TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Bila kufanya hivyo, masetler wangemsumbua kuendesha nchi. Na Idd Amin angetusumbua sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Point yako nini? Kwamba hakuna wakulima matajiri?
Mambo yote yanazunguka kwenye uchumi. Huwezi kupambana na wale maadui wa nchi bila kuwa na uchumi imara.
Jambo jema sana hili.sasa hivi mtu anaishi popote tz hiiLakini kwa upande mwingine Kulikuwa na faida, Maana kabla watu hawajaamishwa kwenda kwenye vijiji vya ujamaa watu waliishi kulingana na koo zao hii ingetuletea shida Leo.Vijiji vimesaidia socialization.Unaenda kijiji chochote ndani ya Nchi hii unafanya maisha bila kuulizwa wewe ni koo gani.Tuangalie na upande wa pili wa shilingi.
Lakini kwa upande mwingine Kulikuwa na faida, Maana kabla watu hawajaamishwa kwenda kwenye vijiji vya ujamaa watu waliishi kulingana na koo zao hii ingetuletea shida Leo.Vijiji vimesaidia socialization.Unaenda kijiji chochote ndani ya Nchi hii unafanya maisha bila kuulizwa wewe ni koo gani.Tuangalie na upande wa pili wa shilingi.
Kijiji chetu ,nyumba zilipangwa kwa mitaa Kama mjini, kulikuwa na maji Kila Angalau Km.moja ,zahanati,ilijengwa ,shule mbili za msingi,kulikuwa na Bwaana Maji,Kilimo,Mifugo wot3 Hawa walikuwa wanafanya kazi kwa ufanisi ..Kabisa. Mimi nimezaliwa ktk Kijiji cha Ujamaa. Kulikuwa na maendeleo makubwa mno. Issue kama unavyosema imekuaje zile mali za vijiji zilipotea. Najua hadi leo kwa mfano, kijiji nilichotoka kina mali issue ni usimamizi.
Hilo no swali la kijiuliza wote...me no ujamaa ulioanzisha hizo Zahanati au no kitu gani ?Zilienda wapi hizo zahanati? Vijiji vya ujamaa vilionyesha uzalishaji umekua sababu ya kupika data, na hilo lilifanyika kote vilikoanzishwa, China na Russia. Kote huko vijiji vya ujamaa vilikuwa ni disaster kubwa. Unafikiri hapa palikuwa special sana kwamba vilileta mafanikio?
Vipimo vya maendeleo vipo vingi lakini vyote vinategemea uchumi. Nipe mfano wa maendeleo yasiyoendana na maendeleo ya kiuchumi? Maendeleo yanayopimwa nje ya maendeleo ya uchumi bila shaka ndiyo hiyo scamndo maaana ukiwa unanunua kitu unaomba kupungiziwa ama kusubiria discount,katika hali halisi uchumi ni scam! uchumi hauna uhusiano sawa na maisha yetu ndo maaana nyerere alielezea maendeleo halisi yakoje, kipindi anaenda south alihutubiwa mbele ya mandela akamwambia japokua afrika inaona nchi yenu kama tajiri sana lakini bado nyinyi ni maskini, of which ni kweli, sasa unapopima hatua za maendeleo kwa kutumia uchumi basi umepotea
Ujamaa ulianguka kwa sababu zake zenyewe. Hizo vita ni visingizio tu, unaweza kueleza ilikuwaje mfumo mzuri na effiecient wa uzalishaji uliathiriwa na vita ya Uganda? Hiyo experiment ya vijiji vya ujamaa ilifeli China, ilifeli Urusi. Na kote huko vijiji vya ujamaa vilisababisha njaa na umaskini mkubwa kwa watu.Kijiji chetu ,nyumba zilipangwa kwa mitaa Kama mjini, kulikuwa na maji Kila Angalau Km.moja ,zahanati,ilijengwa ,shule mbili za msingi,kulikuwa na Bwaana Maji,Kilimo,Mifugo wot3 Hawa walikuwa wanafanya kazi kwa ufanisi ..
Pia lilikuwa na Chama Cha Ushirika
Shida iliamza miaka ya 1980s baada ya Vita vya I'd Amin
Naffikiri anguko la Ujamaa halipo kw3nye Ujamaa w3nyewe!
Ni kweli huoni !Ujamaa ulianguka kwa sababu zake zenyewe. Hizo vita ni visingizio tu, unaweza kueleza ilikuwaje mfumo mzuri na effiecient wa uzalishaji uliathiriwa na vita ya Uganda? Hiyo experiment ya vijiji vya ujamaa ilifeli China, ilifeli Urusi. Na kote huko vijiji vya ujamaa vilisababisha njaa na umaskini mkubwa kwa watu.
Leo hii hatuoni zahanati wala miundombinu ya maji yaliyojengwa na wajamaa, hata magofu hakuna. Unazungumzia vyama vya ushirika vilivyojaa rushwa na utapanyaji!
Ujamaa ni mfumo wa unyonyaji, kama tu utumwa. Lazima kuna watu watakumbuka maisha ya zamani na kusema, "Utumwa ulikuwa mzuri."
Yap, mfumo wa uzalishaji mali unahusiana vipi na vita? Unafikiri Uingereza ikipigana vita itaachana na Ubepari? Hivyo vyuo vya maendeleo vingi vilijengwa kwa msaada ya watu wa nje. Na vingi navifahamu, vilikuwa vinafuga na kulima. Inefficiency ya kufa mtu. Leo hakuna kitu.Ni kweli huoni !
Mfumo efficiency was uendeshaji utahimili vipi anguko la kiuchumi linalosabàbishwa na matukio Kama Vita!?!
