Nyerere alifanya uhamishaji wa watu mkubwa kabisa katika Afrika?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Inasemekana kuwa kuhamisha watu waishi kwenye vijiji vya ujamaa ndiyo uhamishaji wa watu mkubwa zaidi kuwahi kutokea Africa. Inasemwa kuwa katika miaka minne, toka 1974 hadi 1977 watu milioni 11 walihamishiwa kuishi kwenye vijiji vya ujamaa.

Inasemwa kuwa moja ya matokeo ya jambo hilo ni kugeuza nchi ambayo ilikuwa ni muuzaji mkubwa wa mazao nje ya nchi, hadi kuwa yenye njaa inayotegemea misaada.
 
Sahihi kabisa.

Na yako mengine mengi ambayo yakisemwa watu wanapotezwa, lakini Ukweli una tabia ya kutopenda kudharauliwa, kupuuzwa au kufichwa; una tabia ya kufika na kujitokeza pasipotarajiwa, una tabia ya kushinda kila hila na vita dhidi yake NO MATTER WHAT.
 
Inasemekana kuwa kuhamisha watu waishi kwenye vijiji vya ujamaa ndiyo uhamishaji wa watu mkubwa zaidi kuwahi kutokea Africa. Inasemwa kuwa katika miaka minne, toka 1974 hadi 1977 watu milioni 11 waliamishiwa kuishi kwenye vijiji vya ujamaa.

Inasemwa kuwa moja ya matokeo ya jambo hilo ni kugeuza nchi ambayo ilikuwa ni muuzaji mkubwa wa mazao nje ya nchi, hadi kuwa yenye njaa inayotegemea misaada.
Na ndio kosa kubwa kabisa kuliko yote aliyofanya Nyerere,ingawa alikuwa na dhamira nzuri tu.

Watu walilazimika kuishi mazingira wasioyajua tofauti na waliyokulia ivyo kuathiri uzalishaji uliosababisha umaskini mkubwa.

Lakini mengi mazuri alifanya ivyo tunamkumbuka kwa vile angalau yeye ana nafuu kuliko hawa watawala wa sasa.
 
Inasemekana kuwa kuhamisha watu waishi kwenye vijiji vya ujamaa ndiyo uhamishaji wa watu mkubwa zaidi kuwahi kutokea Africa. Inasemwa kuwa katika miaka minne, toka 1974 hadi 1977 watu milioni 11 waliamishiwa kuishi kwenye vijiji vya ujamaa.

Inasemwa kuwa moja ya matokeo ya jambo hilo ni kugeuza nchi ambayo ilikuwa ni muuzaji mkubwa wa mazao nje ya nchi, hadi kuwa yenye njaa inayotegemea misaada.
Na ndio kosa kubwa kabisa kuliko yote aliyofanya Nyerere,ingawa alikuwa na dhamira nzuri

Watu walilazimika kuishi mazingira wasioyajua tofauti na waliyokulia ivyo kuathiri uzalishaji uliosababisha umaskini mkubwa.

Lakini mengi mazuri alifanya ivyo tunamkumbuka kwa vile angalau yeye ana nafuu kuliko hawa watawala wa sasa.
 
Lakini kwa upande mwingine Kulikuwa na faida, Maana kabla watu hawajaamishwa kwenda kwenye vijiji vya ujamaa watu waliishi kulingana na koo zao hii ingetuletea shida Leo.Vijiji vimesaidia socialization.Unaenda kijiji chochote ndani ya Nchi hii unafanya maisha bila kuulizwa wewe ni koo gani.Tuangalie na upande wa pili wa shilingi.
 
urbanization ya sasa ni nini kama sio modern vijiji vya ujamaa ?

It cheaper kwa huduma per unit area watu wakiwa karibu karibu kuliko kila mtu mmoja mmoja (mbali mbali)

Implimentation ilikuwa mbovu ila urbanization na miji ya sasa ndio hivyo hivyo tu vijiji ambavyo ni miji
 
Inasemwa na nani? Muache Mwalimu.
Inasemekana kuwa kuhamisha watu waishi kwenye vijiji vya ujamaa ndiyo uhamishaji wa watu mkubwa zaidi kuwahi kutokea Africa. Inasemwa kuwa katika miaka minne, toka 1974 hadi 1977 watu milioni 11 waliamishiwa kuishi kwenye vijiji vya ujamaa.

