Nyerere alikurupuka kuleta mfumo wa Muungano ambao haupo sehemu yoyote Duniani, na hakuna nchi itakayojaribu kuiga

Nyerere alikurupuka kuleta mfumo wa Muungano ambao haupo sehemu yoyote Duniani, na hakuna nchi itakayojaribu kuiga

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Yeye ndie alieanzisha kitu hiki ambacho hakipo duniani nchi yoyote ile zaidi ya hapa kwetu.

Haiingii akilini vya upande A ni vya upande B lakini vya upande B si vya upande A, Very bitter.

Tukiendelea na huu mfumo, basi mateso haya tinayopitia yatakuwa mara 10 zaidi ya hapa miaka ijayo na ndio itakuwa case study kwamba haraka haraka ya akujaribu vitu ambavyo havijafanyiwa uchunguzi wala kuwahi kujaribiwa haina baraka.

Nchi fulani iwe huru lakini hapo hapo iingilie uhuru wa nchi nyingine huku yenyewe haitaki kuingiliwa mambo yake, aiseee!!

Hakuna binadamu Mkamilifu, wote huwa tunakosea, Nyerere ni baba wa taifa na ninamuheshimu mno lakini kwenye hili nae alikuwa na mapungufu kama binadamu wengine, Nashangaa sasa naposikia mtu akipinga muungano anaambiwa si mzalendo, akili za wapi hizi?

Mkamilifu pekee ni Mwenyezi Mungu tu na ndie tunaepaswa kufata sheria zake bila kuzibadili wala kuzikosoa.

hakikisha unapotoa comment ujibu swali muhimu, "MUUNGANO UNA FAIDA GANI KWA NCHI YAKO ?? "
 
Sasa Nyerere si alishafariki?

Nyie mmeshidnwa nini kubadili ili kuweka mfumo mnaouona bora?

Kinachowasumbua ni ukosefu wa akili tu, amueni mnachoona kinafaa kama kweli mna akili. Nyerere alimaliza muda wake mbona aliyoyaanzisha mengi mmeyafuta, hili linawashinda nini?
 
Zanzibar ana "privileges" nyingi kwanye muungano kwa sababu "Tanganyika" ndiye "anayeuhitaji zaidi" huu muungano. Ni simple logic.

Na "hadi tunakwenda mitamboni" ni kwamba mtu yeyote hawezi kuaminiwa "kupewa" madaraka ya Urais (wa upande huu au upande ule) bila "wenye nchi" kujiridhisha juu ya "nia na uwezo" wake wa "kuuenzi na kuudumisha" muungano.

In short, ni hivi, kwa sheria za kimataifa za mipaka ya bahari, kama Zanzibar akiondoka, ataondoka na "a significant share" ya bahari ya Hindi.

Na hiyo siku ambayo atakamilisha "makaratasi ya talaka" na Tanganyika ndio siku ambayo atafuatwa na WANAOJUA NINI MAANA YA BAHARI.

Unapozungumzia bahari, unazungumzia biashara ya usafirishaji na bandari (shipping), unazungumzia mafuta na gesi, unazungumzia nishati endelevu (renewable energy), unazungumzia utalii, unazungumzia uvuvi pamoja na "madude" mengine kibao.

Urusi anaililia Crimea, China anaililia Taiwan, halafu kuna "mtanganyika" anataka "Zanzibar iende zake" ?

Hivi hizi zitakua ni akili kweli ?

Ukiuliza kwanini muungano uondoke, utasikia ooh sababu "wao" wanapata nafasi za uwaziri, Urais, u DC, Ubunge, n.k lakini "sisi" hatupati nafasi hizo kule "upande wa pili" na haturuhusiwi kumiliki ardhi pamoja na blahblah zingine kibao...

Trust me, hayo ni mambo madogo madogo sana (petty internal issues).

Katika picha kubwa, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, we are better together.

Huyo Nyerere unayemlaumu, nadhani ungemlaumu kwa mambo mengine (tena yapo kibao kama kweli uko serious kutaka kumalalamikia huwezi kukosa) lakini sio hili la Muungano, tafadhali sana.

You have no idea to whose hands Zanzibar (with her share) may fall, whoever the new sheriff might be, consequences to "Tanganyika" are nearly unthinkable.

Kama huu muungano unakukera, nadhani unatakiwa kujifunza kuuvumilia. Bado upo sana.

NB: Kwanini muungano "kama huu" haujawahi kuigwa na watu wengine duniani, sijui hii inawezaje kuwa ni hoja ya msingi.
Anyways, niseme tu kwamba "situations do differ", sio kila kisichoigwa hakikuigwa kwa sababu ni kibaya.

Screenshot_20220302-060149_Maps.jpg
 
You have no idea to whose hands Zanzibar (with her share) may fall, whoever the new sheriff might be, consequences to "Tanganyika" are nearly unthinkable.
Mkuu Mwanamaji , ukisikia uzalendo, huu ndio uzalendo.
Kama huu muungano unakukera, nadhani unatakiwa kujifunza kuuvumilia. Bado upo sana.
Huu ndio ukweli wa mambo, Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, wataulinda huu muungano wetu adhimu kwa gharama yoyote.

