Mohamed Said,
Nimekuuliza maswali unajitahidi sana kuyakwepa hata hivyo nitaendelea kuuliza tu na umma utaamua
Dec 10 1963 wakati Zanzibar ikipata Uhuru kiongozi wa chama cha Umma Party, marhum Abdurahaman Babu alisema maneno yafuatayo
Salaam kwa Wazanzibari na wapenda haki wote. Umma Party na Wazanzibari kwa ujumla, wanasubiri kunyakua utawala wa nchi na kuuweka mikononi mwao saa itakapowadia''
1. Je, Abdurahaman alikusudia nini? na ni kweli au si kweli aliyasema maneno hayo?
2. Kwa vile umesema Mapinduzi ni pandikizi la Mwalimu Nyerere lililoanzia Kipumbwi hadi siku ''makomredi walipoingia na kumkuta mwali keshaenda kwa bwana'' na kwa ukweli kuwa takriban miaka 48 Zanzibar imekuwa inasherehekea mapinduzi kama itakavyokuwa jumamosi ya Jan 12 2013
a) Ungepata nafasi ya kuongea na WZNZ ungewaambia nini kuhusu siku hiyo kwa upande wa historia uijauayo?
b) Je kuna ulazima wa kuwa na siku hiyo.
3. Kwa vile mapinduzi ni pandikizi la Nyerere na ukristo dhidi ya Uislam visiwani, viongozi wanaojinasibu kama wana mapinduzi unawaweka katika nafasi ipi ya uzalendo katika Zanzibar
Swali la kwanza lingestahili kujibiwa na Babu mwenyewe. Mimi sijui kusudio lake labda nikisie tu.
Swali la pili. Sijatumia neno pandikizi wala Nyerere. Nilichosema ni kuwa makomredi hawakupindua
waliingia kazini siku ya pili.
a) Sina la kuwaambia
b) Huo ni uamuzi wa Wazanzibari wenyewe
Swali la tatu la uzalendo hilo ni swali lijibiwe na Wazanzibari wenyewe
Mzee Said, kwa vile huna majibu na umeamua kwaachia Wazanzibar wayajibu hii maana yake ni kuwa huwezi kutetea unachokisema.
Umeshindwa kutetea unachokisema pengine kwa kutaka kuficha ukweli ukitaka unachosema kionekane ni kweli.
Kama hujui mambo ya ZNZ unapata wapi ushahidi wa kumshambulia Nyerere kuwa kinara na mapinduzi hali ikikan kuwa hayakufanywa na WZNZ?
Nimekuuliza akina Mwinyi, Jumbe, Nasor Moyo na wengine wapo, je ni vibaraka huna jibu.
Nimekuuliza endapo WZN wanapaswa kuyakana mapinduzi, huna jibu.
Sasa kwanini umshambulie Nyerere kwa kusema alipeleka wamakonde kufanya mauaji?
Kinachokuponza Mzee saidi ni kutoa maandiko yenye kulenga kujenga chuki huku ukijua kuwa ima si ukweli au unapindisha ukweli.
Katika Uislam kuna aya ya mwenyezi mungu inayozungumzia juu ya unafiki na manafiki.
Epusha ndimi na kalam yako isije kuwa ni tatizo siku zijazo.
Ahmed Rajab ambaye ana unasaba na Waarab unaosema wameuawa amekana kama walivyokana wanazuoni wengine.
Kuaminisha umma kuhusu ubaya wa Nyerere huku ukishindwa kutamka neno kwa Karume, Mwinyi, Jumbe, Moyo na wanamapinduzi wengine ni double standard ya hali ya juu sana.
Unafahamu kuwa kuwanasabisha na Nyerere utakuwa umekosa lengo lako la kumshambulia Nyerere na ukristo.
Unafahamu namna gani utakavyowaudhi WZN pale utakaposema mapinduzi si halali.
Umebaki kujificha katika maneno ambayo hayalingani na hadhi ya kile unachojisifia nacho.
Hivi Mzee Said, kwani ukiandika historia bila kutumbukiza mbegu za chuki dhidi ya dini nyingine na hasa Nyerere historia hiyo haikamiliki?
Unaposema vitabu vyako havijaweza kuwa challenged wakati huo huo huwezi kutetea hoja zake huoni unajichanganya.
Ushauri wangu, hakuna kitu kibaya kiroho na kimaadili kuongelea jambo usiloweza kulitetea, kulisimamia na kulihakiki.