Nyerere alikurupuka kuleta mfumo wa Muungano ambao haupo sehemu yoyote Duniani, na hakuna nchi itakayojaribu kuiga

Nyerere alikurupuka kuleta mfumo wa Muungano ambao haupo sehemu yoyote Duniani, na hakuna nchi itakayojaribu kuiga

Zanzibar ana "privileges" nyingi kwanye muungano kwa sababu "Tanganyika" ndiye "anayeuhitaji zaidi" huu muungano. Ni simple logic.

Na "hadi tunakwenda mitamboni" ni kwamba mtu yeyote hawezi kuaminiwa "kupewa" madaraka ya Urais (wa upande huu au upande ule) bila "wenye nchi" kujiridhisha juu ya "nia na uwezo" wake wa "kuuenzi na kuudumisha" muungano...
Hii ngombe imeandika uharo..unasema ni inshu ndogo hizo..bure kabisa wewe..zenji tunaitaka sana na hatuwezi iachia maisha..ila tunaenda kubadili mfumo wa utawara soon.

#MaendeleoHayanaChama
 
Basi tusubiri Nyerere aje ku "fix" katiba.
Sisi tuendelee kulalamika kwa sasa.
Hatulalamiki lakini ndo ukweli, tafakari sana huu msemo' Samaki Mkunje Angalia Mbichi.

Kwenye ukweli lazima tuseme, kuwa haya mambo yametuletea shida sana ambapo kila anayejaribu kuyarekebisha alijikuta kwenye pipa la moto.
 
Nimefuatilia Dubai Expo2020 nikajiuliza pia, nchi ni moja lakini inaonekana nchi mbili 'zinagombea' wawekezaji maana kabla nilijua nje ya mipaka tunaongea lugha moja.

Mwalimu alikuwa na nia njema lakini wajinga sisi tulichoharibu zaidi ni kuamini kuwa alikuwa perfect kwa kila aliloliamua pamoja na yeye kutoka hadharani na kukiri kuwa "hakuwa malaika". Ndio maana miaka karibia 40 tunaendeleza ujinga hata pale Mzee Warioba alipotustua kuwa either serikali moja kwa umoja imara au tatu kila mtu ajijue bado tunajifanya hamnazo.
 
Mimi nitaunga mkono Muungano wa serikali 3! Huu Muungano wa Changu Changu, Chako Changu! Nadhani hauna manufaa yoyote yale.

Zaidi tu ndiyo unasababisha manung'uniko upande mmoja, na kero zisizoisha upande mwingine.
 
Mkuu 'sky', unamlalamikia Mwalimu Nyerere bure.

Mwalimu hakusemamuungano udumu katika hali hii hii iliyouanzisha. Hii ilikuwa ni hatua ya mwanzo, ikitegemewa kuwa utaendelea kuboreshwa kadri watu watakavyozidi kuelewa na kuona manufaa ya muungano wenyewe...
Tena sio ccm bara ni ccm zenji ndio wananufaika zaidi na huu muungano feki..hawataki kabisa uvunjike mana ndio ulaji wao ulipo.

#MaendeleoHayanaChama
 
United Kingdom wana muungano na juzi nilishangaa kuona UK government inazipa funds serikali za Wales, Northern Ireland na Scotland. England inaizidi mapato Scotland mara kumi, wakati Scotland ndio ya pili kwa utajiri kwenye huo muungano. Kama UK wameungana nchi nne iweje sisi tushindwe mbili. Wana muungano mgumu zaidi ila wanatumia akili kuliko sisi walalamishi. Kujitenga na Zanzibar ni hatari kwa usalama wetu sote wawili
 
Rudi nyuma aliposema ....katiba yetu inatoa mwanya wa rais kuwa Mungu mtu.... bado hakujishighulisha kuchochea ibadililishwe hajaja huyo rais kichaa aliyemhisi! Hakuziba ufa. Wenzake wanautumia had leo.
Basi sisi tuendelee kumsubiri aje kutubadilishia.

Maana kwa inavyoonekana ni kama "sisi" tunaona sio jukumu letu kabisa. Tumejipa jukumu pendwa la kulalama.
 
Hii ngombe imeandika uharo..unasema ni inshu ndogo hizo..bure kabisa wewe..zenji tunaitaka sana na hatuwezi iachia maisha..ila tunaenda kubadili mfumo wa utawara soon.

#MaendeleoHayanaChama
Kuita watu ng'ombe katika mijadala inaweza kukuletea picha mbaya sana mahala pengine.

Tafadhali haya yasiwe ni mazoea yako.

Ila unapojadili masuala na mimi (Mwanamaji ), unaweza kuendelea kuniita ng'ombe au kama hautojali chagua jina jingine baya zaidi. I will take it.

Unaposema kubadilisha mfumo wa utawara (bila shaka ulitaka kuandika utawala,) unamaanisha nini mkuu ?

NB: Msimamo wangu wa jumla ni kwamba, kama kuna changamoto au kero yoyote ya Muungano, tunayo fursa ya kuitatua na tukasonga mbele tukiwa wamoja.

