Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Nianze kwa kuweka sawa msemo ''hana doa''. Hapa nilimaanisha kuwa angeandika mtu mwingine zaidi ya Mwislam basi ingeshakuwa doa ya kuwa anapindisha historia kuwadhulumu waislam. Yeye ni Mwislam kama wengine na wala sikuongelea uumini wake kwasababu nia ya mja anaijua mwenyezi mungu peke yake.
Mohamed, Mzee Nasor Moyo katika mada zake nyingi amekuwa kifanyia reference ''mimi ni mwanapinduzi'' na pale bwawani mwezi oktoba 2012 aliuliza nani anayajua mapinduzi zaidi yake.
Karume alikuwa na kauli za mapinduzi kama ilivyokuwa kwa jumbe, Mwinyi, Salim, Abdul Wakili, Thabiti Kombo Jecha, Aman Karume, Abdallah Natepe n.k.
Swali hapa ni kuwa je, hawa wote walikuwa vibaraka wa Mwalimu Nyerere?
Sijajua umekusudia nini hapa.
Hii ni taarifa kwangu au unataka niseme kitu?