Inasemwa kuwa moja ya matokeo ya jambo hilo ni kugeuza nchi ambayo ilikuwa ni muuzaji mkubwa wa mazao nje ya nchi, hadi kuwa yenye njaa inayotegemea misaada.
Inasemwa na nani? Pili elewa kwamba Mwalimu alikuwa anajenga taifa. Hakukuwa na Taifa zaidi ya koo za kikabila. Karagwe chiefdom, kina Marealle, Usambara, Unyenyembe nk. Hawa machifu na watemi walikuwa na Tawala ndogo za koo. Ilibidi Mwalimu azivunjilie mbali.

2. Hii nchi kubwa sana. Ilibidi kuweka watu karibu ili kupeleka huduma za kijamii. Vijiji vya Ujamaa vilikuwa na maendeleo makubwa mno. Miradi, ujenzi wa nchi pia ulikuwa kwa pamoja.

Ktk utekelezaji wa mipango mikubwa changamoto za hapa na pale ni kawaida. Kikubwa Mwalimu alijenga Taifa kwa maana ya Taifa kuliko kiongozi yeyote Afrika.
 
Ni kweli kabisa aisee tena tunapaswa kuwafanyia uhakiki na kuwarudisha makwao! Kama Wakenya hapa kwao ni jirani kabisa!
 
Lakini kwa upande mwingine Kulikuwa na faida, Maana kabla watu hawajaamishwa kwenda kwenye vijiji vya ujamaa watu waliishi kulingana na koo zao hii ingetuletea shida Leo.Vijiji vimesaidia socialization.Unaenda kijiji chochote ndani ya Nchi hii unafanya maisha bila kuulizwa wewe ni koo gani.Tuangalie na upande wa pili wa shilingi.
Kwahiyo kungetokea u-ukoo, na lingekuwa jambo hatari? Sikubaliani na sababu yako. Maana hadi leo unaenda kwenye vijiji na hata wilaya nzima unakuta watu wa kabila moja, lakini ukabila ni kama haupo. Kutokuwa na ukabila(U-ukoo) hakuhusiani na kutengenezwa kwa vijiji vya ujamaa.
 
Inasemekana kuwa kuhamisha watu waishi kwenye vijiji vya ujamaa ndiyo uhamishaji wa watu mkubwa zaidi kuwahi kutokea Africa. Inasemwa kuwa katika miaka minne, toka 1974 hadi 1977 watu milioni 11 waliamishiwa kuishi kwenye vijiji vya ujamaa.

Inasemwa kuwa moja ya matokeo ya jambo hilo ni kugeuza nchi ambayo ilikuwa ni muuzaji mkubwa wa mazao nje ya nchi, hadi kuwa yenye njaa inayotegemea misaada.

MZEE MWAMWINDI TOKA IRINGA ALIPINGA KWA VITENDO, OPERATION YA ZA KIJAMAA..... AMBAPO ZILIKUWA ZINAWABEBA WAVIVU....UJAMAA ILI UFANIKIWE UNAHITAJI WOTE MUWE NA "IMANI KALI" NA IMANI SIYO YA KULAZIMISHA....IKIKOSEKANA KWA BAADHI NA MKAAMUA KULAZIMISHA.....MADHARA YAKE MAKUBWA NA YANAYOKATISHA TAMAA KWA WALIOJITOA ZAIDI.....HIVYO ULIFELI....WALIOJITUMA NA KUPATA WALINYANG'ANYWA VIKAWA VYA UMMA .....WALE WAKAKATA TAMAA NA KUSONONEKA HATA KUFA KABISA ILI KUBEBA WAVIVU.........HII ILIWASUMBUA SANA WAKULIMA WAKUBWA MKOANI IRINGA-ISIMANI AMBAO WALIPASUA MISITU KWA JITIHADA ZAO NA KUWEZA KULISHA MAHINDI NDANI NA KUUZA NJE....BAADAE SERIKALI IKAPOLA NA KUSEMA YAWE MASHAMBA YA UJAMAA, NI DHURUMA YA JASHO LA WATU....MKUU WA MKOA WA IRINGA DR. KRELUU ALISIMAMIA OPERATION HII ILIPELEKEA KIFO CHAKE BAADA YA KUMFANYIA HARASSMENT MKULIMA MZEE MWAMWINDI, NAYE ALIGADHABIKA NA KUFEDHEHEKA SANA...BILA KUJITAMBUA AKAMPIGA RISASI NA KUMWUA KABISA...KISHA KUBEBA MAITI YA MKUU WA MKOA TOKA ISIMANI NA KUENDESHA GARI YA MKUU WA MKOA YEYE MWENYEWE MPAKA CENTRO POLICE IRINGA MJINI NA KUWAKABIDHI POLICE MWILI NA YEYE KUSWEKWA NDANI....BAADAE KESI YAKE IKAENDESHWA FASTA FASTA .....NYERERE ALIHAKIKISHA JAMAA ANAPATIKANA NA HATIA KWANI ALIFANYA JUU CHINI MZEE MWAMWINDI ASIPATE MAWAKILI WA KUMTETEA....IKUMBUKWE WAKULIMA WENZAKE MWAMWINDI WALIFANYA MPANGO WA KULETA MAWAKILI TOKA MAREKANI NA ULAYA ILA NYERERE AKAWAFUNGA MAHABUSU WAKULIMA WALE KWA KUWATAWANYA MAHABUSU TOFAUTI NCHINI ILI KUMKOMESHA MWAMWINDI AMBAYE ALIHUKUMIWA KUNYONGWA HUKO DODOMA....SO SAD
 
