Nyerere aliwanyamazisha kimabavu Watanganyika walioitaka Tanganyika yao kwanini ?

Nyerere aliwanyamazisha kimabavu Watanganyika walioitaka Tanganyika yao kwanini ?

Hivi kuna kumbukumbu zozote za kiserikali kuonyesha kwambi hii ni nchi ya tanganyika?
au tutatizama kijiografia zaidi
maana sioni chochote kinachotuwakilisha kama watanganyika
yaani hatuna hata bendera!
 
Kilichomfanya nyerere kuushikilia muungano ni masharti kutoka kwa wakoloni kabla ya kutupa uhuru kamili.. ilikua lazima piga ua ili kuungana na zanzibar ili waarab wasije kujaa pale kwa kuwa na umoja na wazanibar matoeo yake kungekuwa na makundi ya kigaidi mengi sana na ingekuwa hatari kwa sisi bara huku
 
Kwa nini Nyerere aliwanyamazisha kimabavu Watanganyika walioitaka Tanganyika yao ?

Kwanini G55 walionekana sana wakosefu kisa kuidai na kuipigania nchi yao ?

Nyerere alikuwa ni nani hasa hapa nchi kuwaamulia Watanganyika wote kuhusu hatima ya nchi yao iwe hai au iuawe bila hata kujua wameridhia ama laah ?
Kama ambavyo miaka ya 60s kuliibuka wimbinma madikteta Afrika, kwa namna moja au nyingine hata Mwl aliathirik kidogo
 
Nyerere hakuwa Mungu, na km hakua Mungu basi Anakosea, na tunaposema makosa yake basi tunathibitisha ubinadamu wake.
 
Mnawapa vichwa tu ao vichwa upanga mzenji kakutana na bahati tu..kwa sababu ya ujinga wa mtangyika.
 
Kilichomfanya nyerere kuushikilia muungano ni masharti kutoka kwa wakoloni kabla ya kutupa uhuru kamili.. ilikua lazima piga ua ili kuungana na zanzibar ili waarab wasije kujaa pale kwa kuwa na umoja na wazanibar matoeo yake kungekuwa na makundi ya kigaidi mengi sana na ingekuwa hatari kwa sisi bara huku
Katu Tanganyika isingeweza tetemeshwa asilani kiusalama na hicho kiunguja na hicho kipemba.
 
Kwa nini Nyerere aliwanyamazisha kimabavu Watanganyika walioitaka Tanganyika yao ?

Kwanini G55 walionekana sana wakosefu kisa kuidai na kuipigania nchi yao ?

Nyerere alikuwa ni nani hasa hapa nchi kuwaamulia Watanganyika wote kuhusu hatima ya nchi yao iwe hai au iuawe bila hata kujua wameridhia ama laah ?
yule mzee alikuwa na upumbavu mkubwa sana wa kuamini anachowaza yeye tu ndicho bora na ndiyo maana alikuwa na mawazo ya kimaskini mpaka anakufa
 
Leo naona mmeugeuka baba wenu wa taifa mtakatifu wenu
Wote ninaweza kufukua makaburi mlivokuwaga mnamsifia
 
Nyerere aliulinda Muungano kiusalama zaidi, na ukiangalia Zanzibar kua Islamic state kamili ni rahisi nje ya Muungano,lazima kuwe na strategics kukabilia na hiyo hali,for short & long term
Hakuna mantiki hapo!
Kwani hao islamists wakiwa Islamic state kuna shida gani kwa nchi kubwa ya Tanganyika?? Wangeachwa huru wafanye mambo yao!

Sasa Tanganyika imeambulia kugeuka koloni la hao Wazenji kinyemela..

Tunataka jina halisi la makamu wa Rais mteule | JamiiForums Tanzania https://www.jamiiforums.com/threads...-makamu-wa-rais-mteule.2466750/#post-56727154
 
kwa sababu ya communism, zanzibar ni communist, kama siyo muungano ilikuwa iwe kama somalia ya siad bare, comoro, eritrea au north korea, ilikuwa hamna namna usisahau zanzbar ni umbali wa kama 50 km ktk kwetu bara hivyo haikuwezekana kuishi na communist as a neighbor, na haya yanayoendela leo ndiyo communist zanziibar yenyewe sasa ...
Wasilojua Nyerere baada ya mabalaa yaliyotokea kipindi hicho.
Ikabidi kuchukua maamuzi magumu ya kujichanganya na maadui.
Tatizo ni kwamba wale wenzetu akili zao ziko kwa waarabu huko oman.
Na sasa tunaona huu ujinga wa mpuuzi mmoja kapewa kiti akalie kimasihala tu anajua anachofanya.
Kila kitu ni Zanzibar na taka zote huko tunaokota sisi
 
Wa elfu mbili ,huwezi jua hata Nyerere alinusurika kupinduliwa akaokolewa na kikosi cha jeshi cha Malikia wa UK kililchokua na Base Kenya...
Hizo stori za muungano na Zanzibar ni kwasababu za kiusalama nilianza kuzisikia nikiwa darasa la tano mwaka 1991.
Huo ni uongo mtupu
 
Kwahiyo sababu ni zipi?
Hakuna sababu za msingi zaidi ya upuuzi tu muungano ambao Zanzibar ni kupe wa kwa kila kitu.

Mfano mdogo madini na mafuta ya Zanzibar sio mambo ya muungano ila Tanzanite, Almasi, Dhahabu, uranium n.k. za Tanganyika ni mambo ya muungano.

Zanzibar jumla ya wakazi wake hawawazidi wa DSM wana majimbo hamsini kwenye bunge la muungano wakati DSM ina majimbo kumi tu.

Zanzibar ina serikali yake Tanganyika haina hili halihitaji hata elimu ya kidato cha nne kujua kwamba muungano ni wakimagumashi tu.

Muungano una matatizo mengi sana.

Unafahamu jinsi ujerumani ya mashariki na magharibi zilivyoungana?
 
Back
Top Bottom