Nyerere Against Islam in Zanzibar and Tanganyika




By adolay
Bado unaendeleza umbumbu wako kuhusu mwalimu na uchonganishi wa waislam na wakristu

Hebu tusaide nani anahujumu wasomali na uislam wa wasomali? kama tanzania walihujumiwa na nyerere huko somalia anawahujum nani? na mfumo gani umewafikisha hapo walipo hivi sasa.


swali lipovery clear just lete jibu.
 
Mzee Said,
Baada ya hoja yako ya ZNZ kuleta utata kama si kukosa mashiko sasa umerejea katika eneo lako.
Unachokieleza hapa kuhusu dini ndicho ulichokusudia ili kuleta mitafaruku.

Unapozungumzia Nyerere kuwa na mikakati ya kuukandamiza Uislam, hili nalo pia ni kama la ZNZ kwa undani wake.
Unachokifanya hapa ni kutafuta namna ya kumhusisha Nyerere na tuhuma zako. Hilo halina tatizo kwasababu ni mtazamo wakio. Tatizo linaloonekana ni kukwepa ukweli.

1. Baada ya kuonekana Nyerere ni Mkristo wapo walioanzisha AMNUT. Tumekuuliza mara mia moja ni kwanini waislam hawakuunga mkono AMNUT bali kushirikiana na Nyerere katika kuikomboa nchi? Sidhani kama una jibu kwasababu hujawahi kuwa na jibu

2. Baada ya Uhuru, kamati kuu na Halmashauri kuu ya TANU asilimia 99 iliundwa na Waislam. Baada ya kugundua njama zake kwanini hawakumuondoa kwasababu uwezo huo walikuwa nao.

3. Hivi inawezekanje na inaingiaje kwa akili ya mtu timamu kuamini kuwa Nyerere alifanikisha mipango yake bila ushauri wa watu wengine!Mohamed,
Nini ulikuwa mchango wa Kawawa kwa kushirikiana na Nyerere katika dhulma
Nini ulikuwa mchango wa Fundikira kwa kushirikiana na Nyerere katika dhulma
Nini ulikuwa mchango wa Tewa Said kwa kushirikiana na Nyerere katika dhulma
Nini ulikuwa mchango wa (Ali Hassan Mwinyi) waziri katika serikali ya Nyerere katika dhulma

4. Historia haiandikwi wala kufutwa inajidhiri yenyewe. Mchango wa Wapigania uhuru wa nchi hii hauna kipimo katika nafasi yetu ya sasa. Abdul Wahid Sykes kupewa tuzo ni haki yake na taifa linajivunia hilo bila kujali itikadi za kidini.
Familia ya Sykes inapaswa kujisikia fahari kwa kutoa mtu mwenye mchango kwa nchi yetu.

Unapojitokeza na kusema kitabu chako ndicho kimetambulisha na kumpa tuzo, kwanza ni kudharau mchango wa Sykes ambao hauhitaji andiko lako ili utimie. Pili ni kuidhalilisha familia ya Sykes kwasababu unachukua credit kwa kazi usioifanya wewe.

Tatu, ni kuanza kujenga chuki na hisia kuwa kama mtu hajaandikwa katika kitabu basi mchango wake kwa taifa hili ni mdogo.
Tarehe 26 Dec 2012 Mwalim John Keto alitutoka. Huyu ni Mwalimu kama wengine ambaye ametoa viongozi wa ngazi ya kitaifa wasiopungua 50( I mean PM, majaji n.k.), je tunahitaji kuandika kitabu ili mchango wake uwe halali!

Nakushauri ukijenga hoja basi zijenge kama wewe Mohamed na si Waislam.
Udhaifu au nguvu za hoja zako zibaki kwako na si kwa Waislam wote.

Hili litasaidia hasa nyakati hoja zako zinapokuwa dhaifu sana.
Na mwisho maoni yako yabaki kuwa maoni na si kuayafanya ni facts ili kuinusuru jamii na hoja za mtu mmoja.
 