Kama kubadilisha mfumo wa utawala (japokua sijajua umemaanisha nini haswa) ni miongoni mwa vitu vitakavyoboresha zaidi Muungano wetu, basi namimi naunga mkono juhudi hizo.
 
Mkuu Mwanamaji , ukisikia uzalendo, huu ndio uzalendo.

Huu ndio ukweli wa mambo, Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, wataulinda huu muungano wetu adhimu kwa gharama yoyote.

P
Hilo takwa la huo uzalendo mbona ni very divisive??
Mbona kila muungano huo unapoguswa kunaibuka makelele mengi?
Muundo uliopo wa muungano ni chaka lenye makandokando lukuki.

Wito kwenu "wazalendo" boresheni muundo. Nchi iwe moja. Serikali moja!
Tofauti ni hapo tunaandaa time bombs 💣💣
 
Zanzibar ana "privileges" nyingi kwanye muungano kwa sababu "Tanganyika" ndiye "anayeuhitaji zaidi" huu muungano. Ni simple logic.

Na "hadi tunakwenda mitamboni" ni kwamba mtu yeyote hawezi kuaminiwa "kupewa" madaraka ya Urais (wa upande huu au upande ule) bila "wenye nchi" kujiridhisha juu ya "nia na uwezo" wake wa "kuuenzi na kuudumisha" muungano.

In short, ni hivi, kwa sheria za kimataifa za mipaka ya bahari, kama Zanzibar akiondoka, ataondoka na "a significant share" ya bahari ya Hindi.

Na hiyo siku ambayo atakamilisha "makaratasi ya talaka" na Tanganyika ndio siku ambayo atafuatwa na WANAOJUA NINI MAANA YA BAHARI.

Unapozungumzia bahari, unazungumzia biashara ya usafirishaji na bandari (shipping), unazungumzia mafuta na gesi, unazungumzia nishati endelevu (renewable energy), unazungumzia utalii, unazungumzia uvuvi pamoja na "madude" mengine kibao.

Urusi anaililia Crimea, China anaililia Taiwan, halafu kuna "mtanganyika" anataka "Zanzibar iende zake" ?

Hivi hizi zitakua ni akili kweli ?

Ukiuliza kwanini muungano uondoke, utasikia ooh sababu "wao" wanapata nafasi za uwaziri, Urais, u DC, Ubunge, n.k lakini "sisi" hatupati nafasi hizo kule "upande wa pili" na haturuhusiwi kumiliki ardhi pamoja na blahblah zingine kibao...

Trust me, hayo ni mambo madogo madogo sana (petty internal issues).

Katika picha kubwa, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, we are better together.

Huyo Nyerere unayemlaumu, nadhani ungemlaumu kwa mambo mengine (tena yapo kibao kama kweli uko serious kutaka kumalalamikia huwezi kukosa) lakini sio hili la Muungano, tafadhali sana.

You have no idea to whose hands Zanzibar (with her share) may fall, whoever the new sheriff might be, consequences to "Tanganyika" are nearly unthinkable.

Kama huu muungano unakukera, nadhani unatakiwa kujifunza kuuvumilia. Bado upo sana.

NB: Kwanini muungano "kama huu" haujawahi kuigwa na watu wengine duniani, sijui hii inawezaje kuwa ni hoja ya msingi.
Anyways, niseme tu kwamba "situations do differ", sio kila kisichoigwa hakikuigwa kwa sababu ni kibaya.

View attachment 2135774
Watu hawawezi kuishi kwa kutegemea bahari na bandari tu ni ufinyu wa akili . Nchi ngapi hazina bahari wala madini na zimeendelea kuliko tanzania!? Kuna sababu zaidi ya hizi tunazoambiwa. Ila tunapoenda watatakiwa kuwa wawazi zaidi kama ni sababu za kiusalama watatakiwa waseme tu. Nyerere aliogopa ujio wa waarabu. Wazanzibari wanajiona wao ni kama waarabu ndivyo wanavyopenda kujidanganya kwahiyo kwao ni rahisi kushirikiana na mwarabu kuliko mzungu.
 
Katiba mpya ndio dawa ya vikolokolo vyote
 
Ni nani aliomba kuungana na mwenxake kati ya Zanzibar na Tanganyika?

Samahani lakini mkuu P!
Andiko la huyo P linasisitiza kuwa uzalendo ni kuukubali na kuulinda muungano jinsi ulivyo.
Mwanamaji anatanabaisha kuwa Tanganyika ilihujitaji zaidi muungano hadi ikakubali kupoteza utambulisho wake.
Kifupi; Tanganyika ndiyo ililazimisha muungano kwa maslahi yake binafsi.

NB: Utawaelewa vizuri Watanzania waodai PUTIN kule Russia anafanya kazi nzuri sana dhidi ya Ukraine. Wanaona kabisa Russia inaanza kuiga muungano wa JMT.
China ilishafanikiwa kuzikalia kimabavu Hong Kong na Taiwan.
 
Asante kwa maoni yako juu ya nilichoandika (ujinga).

Kwahiyo unachotaka kusema ni kwamba kila anayetaka kutwaa mapande ya hii nchi na apewe ?