Unasema huoni miundombinu iliyoanzishwa na ujamaa!
Mimi naiona kuna zananati za kutosha,miradi ya maji,shule,taasisi Kama vyuo vya afya, maendeleo ya jamii, Kama Misungwi,mabuhghai,monduli,,Lugemba,nk
Kunavyuo vya Mmaendeleo ya wananchi zaidi ya 50
Taasisi hizi zilizalisha maelfu ya Wataam wa afya,kilimo,ufundi ,mifugo ,mapishi na ushonaji ambao walienda / mpaka leo wan3nda vijijini!
Huo ulikuwa ni msingi mkubwa wa Maendeleo!
Vyama vya Ushirika vilikuwwpo ,na baadaye ikaingia rushwa .....!
Je,Nini kiliangusha Vyama hivi ,ni ujamaa?!
Au nguvu nyingine ya ziada!?
Pamoja na mapungufu yake ,lakini bado mfumo.huu wa maisha ulifaa!
Bila Shaka China ilifanikiwa kupenyeza Sekta Binafsi ndani ya Ujamaa ..ndio ikapaa ilipo Leo kuanzia miaka ya 70s hadi 80s!
Maendeleo yaliyopo Vijijini China msingi wake mojawapo no hiyvo Vijiji vya Mao!
Vipimo vya maendeleo vipo vingi lakini vyote vinategemea uchumi. Nipe mfano wa maendeleo yasiyoendana na maendeleo ya kiuchumi? Maendeleo yanayopimwa nje ya maendeleo ya uchumi bila shaka ndiyo hiyo scam
Hakuna tofauti. Muwekezaji anawwza kuqa mkulima, mvuvi, mfugaji nk. Usifikiri kulima kwa mkono au kulima nusu ekari ndiyo ukulima.
Hii ya watu kupinga GDP kama kipimo cha maendeleo/uchumi haijaanza leo. Ndiyo maana ikazaliwa GDP per Capita, HDI na GINI coefficient. Kama wewe ndiyo umegundua saa hizi hilo safari yako ni ndefu sana.social development, political..., but my point sio hata hio, nlichotaka kukuelimisha ni sakata zima la uchumi ni scam! uchumi ni nadharia na kitu ambacho tunakitengeneza akilini sisi wenyewe, pia unaweza soma apa Beyond GDP: here's a better way to measure people's prosperity
Lakini kwa upande mwingine Kulikuwa na faida, Maana kabla watu hawajaamishwa kwenda kwenye vijiji vya ujamaa watu waliishi kulingana na koo zao hii ingetuletea shida Leo.Vijiji vimesaidia socialization.Unaenda kijiji chochote ndani ya Nchi hii unafanya maisha bila kuulizwa wewe ni koo gani.Tuangalie na upande wa pili wa shilingi.
urbanization ya sasa ni nini kama sio modern vijiji vya ujamaa ?
It cheaper kwa huduma per unit area watu wakiwa karibu karibu kuliko kila mtu mmoja mmoja (mbali mbali)
Implimentation ilikuwa mbovu ila urbanization na miji ya sasa ndio hivyo hivyo tu vijiji ambavyo ni miji
Inasemwa na nani? Muache Mwalimu.
Inasemwa na nani? Pili elewa kwamba Mwalimu alikuwa anajenga taifa. Hakukuwa na Taifa zaidi ya koo za kikabila. Karagwe chiefdom, kina Marealle, Usambara, Unyenyembe nk. Hawa machifu na watemi walikuwa na Tawala ndogo za koo. Ilibidi Mwalimu azivunjilie mbali.
2. Hii nchi kubwa sana. Ilibidi kuweka watu karibu ili kupeleka huduma za kijamii. Vijiji vya Ujamaa vilikuwa na maendeleo makubwa mno. Miradi, ujenzi wa nchi pia ulikuwa kwa pamoja.
Ktk utekelezaji wa mipango mikubwa changamoto za hapa na pale ni kawaida. Kikubwa Mwalimu alijenga Taifa kwa maana ya Taifa kuliko kiongozi yeyote Afrika.
Umaetumia maneno ya Nyerere kutoka kitabu chake kimoja kinaitwa "Tujisahihishe;" sijui unakubaliana naye au unapingana naye. Ila ni kweli inawezekana kabisa kuwa MNyerer alifanya reorganization kubwa ya maikazi ya watu katika utawala wake. Vijiji vya ujamaa ni sehemu moja tu, lakini pile ile reorganization ya maisha ya mjini kwa kuwepo kwa nyumba za National housing, na reorganization ya jumla kwa kuhamisha makabila fulani kutoka sehemu zilizokuwa zimejaaa na kuwapeleka kwenye sehemu zaenye nafasi kama wachagga kutpolewa Kilimanjaro na kupelekwa morogoroa, wakara kuhamishwa kutoka kisiwani ukara na kupelekwa sengerema na geita, na kuna mwakati alikuwa amekubali kuhamisha wakikukuyu kutoka Kenya kwenda Sumbawanga.Sahihi kabisa.
Na yako mengine mengi ambayo yakisemwa watu wanapotezwa, lakini Ukweli una tabia ya kutopenda kudharauliwa, kupuuzwa au kufichwa; una tabia ya kufika na kujitokeza pasipotarajiwa, una tabia ya kushinda kila hila na vita dhidi yake NO MATTER WHAT.
Watu waliotapakaa walihamishwa kuishi kwa pamoja ukaribu (bila hivyo huwezi kuwapelekea watu resources) huduma za maji, umeme na miundombinu ni rahisi na nafuu watu wakiwa pamoja...Ile haikuwa urbanization bali villagization.