Mohamed said

Tunataka kujuwa wewe unasema Tanzania waislamu wamehujumiwa na Nyerere kupitia mfumo kristo sasa tueleze

1. Nani amewahujumu wasomali na uislamu wao?

2. Ni mfumo gani umewafikisha hapo walipo

a) Mfumo kristu

b) Mfumo islam

c) hufahamu

Tukijadili matatizo na maafa ya utawala wa wasomali tutahamia Syria, Libya, Afghanistan, Pakistan, DRC, Lebanon, nk

1. Tutaangalia nani amewahujum/aliwahujumu- nyerere au nani

2. Tutaangalia pia katika nchi hizo ni mfumogani unaotawala Kama ni mfumo kristo au Mfumo Islam na kwanini wawe na matatizo.

3. tutaangalia ukweli wa hoja ya mfumo kristo tukiangazia

a) Utawala wa watanzania tangu uhuru mpaka sasa na matumizi ya madaraka na maamuzi

b) mantiki ya uchinjaji wanyama na uitikio wa wakristu wote kwamba mwislamu ndiyo anauhalili wa kuchinja bila manung'uniko na
yoyote.

Tuanze na la somalia
 
Hakuna hoja kwa sasa. The best thing is tanzanians to think about future. Je Karume alisimu lini kama Mapinduzi ya Zanzibar yalilenga kuuondoa uislam. Hatuhitaji kuongopewa Kwa sasa
 

Endeleeni kushikilia misimamo ya dini mikidhani itawasaidia lkn hakika itawafanya kuwa wakimbizi ndani ya nchi yenu ndogo, kwani dini yako inakusauduaje kuwa bora kuliko mwenye dini nyingine? Unae msema Mwalimu Nyerere juu ya dini ww ndo mwanzo wa matatizo ya dini, hakika ukifuga chui, ukadhani hatakuja kukuma ww au mwanao, endelea kwani kushikilia dini mwisho ni utengano usio na maana yyt ktk jamii.
 
Mohamed said

Naenda kulala, Endelea na mkuu Nguvi3 katika mjadala naona anakusubiri umpe majibu sahihi kwa hoja zake sio porojo.

Kusu swali langu la somalia weka majibu sahihi nitarejea kesho kwa ufafanuzi.

Na mwisho siyovema kupandikiza chuki na kuiteteresha jamii ya watanzania kwa hoja za hovyo, uzushi na uchochezi.

Watanzania wanahitaji amani na upendo zaidi ya kitu kingine chochote bila kujali imani zao.
 
Kwa kawaida mtu mwenye kutukana huwa sijadilinae chochote.
Nimekutukana wapi? thibitisha hili kwanza. Pili sikumbuki kuomba mjadala na mtu yeyote, maana niko bize kukimbiza shilingi, sipo hapa kupiga propaganda ili mkono uende kinywani. Tuelewane ktk hili kwanza.
Lakini hii post ya pili imekuja na adabu.
Huo ni muono wako, I would care less if u do or don't see it that way.
Kuhusu niache wengine wanisemee hili halitowezekana kwa kuwa uleinitukana kuwa mimi ni...ni wewe kwa hiyo siwezi kusubiri mtu mwingine anijibie.
Narejea tena, thibitisha nimekutukana wapi? Hakika muungwana husubiri wengine wathibitishe sifa zake, lakini kwa mtu aso busara huona anachelewa. Huu ni mtazamo wangu.
Ndiyo nikakujibu uongo si sifa yangu na ndiyo maana hata hapa JF natumia jina langu halisi sijajificha.
Kama nilivosema awali, muungwana husubiri watu wathibitishe sifa zake. Suala la wewe kutumia jina lako 'halisi' it is your personal choice, has nothing to do with facts and ultimate truth of your claims.
Ushahidi ninao kwa kila nilichosema nimeweka ushahidi katika kitabu.
Kama maandishi ya kitabu can be substituted as evidence, nazidi kuelewa zaidi kiwango cha uelewa wako. Nahisi kwako kitu kisichoandikwa basi hakina ukweli na kila kitabu ni ushahidi. Unajianika.
Narejea tena kukusihi, utuletee response ya Mwalimu Nyerere baada ya kukisoma hicho kitabu chako. Huenda ikatoa mwanga kwa sisi wengine.
 

Umeandika mengi sitaweza kujibu yote kwa sasa.
Tuanze na uandishi wa historia ya TANU halafu Insha Allah tunaweza kuingia huko kwengine:

Abdulwahid alirudi kwenye ofisi za TANU makao makuu; kwenye ofisi yake ya zamani aliyokuwa akiitumia kama rais wa TAA. Nyaraka zake binafsi, za baba yake nyingine kuanzia mwaka wa 1929 wakati wa enzi za African Association zililetwa pale kwa utafiti kama ushahidi wa yale yaliyopitika zama hizo.

