Nyerere alipenda sana chama cha CCM kuliko nchi ya Tanzania

Nyerere alipenda sana chama cha CCM kuliko nchi ya Tanzania

Mabaya yake ni yapi; hayo ya marekebisho ya katiba wakati wake, na hakuwazuia kuendelea kufanya marekebisho kuendana na nyakati zenu?
Aliwaambia wapi msirekebishe?
Mwl Nyerere alifanya mambo mengi mazuri Sana kwa Tanganyika tena mazuri mno, lakini nia yake kama ya Kina Starlin ya kuungansha vyombo na vyama mpaka Leo vinalitafuna Nchi, hakuna namna ya kujinasua
 
Kwa sababu watu wa aina yako ambao mpo 'fixated' na kupigana na kivuli cha Nyerere badala ya kupambana na huyo Samia.
Sasa hili nalo ni la kujivunia ukiwa binaadam hai kweli?
Dr Samia mnamwonea tu, haihusiki nayeye kayakuta
 
Nyie wajinga mnamuona Nyerere kama Mungu wenu akiguswa tu mnatoa milio ya mbwa koko wajinga nyie
Wewe sina haja ya kuhangaika nawe leo hii, kwa sababu naona ni mbovu zaidi ya huyu niliye naye leo.
Subiri zamu yako siku nyingine.
 
Mwl Nyerere alifanya mambo mengi mazuri Sana kwa Tanganyika tena mazuri mno, lakini nia yake kama ya Kina Starlin ya kuungansha vyombo na vyama mpaka Leo vinalitafuna Nchi, hakuna namna ya kujinasua
Namna zipo nyingi sana; lakini hii ya kumlalamikia Nyerere siyo mojawapo.
 
Ukifuatilia hotuba za Nyerere nyingi utaona anailaumu katiba ya mwaka 1977 ambayo yeye ndo muasisi binafsi haya ni moja ya jambo linalofikirisha sana

Kwamba unatengeneza katiba alafu baadae unatumia mda kuiponda kwamba ni mbovu binafsi hili ni jambo ambalo binafsi mpaka leo linanifikrisha sana

Kwenye marekebisho ya katiba yote ambayo Nyerere alikuwa hai hakuna hata sehemu moja kwenye Marekebisho Nyerere alirekebisha katiba ili kuondoa madaraka makubwa ya Rais ambayo amekuwa akiyalalamikia jibu alikipenda chama kuliko nchi

Mabadiliko ya katiba ya mwaka 1977 wakati Nyerere akiwa hai
  1. Mabadiliko ya mwaka 1979
  2. Mabadiliko ya mwaka 1980
  3. Mabadiliko ya mwaka 1980
  4. Mabadiliko ya mwaka 1982
  5. Mabadiliko ya mwaka 1984
  6. Mabadiliko ya mwaka 1990
  7. Mabadiliko ya mwaka 1990
  8. Mabadiliko ya mwaka 1992
  9. Mabadiliko ya mwaka 1992
  10. Mabadiliko ya mwaka 1994
  11. Mabadiliko ya mwaka 1995

Mabadiliko 11 ya katiba yalifanyika wakati Nyerere akiwa hai ila cha ajabu haikuondoa mambo ambayo yanalalamikiwa kama madaraka makubwa ya Rais cha ajabu Nyerere mwenye alikuwa analalamikia madaraka makubwa ya Rais mpaka alinukuliwa akisema mkipata Rais mbovu atakuwa dikteta ila yakija mabadiliko haondoi hicho kinachomfanya Rais kuwa dikteta na kipo ndani ya katiba

Nyerere ni mwadilifu hili liko wazi hakuna anayebisha ila alisahau alitengeneza mfumo ambao unatoa mwanya kwa watu waliopewa dhamana kufanya ubadhirifu bila kichukuliwa hatua yeyote ile mfano katiba ya Tanzania inasema waziwazi bila kificho Rais akimaliza mda wake hatastakiwa hii ni hatari sana kama akipatikana Rais mbovu atafanya mambo akijua kabisa anakinga ya kutostakiwa swali la kujiuliza kwanini Nyerere aliruhusu kuwepo kwenye katiba sababu alikuwa ana uwezo wa kukitoa ila kwenye amendment zote zilizofanyika yeye akiwa hakuwa kukiondoa hiki kipengele ila akija majukwaani akawa anaendelea kulalamika madaraka ya Rais ni makubwa sana lakin jibu ni lile alikipenda sana chama kuliko nchi

Hata sasa hivi malalamiko ya katiba ni mengi ila sidhani kama kuna kiongozi aliyetoka ccm atakubali kuibadilisha katiba kama watu wengi wanavyodhani kwa sababu viongozi wengi wa ccm wanapenda chama kuliko nchi
Kweli kabisa
 
Shida yenu nyie mkishalewa BRUTAL, mnataka Nyerere alitakiwa KUMALIZA MATATIZO yote kwa 100%.

