Nyerere alipenda sana chama cha CCM kuliko nchi ya Tanzania

Nyerere alipenda sana chama cha CCM kuliko nchi ya Tanzania

"...kuna mambo mengi aliyoyafanya...", lakini wewe huyajui?
Ndiyo sababu ukajipachika jina sahihi la 'Bush Dokta'; linaendana vizuri sana na fikra zako.
Hahaha Bush Dokta ni Sisi wa mitishamba, conservatives
 
Nyerere akijenga TAIFA.

Mao alijemmnga TAIFA.

Wao kujenga UCHUMI wameshimdwa, lawama zote kwa Nyerere.

Nyerere ameacha ARDHI, WATU, MADINI bila hata kuchimba, KILIMO, VIWANDA ila leo wanauza mpaka HEWA (CARBON CREDITS) halafu lawama ni Nyerere.

Unaokea elfu 2, za Mwanasiasa MWIZI na MUUAJI halafu unamlaumu Nyerere.
Mkuu, sijui mimi ningeyasemaje haya vizuri zaidi ya ulivyoyaandika wewe.
Binafsi huwa ninajiuliza sana kwa nini inakuwa rahisi sana kwa baadhi ya watu kulaumu Nyerere kuliko kutumia akili zao kuchanganua haya yanayotukabili sasa hivi.

Kwa nini iwe rahisi kutupa lawama kwa Nyerere, kuliko kuwasema hawa waliopindisha kila kitu alichokisimamia katika taifa hili?
Ajenda yao ni ipi hasa, na inamsaidia nani kama siyo hawa hawa waliopindisha kila kitu.
 
Acha kutetea ujinga na uchoyo wa huyo mchonga meno. Alipokuwa hai alikuwa Bado na nguvu yakuwashauri aliokuwa anataka wawe VIONGOZI wa nchi cha ajabu hakufanya hivyo!!. Kwahiyo matatizo na ubovu wa VIONGOZI huu umetokana na unafiki wake.
Mimi naweza kutetea "ujinga"; lakini ni wazi kabisa hapa kwamba wewe unatetea upumbavu, hata hujui unachotetea.
 
Nyerere alikuwa Anamfuata Ben Usiku wa Manane magogoni kuhusu Sheria ya Ubinafsishaji hasa baada ya Kuuza Benki ya NBC kwa Bei ya hasara mno.
 
Kikubwa kuliko yote nikashauri kusoma sana Mzee.
Unatakiwa kusoma mno
 
Nyerere alikuwa Anamfuata Ben Usiku wa Manane magogoni kuhusu Sheria ya Ubinafsishaji hasa baada ya Kuuza Benki ya NBC kwa Bei ya hasara mno.
Leo hii Samia anagawa gesi ya Ntorya, Mtwara kwa wajomba zake wa Oman, hakuna anayeuliza chochote juu ya hilo; kwa vile tu kwamba Nyerere ndiye aliyeshindwa kufanya marekebisho ya katiba!.

Mtu anaua waTanzania ili aendelee kubaki madarakani kwa nguvu; halaumiwi yeye, bali Nyerere ambaye alishindwa kubadili katiba miaka zaidi ya 20 iliyopita!
 
Jamii yetu kwa kiasi kikubwa sana imejengwa kwenye misingi ya unafki lakin haya tunayoyalalamikia leo chanzo ni Nyerere ni mbaya zaidi aliyajua yote haya kwa maksudi akayaacha
Hakuyaacha kwa makusudi, uwezekano mkubwa ni kwamba alikuwa anaona raia wengi wa Tanzania hawana akili za kutosha kuweka rais sahihi kupitia uchaguzi bila intervention ya 'system' au bunge kuwa na uwezo wa kumdhibiti rais bila kuleta vurugu.
 
Leo hii Samia anagawa gesi ya Ntorya, Mtwara kwa wajomba zake wa Oman, hakuna anayeuliza chochote juu ya hilo; kwa vile tu kwamba Nyerere ndiye aliyeshindwa kufanya marekebisho ya katiba!.

Mtu anaua waTanzania ili aendelee kubaki madarakani kwa nguvu; halaumiwi yeye, bali Nyerere ambaye alishindwa kubadili katiba miaka zaidi ya 20 iliyopita!