Maelezo ya Abdulwahid katika kuanzishwa kwa Africa Association inasemekana hayakumpendeza Nyerere, kwa kuwa mwanzo wa harakati dhidi ya ukoloni jina la baba yake Abdulwahid, Kleist Sykes, lilikuwa likitawala. Halikadhalika ilipofika kueleza namna TAA ilivyokujabadilishwa kuwa TANU watoto wake wote watatu Abdulwahid, Ally na Abbas wakiongozwa na kaka yao mkubwa Abdulwahid halikadhalika likawa linatawala harakati zile.

Historia hii inasemekana haikumpendeza Nyerere na baadhi ya viongozi wa TANU. Haukupita muda Abdulwahid akatambua kuwa viongozi wapya walioshika nafasi katika TANU kwa kweli hawakuwa na nia hasa ya kutafiti na kuandika historia ya Tanganyika bali nia na azma yao ilikuwa ni kumjenga Nyerere na kumkuza kwa sifa ambazo hazikumstahili. Abdulwahid alipong'amua hili haraka akajitoa katika kazi ile.

Hata hivyo Dr Kleruu aliendelea na utafiti na akaandika historia ya TANU. Historia hii iansemekana ilifuta mchango mzima wa akina Sykes katika kuunda TAA na baadae TANU. Hata hivyo baada ya kazi hii kukamilika haikuchapishwa na ikabaki katika maktaba ya TANU, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.

Lakini baadae kazi ile ilitoweka
...
 

Naomba nikuulize hivi:

1. Nitajie nchi moja tu duniani ya Kiislamu ambayo ni nchi ya amani na haina umwagaji damu (machafuko) ya kidini au kisiasa.
2. Je, nchi za Kiislamu zenye machafuko na Nyerere alitawala huko au kuna Mkristo anayetawala huko?
3. Kama dini yenu ni ya amani mbona nchi ambazo waumini wake walio wengi ni Waislamu ndizo pia zinaongoza kwa vurugu?
4. Jana nilikuwa nasikiliza mhadhara fulani kwenye CD kati ya Waislamu na Wakristo na kwenye mhadhara huo kila mara mwenyekiti alikuwa akiwatuliza Waislamu waache vurugu (watoe nafasi ili Wakristo nao waseme kama wao wanavyosema na kusikilizwa bila kufanyiwa fujo) na kila mara ilikuwa inachukua muda mrefu kuwatuliza na hivyo dakta zilizokuwa zimepewa Wakristo kufidiwa tena. Mbona kila mara kwenye mihadhara ya namna hii inaonekana waumini wenu wanakosa uvumilivu? Ni sehemu ya mafundisho yenu?
 

Unakusudia vipi kusema kuwa nchi ya uislam? Je umekusudia dola ya kiislam? Kama ni dola ya kiislam basi hakuna duniani nzima ndio mana kila kona kuna fujo tu, sio nchi za syria tu na kwengine hata nchi za wazungu nao zinavurugu, tena wao ndo wakubwa hasa, hebu chungulia world war 1 na 2 walioshiriki ni kina nani? Naomba unijibu

Naendelea na kipengele chako sasa cha kwanza, kama umekusidia nchi ya waislam kwa maana ya kuwa na waislam wengi, basi mfano mzuri kuliko yote ni nchi ya oman, hakuna vurugu, lakini sio oman peke ake, UAE nayo iko salama sana tu..... Tatizo sio uislam, tatizo ni hii mifumo ya utawala ya kikafiri, eti demokrasia, dictatorship, monarchy, totalitarian, anarchy (kama somali) hii mifumo ni ya kikafiri ndio maana kutwa ugomvi na vurugu! HUWEZI KABISAAAAAA KUULAUMU UISLAM, huwezi kusema eti Syria mbona waislam lakini vuruguso it means uislam vurugu la hasha ndugu, kwanza tizama tatizo lao ni nini hao wasyria? Ni Assad, haya Assad amewekwa kwa mfumo gani? Hili nakuachia ujijibu mwenyeo!

