Nyerere alipenda sana chama cha CCM kuliko nchi ya Tanzania

Mwalimu alifanya alichoweza kukifanya 🙄 ! Full stop 🛑
Na sisi tuliopo sasa tufanye kile tunachotakiwa kufanya kwa muda uliopo 🙄 !

Kama tumeshindwa na hatujui cha kufanya maana yake sisi ni BURE KABISAAA !!
Au nasema uongo ndugu zanguni ??!
 
Wajukuu mbona hamna adabu kwa babu yenu
Sio kwamba hawana adabu bali ni ujanja ujanja mwingi umejaa mpaka unafurumia kiasi kwamba wanaamua kumuangushia Jumba bovu mtu ambaye hayupo miaka mingi ili waendelee kuhomondola kwa ulaini bila jasho !!

Ndio maana Waswahili walisemaga ujanja ni kupata sio kuwahi 🙄😳 !
 
Jibu hoja kwanini kwenye amendment 11 akiwa hai kwanini hakuondoa jambo ambalo amekuwa akililamikia majukwaani ya madaraka makubwa ya Rais

Kwani ni uongo hakukua na amendment 11 za katiba ya Tanzania wakati Nyerere akiwa hai???
Nyerere ndie alikuwa na mamlaka ya kubadilisha Katiba?
 
Nyerere ndie alikuwa na mamlaka ya kubadilisha Katiba?
Alikuwa na ùshawishi mkubwa sana
Mwaka 1992 wananchi walikataà vyama vingi ili yeye akàlazimisha na akafanya amendment za katiba kwa kuweka vyamà vingi

Mwaka 1979, na 1980's yalifanyika mabadiliko ya katiba bila hata wananchi kudhirikishwa
 
Tunatumia katiba ya mwaka 1977 mpaka sahivi navyoandika hii sms sasa kwanini asilaumiwe

Inaonekana hujui somo la katiba na legacy
 
Katiba yake ya 1977 inawafaidisha watawala unafikiri watakubali kuiacha

Yaani wabadilishe kitu ambacho kinawahakikisha ushindi kabla hata ya uchaguzi, na ulinzi baada ya kustafu hata kama walifanya mambo ya hovyo mengi wakatì wanatawala alafu unataka walete katiba itakayowabana utasubiri sana
 
Alisema CCM si mama yake au baba yake, kumbuka alikuwa mzee wa abracadabra.
 
Alisema CCM si mama yake au baba yake, kumbuka alikuwa mzee wa abracadabra.
Ile ilikuwa danganya toto
Na mbaya zaidi somo la katiba ya mwaka 1977 na amendment zake 14 na sababu za amendment wananchi wengi hawalijui na hawafundishwi maksudi ili waendelee kukaa gizani
 
Kuwa na ushawishi hakuna maana kwamba kila wazo ndio litoke kwake.

Acha lawama zisizo na msingi.
 
Kuwa na ushawishi hakuna maana kwamba kila wazo ndio litoke kwake.

Acha lawama zisizo na msingi.
Hujui historia ya Tanzania na nguvu alizokuwa nazo Nyerere

Mwaka 1984 baada ya abdul jumbe kujiuzurù na Nyerere kuagiza awekwe house arrest kigamboni kumbuka ni Nyerere na sio mahakama alimuagiza mwinyi achukue mikoba kama Rais wa Zanzibar aliyafanya haya kwa utashi wake yeye sasa unasemaje huyu mtu alikuwa wa kawaida

Mwaka 1995 Nyerere aliwaambia wananchi mtake mstake mkapa ndo Rais sasa huyu mtu kawa akili zako alikuwa wakawaida

Nyerere aliacha urais wa Tanzania mwaka 1985 cha ajabu akaendelea na uenyekiti wa chama cha ccm mpaka mwaka 1990
 
Hapo unaweza kuta mtoa post ana cheti cha degree au masters fulani ndani. Aibu hii !!

Mwalimu kafariki miaka 27 imepita...

Awamu nyingi zimepita na zinaendelea bila uwepo wa mwalimu.

Katika circle ya wafanya maamuzi mazito ya nchi wapo watu wengine nje, si mwalimu tena.

Je, tusubiri mwalimu afufuke kutoka kwa wafu aje aturekebishie tunayomlaumu leo ?

Je, tuwakomalie waioshika hatamu sasa ktk vyombo vya kimaamuzi ili wafanye maamuzi ya kubadili katiba kulingana na wakati tuliopo au vizazi na vizazi tuendelee kumlaumu mwalimu ?

Kuna mahala mwalimu aliweka azimio kuwa katiba na yote aliyoyaanzisha yasijebadilishwa ata kama hayaendani na nyakati husika ?

Awamu ya 4 alijaribu ishu ya katiba na ilifika pazuri, wakaivuruga wao wenyewe kule ndani, nalo tumlaumu mwalimu aliekua kalala zake miaka mingi nyuma....

Hatuwezi yashinda mabadilko kwa akili hii ya kulia na mtu ambae kapumzika zake miaka mingi nyuma.

Kama kweli sio wanafiki, waoga, machawa na watumwaji.. Tuangalie wenyewe nini kifanyike kujinasua hapa tulipo.
 
Nyerere alikuwa mbinafsi alijitengenezea umungu katika nchi, hakuwa na uzalendo wowote kwa nchi, ndio maana alijewekea mazingira ya kutowajibishwa na chombo chochote na hicho ndicho kinaitafuna nchi sasa
 
Still tunatumia katiba ya mwaka 1977 ambayo iliundwa wakati Nyerere akiwa Rais na katiba hiyo ndo ambayo imetengeneza na kusimamia mifumo yote ya kiuongozi ya sasa sasa unasemaje hausiki

Ccm hawawezi badilisha katiba ya sasa sababu inawafaidisha sana na hata wakibadilisha itakua ni katiba mpya jina ila maudhui ni yale-yale ya katiba ya zamani

Huwezi badilisha kitu/jambo ambalo linakufaidisha ndo kilichotokea mwaka 2014 kwenye katiba ya warioba
 
Nyerere alikuwa mbinafsi alijitengenezea umungu katika nchi, hakuwa na uzalendo wowote kwa nchi, ndio maana alijewekea mazingira ya kutowajibishwa na chombo chochote na hicho ndicho kinaitafuna nchi sasa
Na hayo mazingirà ya kutokuwajibishwa ndo waliomtangulia wanaitumia hiyo loopholes kikamilifu
 
Nyerere hakuwa malaika atufanyie kila kitu. Wewe anzisha movement sasa ya kudai hicho ukitakacho wacha kupoteza muda kumsema marehemu.

Suala la nguvu ya Nyerere hata kama lilikuwepo still alikuwa human, alishakaririwa akisema badala muige mazuri nyie mnaiga yale mabaya, naona hiyo ndio mindset yako pia kwa hizi lawama zako kwake.
 
Hizi beji za platinum mnapewa kwa kigezo cha uelewa au upumbavu mlio nao?.
Chukuwa hiyo kama ndiyo sifa unayoitafuta hapa.
Najuwa itakuwa ni ya hadhi hiyo katika upumbavu
 
Unajua katiba ya mwaka 1977 inavyoitesa nchi mpaka leo na pia mimi ndo maana nimeanza movement ya kuwa Rais wa Tanzania ili kuhakikisha nchi inakua na katiba nzuri zaidi ya hii iliyopo
 
RIP Tanganyika....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…