Huyo jamaa Sio mzima Kabisa.
Hajui mwalimu alipoitoa hii nchi.
1961.

Huyu anaweza akawa anamlaumu Babu yake kwa makosa ya Baba yake.
 
1. Siasa ya Ujamaa
2. Muungano
3. Katiba
Hayo mambo matatu ndio doa kubwa kwa legacy ya Nyerere
 
Legacy ya Nyerere haihusiani chochote na mabadiliko yatakayotokea Tanzania kwa enzi zote.
Legacy yake inahusu yaliyofanyika wakati wake siyo nyakati zote wa uwepo wa taifa hili.

Kuna viongozi chungu nzima wataacha 'legacy' zao nyakati mbalimbali za uongozi wao.
Akiwa kama founder wa Taifa legacy ni kubwa zaidi kwa wakati wote tofauti na waliomfuatia. Ni kweli kuna mengi Nyerere aliyakosea nchi hii lakini huenda nyakati na nia yake ndivyo vya kuangalia zaidi tukizingatia hakuwa fisadi, hakuuza nchi kwa mabepari wala hakupendelea na kunufaisha familia yake.
 
Majuzi hapa kuna Rais kaunda bunge la katiba na rasmu ya katiba ikatengenezwa na kupotezewa na Rais huyo huyo huku pesa za walipa kodi zikiwa zimepotea bure.
Huyo Rais haongelewi kabisa.

Eti Nyerere tu ndiye alaumiwe...
 
1. Siasa ya Ujamaa
2. Muungano
3. Katiba
Hayo mambo matatu ndio doa kubwa kwa legacy ya Nyerere
Utanisamehe kwa kuuliza:
Ni "doa kubwa" kivipi?
Kwa nini siasa ya ujamaa ilikuwa ni doa; kulinganisha na nani. Hakuna nchi zilizofuata mlengo huo wa kimfumo ambazo sasa zimefanikiwa?
Hakuna nchi ambazo hazikufuata mfumo huo, lakini hadi leo hii hazina tofauti yoyote na Tanzania iliyofuata Ujamaa?

Unaweza kueleza kwa nini wewe binafsi unafikiri Ujamaa ilikuwa ni doa?

Muungano: hapa pia hujaeleza chochote kwa nini unafikiri muungano ulikuwa ni doa. Kushindwa kwetu kuurekebisha ukidhi mahitaji yetu ya sasa, iwe ni sababu ya kumlaumu Nyerere kuhusu muungano huo?
Muungano aliouacha Nyerere, ndio huu tunaoushuhudia leo chini ya Samia?
Huoni kabisa tofauti yoyote iliyopo sasa na ule ulivyokuwa wakati wa Nyerere? Mbona wakati wa Nyerere kero nyingi zilikuwa zinaibuliwa toka upande wa pili, na sasa hakuna kero yoyote toka upande huo?
Hili pekee halikuonyeshi wewe kwamba huu siyo muungano aliouacha Nyerere?

Hilo la katiba ndilo tunaloendelea kuvutana nalo hapa. Kwa nini liwe doa wakati katiba ipo na inaweza kurekebishwa. Nyerere alisema isifanyiwe marekebisho yoyote kukidhi mahitaji yatakayokuwepo wa wakati husika?.
Kwa nini liwe doa wakati katiba hiyo hiyo ilihitajika kwa wakati wake?
 
Akiwa kama founder wa Taifa legacy ni kubwa zaidi kwa wakati wote
Sasa unatilia mashaka juu ya hilo, la kuweka misingi ambayo hawaa wengine wamekuja kuing'oa; au kuna jngine.

Kuna yeyote anayehoji jinsi Tanzania ilivyojengwa katika misingi ya kuheshimu utu wa waTanzania? Hiyo ndiyo 'legacy' unayoweza kupindisha lakini huwezi kuifuta.

Misingi iliyowekwa ilikuwa ni ya kumpa mTanzania heshima bila kujali tofauti miongoni mwetu; leo wanakuja wengine wanafanya kinyume na hayo, unasinmama kumlaumu Nyerere na siyo hao; kwa nini?
 
Msingi Nyerere aliuweka ni hii katiba mbovu ya mwaka 1977
 
Back
Top Bottom