Mfumo wa uongozi katika uislam ni wa Ukhalifa, huo ndio mfumo ambao ingeweza ukaleta lawama za kuulaumu uislam.....
Lakini uongozi wa kikafiri ndo huzalisha yote! Au wewe unaona mifumo nlokutajia ni ya uislam? Ni kina nani wameileta? Ebu nijibu basi ili nijue uelewa wako umefikia wapi kati ya kutenganisha uislam na matukio yanayotokea.

Mana kama unakumbula juzi UK kulikua na fujo kubwa sana, sasa tukisema ukiristo dini ya fujo tutakua tumefanya haki kweli?

Kidogo chuki zako weka pembeni japo kidogo tu ili ukweli uujue, wewe hujiulizi mbona katika tawala za makhalifa wawili wa mwanzo wa uislam ulikua stable na hakukua na resistance?
 
Mimi nawashangaa sana awa watu, eti mtu akiongea ukweli ni mdini,hivi nini maana ya udini?
 

Nilikuahidi kuwa kwa kuwa umeuliza maswali mengi Insha Allah nitajitahidi kukujibu kwa taratibu.

Soma ndugu yangu habari za AMNUT. Kumbuka kuwa AMNUT ilikuja baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu ambapo baadhi ya Waislam walihisi kuwa Nyerere alikuwa anawaleta jamaa zake wa Kikristo katika TANU kujitayarisha kuchukua madaraka uhuru utakapopatiakana. Ili uelewe kwa nini AMNUT ilikuja ni lazima ujue kisa cha Kura Tatu. (Nimeandika kitabu, ''Uamuzi wa Busara,'' Abantu Publications 2007, Dar es Salaam kisa kizima cha Kura Tatu kimo mle).:

Mwaka 1959, Ramadhani Mashado Plantan, mhariri hodari wa gazeti la Zuhra wakati mmoja gazeti hili likiwa ndiyo sauti ya TANU na wananchi wa Tanganyika, pamoja na kikundi kidogo cha Waislam akiwemo Saleh Muhsin walijiuzulu kutoka TANU na kuunda chama chao cha upinzani, All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT).[1]

Wanachama wengine waasisi walikuwa Abdallah Mohammed ambaye alichaguliwa kuwa rais na Plantan akiwa katibu. Plantan alijitolea chumba kimoja nyumbani kwake Kirk Street, Gerezani kama ofisi ya kwanza ya AMNUT.

Mara tu baada ya kuundwa kwa AMNUT, ulizuka mgogoro katika uongozi na ofisi hiyo ilibidi ihamishwe kutoka nyumbani kwa Plantan hadi Libya Street, eneo lenye Wahindi wengi katikati ya mji. Uongozi mpya ulikuja madarakani na katibu mpya Abduwahid Abdulkarim. Abduwahid Abdulkarim, kijana mwenye umri wa miaka 25 alichaguliwa kuchukua nafasi ya Plantan.

Abdallah Mohamed alibakia na cheo chake kama rais. AMNUT haikuweza kumudu kodi ya nyumba katika eneo lile la matajiri wa Kihindi. AMNUT ikaihamisha ofisi yake na kwenda Kariakoo, Narungíombe Street, karibu na msikiti wa Sheikh Idris bin Saad.


Lengo kuu la AMNUT lilikuwa ni kulinda haki na maslahi ya Waislam ambayo ilikuwa ikihisi yalikuwa hatarini katika serikali iliyoshikiliwa na Wakristo. Abdulkarim alikwenda Tabora kujaribu kutafuta kuungwa mkono AMNUT lakini matokeo yalikuwa ya kukatisha tamaa. Abdulkarim alichagua Tabora kwa sababu ilikuwa mahali penye athari kubwa ya Uislamu.

Hata hivyo Abdulkarim alifanikiwa kupokea mwaliko kutoka kwa Ali Muhsin Al Barwani kiongozi wa Zanzibar Nationality Party (ZNP) ahudhurie mkutano wa kamati kuu na awakilishe suala la AMNUT. Mkutano huu ulifanyika katika ofisi ya ZNP Darajani huko Zanzibar.