P
 
Yeye ndie alieanzisha kitu hiki ambacho hakipo duniani nchi yoyote ile zaidi ya hapa kwetu.

Haiingii akilini vya upande A ni vya upande B lakini vya upande B si vya upande A, Very bitter...
Kwani lazima tuige mifumo mingine duniani!!?

Sisi wa kwetu ni wakipekee jiamini brother
 
Yeye ndie alieanzisha kitu hiki ambacho hakipo duniani nchi yoyote ile zaidi ya hapa kwetu.

Haiingii akilini vya upande A ni vya upande B lakini vya upande B si vya upande A, Very bitter...
Mkuu 'sky', unamlalamikia Mwalimu Nyerere bure.

Mwalimu hakusemamuungano udumu katika hali hii hii iliyouanzisha. Hii ilikuwa ni hatua ya mwanzo, ikitegemewa kuwa utaendelea kuboreshwa kadri watu watakavyozidi kuelewa na kuona manufaa ya muungano wenyewe.

Haya unayolalamikia hapa yametokana na viongozi waliofuata kuzidiwa kete na wale Wazanzibari waliokuwa hwataki muungano.

Tumeshuhudia mambo ya "Kero za Muungano" yakishamiri zaidi baada ya Nyerere. Kiala mwaka "Kero" za upande mmoja wa muungano zinaongezeka, huku upande wa pili wakiona upande wao kuko shwari tu, bila ya kero zozote. Matokeo ya kutatua hizo kero za upande mmoja ndiyo haya sasa unayoyalalamikia hapa. Wazanzibar wachache ambao hawakutaka uwepo wa muungano ndio wameendelea kuufanya muungano uwe kama ulivyo sasa; na kusema kweli wamefanikiwa sana.

Lakini nirudi nyuma kidogo. Hapa tulipofikia na muungano wetu huu ni ujinga tu wa waTanganyika kudhani kwamba Zanzibar inaweza kuwa na ubavu wa kujitenga. Sijui ni kutojiamini au kitu gani kinachowafanya waTanganyika wawe na hofu ya visiwa hivi vinavyokaa mlangoni mwa li-nchi kubwa hili kujitenga! Kwani wataanzia wapi? Ni nani atakuja hapa na kulazimisha nchi moja hii kumegwa kwa njia yoyote ile! Labda waje hao wakubwa wa manuklia, vinginevyo hakuna njia ya kuinasua Zanzibar kuwa nchi tofauti na Tanzania. Zanzibar ni 'HongKong' yetu, haiwezekani tena kuwa vinginevyo.

Na kwa upande mwingine, CCM wanafaidika sana na hali ya muungano ilivyo sasa, kwa maana inawahakikishia kuwepo kwenye madaraka milele.

Kwa hiyo kinachotakiwa sasa ni kuachana na hizi siasa za kubembelezana za enzi za Nyerere. Tunatakiwa sasa kuhakikisha lile kundi dogo la Zanzibar linalofanya kila juhudi ya kuuvunja muungano haliendelei kulelewa na kubembelezwa, kwa maana hata lifanyiwe mema gani, bado wataendelea kuibua kero mpya kila mwaka ili hatimae wafikie lengo lao la kuuvunja muungano kwa visingizio vya kero kutotatuliwa.
 
Zanzibar ana "privileges" nyingi kwanye muungano kwa sababu "Tanganyika" ndiye "anayeuhitaji zaidi" huu muungano. Ni simple logic.

Na "hadi tunakwenda mitamboni" ni kwamba mtu yeyote hawezi kuaminiwa "kupewa" madaraka ya Urais (wa upande huu au upande ule) bila
Sijui kwa nini watu wanapita bila kukupa "Like"

Mkuu, mi nimeshakupa ya kwangu...
 
Muungano ulikuwa na muhimu wakati ule tena ulikuwa na muhimu sana
Kwa sasa muungano huu hauna maana zaidi ya watanganyika kuwatunza watu wa visiwani
 
Zanzibar ana "privileges" nyingi kwanye muungano kwa sababu "Tanganyika" ndiye "anayeuhitaji zaidi" huu muungano. Ni simple logic.

Na "hadi tunakwenda mitamboni" ni kwamba mtu yeyote hawezi kuaminiwa "kupewa" madaraka ya Urais (wa upande huu au upande ule) bila "wenye nchi" kujiridhisha juu ya "nia na uwezo" wake wa "kuuenzi na kuudumisha" muungano...

Mbona Burundi na Rwanda zote hizi zilikuwa sehemu za tanganyika na ziliachiwa !!! Au hujui Hilo ?
 
Yeye ndie alieanzisha kitu hiki ambacho hakipo duniani nchi yoyote ile zaidi ya hapa kwetu.

