Nyerere na Wachina waliwezaje kujenga reli ya TAZARA kwa miaka minne tu KM zaidi ya 2000?

Naungana na hoja.
TAZARA ilijengwa kwa miaka mitano(5).
Ujenzi ulianza 1970 mpaka 1974.
Kwa siye tuliokuwepo miaka hiyo Mchina alitaka kwanza ku prove duniani kwamba teknolojia yake , spidi yake na uwezo kiujumla uko poa.
Na kweli alifanikiwa kuonyesha spidi kali ambayo katika ujenzi wa reli bado haijafikiwa mahali pengi duniani.

Umbali wa mradi kutoka Dar es salaam mpaka Kapiri Mposhi ni 1,860km, hii ni sawa kwa wastani kujenga kilometa 372 kwa mwaka.
Au kwa kulinganisha ni kama kujenga reli toka DSM Mpaka Mpwapwa kwa mwaka mmoja tu.

Ni dhahiri kuwa Mchina aliweka nguvu kubwa sana ya kifedha katika mradi maana alijua dunia nzima inautazama .
Miaka hiyo Marekani ilikuwa ikiubeza mradi na kuuita "The bamboo railway" ili kuukatisha tamaa.
Lakini Tanzania, Zambia na China hawakurudi nyuma.
Wakati huo huo, barabara ambayo iliitwa the TANZAM Highway ilikuwa ikijengwa na kampuni ya kimarekani, nafikiri ikiitwa Stirling Astaldi.
Pale Makambako yalitokea mapigano ya ngumi kali kalti ya wachina na wamarekani.
Mnaopita njia hiyo mnajua kwamba kuna muingiliano kati ya barabara na reli ya TAZARA pale Makambako.
Hizo ni simulizi za wakati huo.
TAZARA: How the great Uhuru Railway was built
 
Barabara haikujengwa na Wamarekani. Ni Waitaliano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…