1. Unajua ni kwanini Tanzania na Uganda ya Iddi Amini ziliingia vitani mwaka 1978 ?

2. Unajua kwanini Tanzania na Malawi zilitaka kuingia kwenye "military negotiations" juu ya mipaka ya Ziwa Nyasa miaka kadhaa iliyopita ?

3. Unajua kwanini Kenya na Somalia miezi kadhaa iliyopita walitaka kuchukuliana hatua za kijeshi baada ya ICJ kutoa hukumu "iliyoipendelea" Somalia juu ya mzozo wa mgogoro wa mpaka wa baharini ?

It's all about territories.

Hata kilomita tano zinatosha kabisa kuleta mzozo, suala la mipaka halina mzaha.

Samahani kwa kukuandikia "ujinga" mwingine, nivumilie nduguyo, ndivyo nilivyo.
Kwa bahati mbaya ni kwamba katika jamii hamuwezi kuwa werevu wote, ni lazima mchanganyike na "akina sisi" (wajinga wajinga). It's nature.
Naomba utuelezee jambo moja hapa wewe uko Well informed kuhusu hu muungano hivi:
huu muungano umuhimu wake hasaa uko wapi na kwa kiwango gani kwamba we can't go with out it
Kiuchumi hiyo sehemu ya bahari inachangia kias gani kwenye GDP ya taifa? Naomba takwimu

Ki Usalama nchi gani ni tishio kwetu kutuvamia na ipate nini? hapa kwetu ikiwa ine base visiwani zazibar au ni nadharia yako tu?..... all those are outdated security threats na wanao hofia sana ni wale watu walio zaliwa katika utawala wa Nyerere miaka 60s en 70s we need new mindset.
Huo muungano unapromote national unity en nationalism (uzalendo) viko wapi? Mzazibar ni mzabari hamkubali mtaganyika hata siku moja,
unagawana je nchi ya watu1m kwa watu 50m, sio sahihi kabisa, unfair kabisa huo muungano lzma urekebishwe kwenye vipengere vingi au zazibar ipewe uhuru wake tusiogope ushindani kwa kujificha kwenye muungano.
 
Hatulalamiki lakini ndo ukweli, tafakari sana huu msemo' Samaki Mkunje Angalia Mbichi.

Kwenye ukweli lazima tuseme, kuwa haya mambo yametuletea shida sana ambapo kila anayejaribu kuyarekebisha alijikuta kwenye pipa la moto.
Ukitaka kujua kuvunja muungano ilivyo ngumu.

Hebu nenda kwenye mipaka ya Jirani yako, halafu jiongezee hata Inches 10 kutoka kwenye Kiwanja Cha jirani.

Kama damu haijamwagika, then ndio utaona Ni rahisi kuachia ardhi hiyo ya Zanzibar kirahisi tu.
 
Yeye ndie alieanzisha kitu hiki ambacho hakipo duniani nchi yoyote ile zaidi ya hapa kwetu.

Haiingii akilini vya upande A ni vya upande B lakini vya upande B si vya upande A, Very bitter.

Tukiendelea na huu mfumo, basi mateso haya tinayopitia yatakuwa mara 10 zaidi ya hapa miaka ijayo na ndio itakuwa case study.

Nchi fulani iwe huru lakini hapo hapo iingilie uhuru wa nchi nyingine huku yenyewe haitaki kuingiliwa mambo yake, aiseee!!

Hakuna binadamu Mkamilifu, wote huwa tunakosea, Nyerere ni baba wa taifa na ninamuheshimu mno lakini kwenye hili nae alikuwa na mapungufu kama binadamu wengine.

Mkamilifu ni Mwenyezi Mungu pekee na ndie tunaepaswa kufata sheria zake bila kuzibadili wala kuzikosoa.
Kwa nini mtu aje na mfumo wa muungano ambao haupo mahali popote pale duniani na wakati ana akili timamu? Je, ni kwa bahati mbaya tu alifanya hivyo au ni kwa makusudi? Na kama alifanya kwa makusudi ni kwa nini?
Ifikie mahali watu waanze kuhoji sababu za kwa nini mwalimu aliamua kufanya hivi, na si kuhoji kwa nini Muungano uko kama ulivyo. Lazima kuna sababu za msingi zilizopelekea afanye hivyo. Zitafute hizo sababu uzijue kwanza halafu ukishazijua ndiyo uanze kuu-criticize muungano. Usipofanikiwa kuzipata, pengine labda inaweza ikapendeza zaidi ukanyamaza. Unajua tatizo leu sisi siku hizi tumesoma sana kuwapita wote waliotutangulia huko nyuma
 
Ukitaka kujua kuvunja muungano ilivyo ngumu.

Hebu nenda kwenye mipaka ya Jirani yako, halafu jiongezee hata Inches 10 kutoka kwenye Kiwanja Cha jirani.

Kama damu haijamwagika, then ndio utaona Ni rahisi kuachia ardhi hiyo ya Zanzibar kirahisi tu.
Hilo ni suala la imotional sio reality kila mtu hapendi kuonewa tu
 
Back
Top Bottom