lazima ayasome kwanza ndipo atakapoweza kuyahukumu kama ni ya mtu mjinga.

Kukitazama kitabu tu gamba lake hatoweza kujua kilichomo.

Iwe itakavyokuwa.

Kitabu changu kimepata ''review'' mbili ndani ya Cambridge Journal of African History kutoka kwa mabingwa wa historia
ya Afrika - John Iliffe na Jonathon Glassman kutoka Cambridge University na Nortwestern University Chicago.

Haikuishia hapo ikafuatilia na mialiko kadhaa kutoka vyuo vikuu Marekani na Ulaya.
Nimealikwa Nortwestern University kuzungumza na katika wasikizaji na wauliza maswali alikuwa Prof. Jonathon Glassman.

Haikuishia hapo.

Mwaka jana Abdulwahid Sykes akapewa medali kama mpigania uhuru wa Tanganyika
baada ya kusahaulika kwa miaka 50.

Kitabu kimechangia sana katika kumtambua kuwa yeye ndiye chimbuko la TANU.

Bado.
Kitabu kinakwenda toleo la tatu Insha Allah.

Sasa mjinga nani?
Mimi mwandishi au wasomaji wangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…