Nyerere amekuwa Rais Tanzania kwa miaka 24.


Mnabweka kuhusu mfumo, ila mkiulizwa kuhusu huo mfumo hamjui chochote.
Hata Wachina kama wangekuwa na mentality’s kama za wabongo wangekuwa mpaka sasa wanaendelea kumlaumu Mao tse Tung !
Kinyume chake ya Mao waliyaacha yakapita kama yalivyo pita wakayaanzisha mapya waliyoona yanafaa kwa wakati uliopo na sasa Dunia yote imebaki kuikodolea macho China ikiserereka matawi ya juu !
Nyerere alifanya aliyoweza kufanya na sisi tufanye tunayoweza kufanya sio kulalamika eti hakufanya hivi na hakufanya vile ! 😳
 
Jitahidi sana Uwe unapenda Kusoma vitabu itakusaidia Ili kuepuka Aibu ndogo ndogo mzee.
 
Hana mzigo wowote.
Alishautua siku ile alipoachia madaraka. Kaukabidhi kwetu sote tufanye lolote tutakalo na mzigo huo.

Hivi vyote ni vsingizio tu vya kukwepa mzigo tulioachiwa.
Nakuomba ukasikilze Hotuba ya Tundu Lissu siku Ile akiwa Kampala University Uganda " Conversation with Hon Tundu Lissu" akiwa na wanazuoni mbali mbali duniani.

That I the best speech I have ever listened to from Hon Tundu Lissu.

Nadhani hata Wewe utaipenda, siku Ile nilidhani Lissu hatatoka salama kwenye mikono ya M7, lakini M7 ni Mtoto wa Mjini
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia
Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.
tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.
Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.
Amina Tena Amina Amina Tena amina


UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MWALIMU JK NYERERE
 
Hata Wachina kama wangekuwa na mentality’s kama za wabongo wangekuwa mpaka sasa wanaendelea kumlaumu Mao tse Tung !
Kinyume chake ya Mao waliyaacha yakapita kama yalivyo pita wakayaanzisha mapya waliyoona yanafaa kwa wakati uliopo na sasa Dunia yote imebaki kuikodolea macho China ikiserereka matawi ya juu !
Nyerere alifanya aliyoweza kufanya na sisi tufanye tunayoweza kufanya sio kulalamika eti hakufanya hivi na hakufanya vile ! 😳
Nyerere akijenga TAIFA.

Mao alijemmnga TAIFA.

Wao kujenga UCHUMI wameshimdwa, lawama zote kwa Nyerere.

Nyerere ameacha ARDHI, WATU, MADINI bila hata kuchimba, KILIMO, VIWANDA ila leo wanauza mpaka HEWA (CARBON CREDITS) halafu lawama ni Nyerere.

Unaokea elfu 2, za Mwanasiasa MWIZI na MUUAJI halafu unamlaumu Nyerere.
 
Mtoa mada ameeleza mabadiliko ya katiba ambayo yote yamefanyika huyo nyerere akiwa hai, na kwenye hutoba zake analalamika madaraka ya rais kuwa makubwa and yet hakufanya chochote na alikuwa ana influence ya kufanya mabadiliko.
Anawezaje au angewezaje kuwa na influence ilihali alikuwa nje ya madaraka ?
Wakati wa Mwinyi alikuwa analalamika lalamika lakini hakuna chochote kilichobadilika katika yale aliyoyalalamikia na kwa Mkapa pia aliendelea kulalamika yale aliyoyaona yanaenda vibaya lakini hakuna chochote alichoweza kukibadilisha !
Ndio maana Waswahili Wanasemaga Nguvu ya mamba ni kwenye maji tu ! Nje ya maji hamuna kitu bandugu !
 
Unajuwa maana ya 'fact' ni nini?
Kwamba Nyerere alisema(aliagiza) pasiwepo na mabadiliko yoyote/nyakati zote katika uhai wa taifa hili; hizo ndizo "fact"?
Eti 'audacity', ni kitu gani kinachokufanya wewe uje hapa kuhoji nyakati tofauti na hizi ulizomo sasa. Kwa nini huna hiyo 'audacity' ya kuwahoji hao wanaokushibisha sana na kukutuma ukawakingie kifua kwa uchafu wanaofanya sasa na kuugeuza kuwa wa aliyofanya Nyerere?

Kwa nini huwahoji hao wa wakati huu, na unaona rahisi zaidi kuhoji ya nyakati tofauti kabisa na hizi zilizopo sasa?

Huna akili ya ya kukuwezesha kudadisi hayo, ila unayo tu ya kudadisi nyakati za Nyerere?
Acha kutetea ujinga na uchoyo wa huyo mchonga meno. Alipokuwa hai alikuwa Bado na nguvu yakuwashauri aliokuwa anataka wawe VIONGOZI wa nchi cha ajabu hakufanya hivyo!!. Kwahiyo matatizo na ubovu wa VIONGOZI huu umetokana na unafiki wake.
 
Back
Top Bottom