Inasemwa na nani? Muache Mwalimu.

Inasemwa na nani? Pili elewa kwamba Mwalimu alikuwa anajenga taifa. Hakukuwa na Taifa zaidi ya koo za kikabila. Karagwe chiefdom, kina Marealle, Usambara, Unyenyembe nk. Hawa machifu na watemi walikuwa na Tawala ndogo za koo. Ilibidi Mwalimu azivunjilie mbali.

2. Hii nchi kubwa sana. Ilibidi kuweka watu karibu ili kupeleka huduma za kijamii. Vijiji vya Ujamaa vilikuwa na maendeleo makubwa mno. Miradi, ujenzi wa nchi pia ulikuwa kwa pamoja.

Ktk utekelezaji wa mipango mikubwa changamoto za hapa na pale ni kawaida. Kikubwa Mwalimu alijenga Taifa kwa maana ya Taifa kuliko kiongozi yeyote Afrika.
Aliwaleta watu kwenye vijiji vya ujamaa ili walime kwenye mashamba ya ujamaa na aweze kuwatoza ushuru vizuri. Nyerere siyo muanzilishi wa collectivization, aliiga tu, Ilianza huko Urusi, Ikaenda China. Kote huko ilifeli vibaya na kutumbukiza nchi hizo kwenye njaa. Hata hapa ikatutoa kuwa wauza chakula hadi wenye njaa wanaotegemea misaada.
 
Alaumiwe Mao wa China kukubali kujenga reli ya tazara maana amerika ilivosema tunajenga condition mgodi wamara utalipa Deni ,mzee akaona iwavyo na iwavyo mgodi hapana pamoja na hivyo chamana hakuna tunapata toka migodini
 
MZEE MWAMWINDI TOKA IRINGA ALIPINGA KWA VITENDO, OPERATION YA ZA KIJAMAA..... AMBAPO ZILIKUWA ZINAWABEBA WAVIVU....UJAMAA ILI UFANIKIWE UNAHITAJI WOTE MUWE NA "IMANI KALI" NA IMANI SIYO YA KULAZIMISHA....IKIKOSEKANA KWA BAADHI NA MKAAMUA KULAZIMISHA.....MADHARA YAKE MAKUBWA NA YANAYOKATISHA TAMAA KWA WALIOJITOA ZAIDI.....HIVYO ULIFELI....WALIOJITUMA NA KUPATA WALINYANG'ANYWA VIKAWA VYA UMMA .....WALE WAKAKATA TAMAA NA KUSONONEKA HATA KUFA KABISA ILI KUBEBA WAVIVU.........HII ILIWASUMBUA SANA WAKULIMA WAKUBWA MKOANI IRINGA-ISIMANI AMBAO WALIPASUA MISITU KWA JITIHADA ZAO NA KUWEZA KULISHA MAHINDI NDANI NA KUUZA NJE....BAADAE SERIKALI IKAPOLA NA KUSEMA YAWE MASHAMBA YA UJAMAA, NI DHURUMA YA JASHO LA WATU....MKUU WA MKOA WA IRINGA DR. KRELUU ALISIMAMIA OPERATION HII ILIPELEKEA KIFO CHAKE BAADA YA KUMFANYIA HARASSMENT MKULIMA MZEE MWAMWINDI, NAYE ALIGADHABIKA NA KUFEDHEHEKA SANA...BILA KUJITAMBUA AKAMPIGA RISASI NA KUMWUA KABISA...KISHA KUBEBA MAITI YA MKUU WA MKOA TOKA ISIMANI NA KUENDESHA GARI YA MKUU WA MKOA YEYE MWENYEWE MPAKA CENTRO POLICE IRINGA MJINI NA KUWAKABIDHI POLICE MWILI NA YEYE KUSWEKWA NDANI....BAADAE KESI YAKE IKAENDESHWA FASTA FASTA .....NYERERE ALIHAKIKISHA JAMAA ANAPATIKANA NA HATIA KWANI ALIFANYA JUU CHINI MZEE MWAMWINDI ASIPATE MAWAKILI WA KUMTETEA....IKUMBUKWE WAKULIMA WENZAKE MWAMWINDI WALIFANYA MPANGO WA KULETA MAWAKILI TOKA MAREKANI NA ULAYA ILA NYERERE AKAWAFUNGA MAHABUSU WAKULIMA WALE KWA KUWATAWANYA MAHABUSU TOFAUTI NCHINI ILI KUMKOMESHA MWAMWINDI AMBAYE ALIHUKUMIWA KUNYONGWA HUKO DODOMA....SO SAD
Very sad. Na hayo maendeleo ya vijiji vya ujamaa yako wapi? Maana vijiji vipo hadi leo havina zahanati, maji wala maendeleo yoyote. Hivi vijiji vilikuwa ni namna watu wafanye kazi kama wako camp ili kurahisisha serikali kupata pesa. Pesa ambazo zilienda kutapanywa kwenye inefficiency factories na miradi mingine ya serikali.
 