Ali Muhsin alimwambia Abdulkarim kwamba ZNP haiwezi kujifungamanisha na tatizo la Uislam kwa sababu ZNP haikuwa inaamini kama Ukristo una uwezo wa kuhatarisha Uislam hasa ukichukulia kuwa Waislam ni wengi nchini Tanganyika. Waislam wa Tanganyika walikataa kuiunga mkono AMNUT wakihisi sera zake zilikuwa za kuwagawa watu kwa misingi ya dini. Kwa ajili hii basi AMNUT haikuwa na maslahi ya wananchi.


Lakini pigo kubwa kwa AMNUT lilikuja kutoka kwa masheikh wa Tanga. Masheikh na waalimu wa Qur' an mjini Tanga walitia sahihi azimio la pamoja kuipinga AMNUT. Azimio hilo lilisema kuwa AMNUT ingezua janga. Masheikh walisisitiza kwamba wataiunga mkono TANU mpaka uhuru upatikane kwa sababu wana imani na malengo yake.[1]

AMNUT ikikabiliwa na mashambulio kama hayo kutoka tabaka ambayo ilidai inawakilisha maslahi yao, chama hicho hakikuweza kustawi. Haukupita muda mrefu AMNUT ikafa.

Mwaka 1960, Plantan sasa akiwa nje ya AMNUT na siasa, alitoa kauli moja iliyokuwa kama anatoa buriani kuteremsha pazia na kuaga jukwaa la siasa.

Plantan aliwaambia Waislam kwamba hata kwa miaka mia moja hawataweza kuwafikia Wakristo. Baada ya kauli hiii hakuna kilichosikika kuhusu Ramadhani Mashado Plantan. Aliishi miaka ya mwisho ya maisha yake hapo Gerezani, akitumia wakati wake baina ya nyumba yake na msikiti wa jirani ambao alikuwa akiufagia kuuweka safi akisubiri mauti yaje akasimame mbele ya haki.


Nyerere alikubali ukweli kuwa kulikuwa na upogo baina ya Waislam na Wakristo hususan katika elimu ambayo itawazuia Waislam kushika nafasi za uongozi katika serikali ya wananchi. Nyerere aliwaomba Waislam waweke matumaini yao kwa TANU ambayo itaanzisha mabadiliko ya lazima kuwainua Waislam kwenye nafasi za usawa pamoja na Wakristo mara tu uhuru utakapopatikana.

Lakini hili, Nyerere aliwakumbusha Waislam mara kwa mara kuwa linaweza kufanyika tu kwenye Tanganyika huru na siyo chini ya utawala wa Kiingereza. Waislam katika TANU, kwa upande wao, waliamini kwamba ilikuwa kinyume kwao kuanzisha chama cha kisiasa chini ya maslahi ya kikundi kimoja kama ndiyo lengo la kudai uhuru.

Hili, wengi waliamini, lingesaidia kuunda vikundi vingi na kusababisha mfarakano. Kwa kweli madai yaliyokuwa yakitolewa na AMNUT hayakuwa madai ambayo yangetolewa kwa TANU katika wakati ule. Vita vya mwaka 1947 kati ya India na Pakistan vilivyosababisha kupoteza maisha ya watu wengi, vilikuwa bado vinakumbukwa na watu wengi.

Chanzo cha ugomvi huo kilikuwa ushindani baina ya Waislam na Wahindu. Kabla ya mwaka 1947 India na Pakistan zilikuwa nchi moja chini ya ukoloni wa Mwingereza. Waislam na Wahindu walipigania uhuru pamoja na walifarakana mara tu ilipokuwa wazi kuwa Uingereza ingetoa uhuru kwa India.

Watu wengi nchini Tanganyika walihofia kwamba kuruhusu fikra kama zile zilizotolewa na Sheikh Takadir kuota mizizi kulikuwa kukaribisha ile hali ya India na Pakistan Tanganyika. Nyerere alionya kuwa hakutaka hali kama ile ije kuisibu Tanganyika.
 

Na hao waliouweka huo mfumo wa ukafir ni Waislamu au Wakristo?
 

the good thing is all of the false allegations against Nyerere can only be written and spoken but they can not be shown because they do not exist, haroub was a muslim and islam forces people to believe without questioning, do you expect him to come with different opinion after reading his fellow muslim gutter level writings?
 

can you prove which quranic verse proves that ALI is an islamic name? una akili ndogo sana dogo kama JK, names has nothing to do with religion but tribes, we ni mjinga dunia haijapa kushuhudia mpaka utakapo kufa. so huyo mungu wenu angeshusha huo upuuzi kwa mtu wa kabila ingine let say m.k.w.e.r.e kwa hiyo yule mpenzi wangu m.k.w.e.r.e anaekwenda kwa jina la HATUJUANI, mimi huwa nalifupisha namuita HATUJU, kwa hiyo HATUJU lingekuwa jina la kiislamu? very stupid.
 