Haiingii akilini vya upande A ni vya upande B lakini vya upande B si vya upande A, Very bitter...
Alifanya makosa mengi na mazuri machache. Likiwemo la kuificha historia halisi ya Taifa letu na ubinafs wa kuficha jitihada za wenzake.
Ujamaa wake unatutesa had leo. Kutuachia katiba ile ni janga lingine. Hata hivyo Nampongeza upande wa kutuunganisha kwa kiswahili.
 
Umeandika ujinga Sana ?

Mbona Burundi na Rwanda zote hizi zilikuwa sehemu za tanganyika na ziliachiwa !!! Au hujui Hilo ?
Asante kwa maoni yako juu ya nilichoandika (ujinga).

Kwahiyo unachotaka kusema ni kwamba kila anayetaka kutwaa mapande ya hii nchi na apewe ?

1. Unajua ni kwanini Tanzania na Uganda ya Iddi Amini ziliingia vitani mwaka 1978 ?

2. Unajua kwanini Tanzania na Malawi zilitaka kuingia kwenye "military negotiations" juu ya mipaka ya Ziwa Nyasa miaka kadhaa iliyopita ?

3. Unajua kwanini Kenya na Somalia miezi kadhaa iliyopita walitaka kuchukuliana hatua za kijeshi baada ya ICJ kutoa hukumu "iliyoipendelea" Somalia juu ya mzozo wa mgogoro wa mpaka wa baharini ?

It's all about territories
Hata kilomita tano zinatosha kabisa kuleta mzozo, suala la mipaka halina mzaha.

Samahani kwa kukuandikia "ujinga" mwingine, nivumilie nduguyo, ndivyo nilivyo.
Kwa bahati mbaya ni kwamba katika jamii hamuwezi kuwa werevu wote, ni lazima mchanganyike na "akina sisi" (wajinga wajinga). It's nature.
 
Alifanya makosa mengi na mazuri machache. Likiwemo la kuificha historia halisi ya Taifa letu na ubinafs wa kuficha jitihada za wenzake.
Ujamaa wake unatutesa had leo. Kutuachia katiba ile ni janga lingine. Hata hivyo Nampongeza upande wa kutuunganisha kwa kiswahili.
Yaani hata kwenye suala la katiba analaumiwa Nyerere ?
Mtu ambaye ametoka madarakani miaka 37 iliyopita ?

Hakika dunia imebeba mengi.
 
Yeye ndie alieanzisha kitu hiki ambacho hakipo duniani nchi yoyote ile zaidi ya hapa kwetu.

Haiingii akilini vya upande A ni vya upande B lakini vya upande B si vya upande A, Very bitter...
Hivi wewe ushawahi fika Zanzibar ukaona hicho wanachotuzidi?
Jibu ni Hakuna wanachotuzidi bara
Na kama una busara utajua ni bora hivyo wana serikali yao ya ndani, itasaidia kuleta maendeleo zaidi kwao

Mfano, tazama bara inavyosahau kuleta maendeleo katika baadhi ya maeneo yake mfano kule Mafia, sasa imagine ndio Zanzibar isahaulike hivyo, si ungekuwa ni ufala wa hali ya juu kwa Zanzibar

Halafu mnaolalamika kuhusu muungano wengi wenu huo muungano mnausikia mitandaoni ila haujawagusa kwenye familia na maisha yenu moja kwa moja
 
Yaani hata kwenye suala la katiba analaumiwa Nyerere ?
Mtu ambaye ametoka madarakani miaka 37 iliyopita ?

Hakika dunia imebeba mengi.
Aliyechonga njia na ikawa haieleweki ana haki ya kulaumiwa hata kwa miaka 200 achilia mbali miaka 37....Nyumba ni Msingi.

La maana walipo sasa warekebishe yale ambayo hayako sawa..!
 
Sasa Nyerere si alishafariki?

Nyie mmeshidnwa nini kubadili ili kuweka mfumo mnaouona bora?

Kinachowasumbua ni ukosefu wa akili tu, amueni mnachoona kinafaa kama kweli mna akili. Nyerere alimaliza muda wake mbona aliyoyaanzisha mengi mmeyafuta, hili linawashinda nini?
Kweli kulalamikia hayati ni upunguani, mtu uko hai na una akili badala ya kuleta ufumbuzi unalalamika, kama anasubiri Nyerere afufuke aje afanye anavyotaka huo ni upungufu wa akili.
 
Yaani hata kwenye suala la katiba analaumiwa Nyerere ?
Mtu ambaye ametoka madarakani miaka 37 iliyopita ?

Hakika dunia imebeba mengi.
Rudi nyuma aliposema ....katiba yetu inatoa mwanya wa rais kuwa Mungu mtu.... bado hakujishighulisha kuchochea ibadililishwe hajaja huyo rais kichaa aliyemhisi! Hakuziba ufa. Wenzake wanautumia had leo.
 
Aliyechonga njia na ikawa haieleweki ana haki ya kulaumiwa hata kwa miaka 200 achilia mbali miaka 37....Nyumba ni Msingi.
Basi tusubiri Nyerere aje ku "fix" katiba.
Sisi tuendelee kulalamika kwa sasa.
 
Back
Top Bottom