Inasemwa na nani? Muache Mwalimu.

Inasemwa na nani? Pili elewa kwamba Mwalimu alikuwa anajenga taifa. Hakukuwa na Taifa zaidi ya koo za kikabila. Karagwe chiefdom, kina Marealle, Usambara, Unyenyembe nk. Hawa machifu na watemi walikuwa na Tawala ndogo za koo. Ilibidi Mwalimu azivunjilie mbali.

2. Hii nchi kubwa sana. Ilibidi kuweka watu karibu ili kupeleka huduma za kijamii. Vijiji vya Ujamaa vilikuwa na maendeleo makubwa mno. Miradi, ujenzi wa nchi pia ulikuwa kwa pamoja.

Ktk utekelezaji wa mipango mikubwa changamoto za hapa na pale ni kawaida. Kikubwa Mwalimu alijenga Taifa kwa maana ya Taifa kuliko kiongozi yeyote Afrika.
Wakumbuke pia hivyo Vijiji vingi vilipatiwa maji ,shule na zahanati.
Ningefurahi kupatuwa uthibitisho was anguko.la uzalishaji vs vijiji vya Ujamaa.
Kwa maeneo machache niliyokwenda Nimeona vijiji vya Ujamaa vilisukuma maendeleo !
 
Kabisa. Mimi nimezaliwa ktk Kijiji cha Ujamaa. Kulikuwa na maendeleo makubwa mno. Issue kama unavyosema imekuaje zile mali za vijiji zilipotea. Najua hadi leo kwa mfano, kijiji nilichotoka kina mali issue ni usimamizi.
 
Prof. Cuthbert Omari aliwahi kuandika kitabu kuhusu siasa ya Ujamaa. Kuna yeyote anayekikumbuka jina lake?
 
Lakini kwa upande mwingine Kulikuwa na faida, Maana kabla watu hawajaamishwa kwenda kwenye vijiji vya ujamaa watu waliishi kulingana na koo zao hii ingetuletea shida Leo.Vijiji vimesaidia socialization.Unaenda kijiji chochote ndani ya Nchi hii unafanya maisha bila kuulizwa wewe ni koo gani.Tuangalie na upande wa pili wa shilingi.
Hakika. Pamoja na kasoro nyinginezo, Ila palikuwa na faida
 
Aliwaleta watu kwenye vijiji vya ujamaa ili walime kwenye mashamba ya ujamaa na aweze kuwatoza ushuru vizuri. Nyerere siyo muanzilishi wa collectivization, aliiga tu, Ilianza huko Urusi, Ikaenda China. Kote huko ilifeli vibaya na kutumbukiza nchi hizo kwenye njaa. Hata hapa ikatutoa kuwa wauza chakula hadi wenye njaa wanaotegemea misaada.
Ikafaulu sanaaa Israel katika "kibutzi".
 
Back
Top Bottom