Ikiwa umeingia humu kwa nia ya kutukana na kuonyesha ujuvi utabaki hivyo hivyo na kiburi na matusi.

Lakini ikiwa umeingia humu kwa nia ya kupanua elimu yako nafasi iko tele ya wewe kufaidika.

Juu ya matusi nina wajibu wa kukuelekeza.
Inaelekea hujasoma historia ya Vita Vya Maji Maji.

Ungesoma kuhusu vita ya Maji Maji usingekuja na hoja hiyo ya jina.

Hebu tuanze darsa hapa chini:

Uislam dhidi ya ukoloni na Ukristo una historia ndefu. Ukristo ukawa kama kibaraka ukijikurubisha na kujinasibisha na ukoloni hata Wakristo kupigana vita pamoja na wakoloni dhidi ya majeshi ya wazalendo katika vita vya Maji Maji mwaka 1905. [1]

Kuelewa hali ya Uislam wakati ule, unahitaji kusoma barua iliyoandikwa na Chifu Songea bin Ruuf wakati alipokuwa akikusanya nguvu za raia wake dhidi ya majeshi ya Wajerumani na huku akijaribu kupata ushirika wa machifu wengine katika sehemu za kusini ya Tanganyika na ngíambo ya Mto Ruvuma katika Msumbiji. Barua hii aliyoandikiwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:


''Sultan Songea bin Ruuf anasema: Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga. Asalaam Aleikum, Ninakuletea barua kupitia Kazembe. Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini. Tupo katika kupigananao hapa. Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano. Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea. Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).


Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu. Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa. Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe. Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.

Chupa hii, na daíwa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita. Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.

Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.

Hassan bin Ismaíil anakusalimu.
Salam nyingi,''

Sultan Songea bin Ruuf. [1]
 


sijakataa kama Songea hakuwa muislamu, nachosema ALI sio jina la kiislamu ni jina la kiarabu, kama wewe una ushahidi kuwa ALI ni jina la kiislamu leta ushahidi wa maandiko kuwa ALI ni jina la kiislamu. Niko na dada yangu naemfuata anaitwa Amina ni mkristo ila wazazi walimpa jina la kiarabu. kuhusiana na hiyo barua nafikiri ungeiscan ukaibandika hapa sio unatunga maneno unapachika kwenye mtandao eti ilikuwa barua ya sheikh wa vita ya majimaji. ni kawaida kwa wakristo kujipendekeza kwa wazungu kama ilivyo kwa waislamu kujipendekeza kwa waarabu, na hili huwa unalithibitisha mwenyewe kuwa mapinduzi ya zanzibar yalifanywa na wakristo wakati waislamu watumwa weusi chini ya sultani wakiwa hawana tatizo na ubwana wa sultan juu yao.
 

Hivi kweli unategemea mimi niingie na wewe katika mjadala wa sampuli hii?
Hapana haja.

Hatuwezi kupata tija wala wanaukumbi hawawezi kunufaika.
Muhimu kwako katika ile post ni kuwa na tabia njema.
 
Nyerere ni kweli alikuwa mdini sana, hata ukichunguza kwa umakini utagundua vita ya Kagera ilisukumwa sana na udini!,
Na si kweli kuwa hapa TZ waislam na wakristo wanaishi kwa amani NO NO NO sema tu wakristo kwa asili ni waoga ila wanachuki mbaya sana dhidi ya uislam , mi binafsi kabla sijasilimu nilikuwa hivyo hivyo na tulikuwa tufundishwa kuuchukia na kudharau UISLAM!
Mahali popote pale duniani ukiona hakuna amani basi UKRISTO unatafuta njia ya kujipenyeza, mfano SOMALIA ilikuwa 100% ni waislam lakini baada ya miongo 2 ya vita sasa kunakadiriwa Wasomali wakristo 2,000 na zaidi. Tafakari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…