britanicca
Platinum Member
- May 20, 2015
- 18,261
- 48,864
Jumapili ni tulivu! Pamoja na kwamba Tuna PM wa mchongo, na wakati huo Namba moja na Namba mbili hawapatani wanaogopa kutiliana sumu tuangalie hapa chini
Haina ubishi wote mliokuwapo wakati wa Nyerere alikuwa dictator Lakin mwenye akili natoa mifano michache tu
1. Mzee mtei aliachana naye kwa kutofautiana kwa sera Lakin akaachwa tu na wakaendelea kuwa wanasiasa wanaoheshimiana, pamoja na mtei kukosoa sera zote za mwalimu hadi ku resign lakin ilikuwa ni busara tu za kuamini katika kutofautiana, Swali kwa Magufuli au Samia unaweza andika hata barua ya kuacha kazi bila kufuatwa na wasiojulikana na kukupa vititsho au kukupoteza kabisa ? Nakumbuka wakati wa Magufuli kuna mtu alikataa uteuzi ikabidi awajibishwe kabisa na kuambiwa mtoro kazini na anasakwa! Lakin kwa Nyerere tumeona akitotofautiana na mtei,
2. Nyerere alikataliwa na Warioba kwa baadhi ya sheria na akasema kama ni hivi basi najiuzulu, Lakin leo hii hakuna mwanasheria wa SERIKALI Anaweza tofautiana na Rais wakawa SALAMA , tuna mifano ya Ummy Mwalimu, Ndugai, Hata Tulia kwa sasa weka mbali akina Mpango na Majaliwa Lakin ukweli ndo huo !
3. Mwaka 1982 Vijana waliiteka ndege ya Tanzania na kuipeleka uingereza , nauliza kwa sasa unaweza teka hata basi tu la mwendo kasi? Ukaachwa SALAMA ??
Nyerere alisikiliza Hoja za vijana na baadae akazifanyia kazi baadhi Lakin hakuwa na jaziba kuwasaka na kuwaua!
4. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza miaka ya 1980 Mzee Abdunuru Suleiman walitofautiana na Nyerere hata kwa kuonekana hatii maagizo ya Nyerere na akawekwa pembeni wala hakuambiwa kwamba awekwe kizuizini au auwawe! Lakin kwa sasa ni Hatari zaidi
Mkapa nimemuweka maana alitofautiana na baadhi Ila hakuwaua!
Ila JPM, SAMIA, JAKAYA, hawa ni madikteta wanaojifanya kucheka Lakin wanaua watu
Tunataka katiba nzuri na pia Taasisi za kuweza kuisimamia na kumsimamia kila mtu
Britanicca