Inasemwa na nani? Muache Mwalimu.
Inasemwa na nani? Pili elewa kwamba Mwalimu alikuwa anajenga taifa. Hakukuwa na Taifa zaidi ya koo za kikabila. Karagwe chiefdom, kina Marealle, Usambara, Unyenyembe nk. Hawa machifu na watemi walikuwa na Tawala ndogo za koo. Ilibidi Mwalimu azivunjilie mbali.
2. Hii nchi kubwa sana. Ilibidi kuweka watu karibu ili kupeleka huduma za kijamii. Vijiji vya Ujamaa vilikuwa na maendeleo makubwa mno. Miradi, ujenzi wa nchi pia ulikuwa kwa pamoja.
Ktk utekelezaji wa mipango mikubwa changamoto za hapa na pale ni kawaida. Kikubwa Mwalimu alijenga Taifa kwa maana ya Taifa kuliko kiongozi yeyote Afrika.