Nyerere ndiye anayepaswa kubebeshwa mzigo wa lawama juu ya mfumo mbovu hapa nchini

Nyerere ndiye anayepaswa kubebeshwa mzigo wa lawama juu ya mfumo mbovu hapa nchini

Nyerere aliyeitawala Tanzania miaka hishirini na ushehe. Wananchi wa wakati wake walikuwa na uelewa mdogo wa mambo mbalimbali ikapelekea kumkubali sana huyu mtu.

Alikuwa na uwezo wa kubadili katiba ya nchi hii na kutupatia katiba yenye kuyapa majimbo, mikoa au wilaya mamlaka kamili.

Mfano kwenye hili suala la COVID 19 wakuu wa mikoa hawana mamlaka ya kufunga mikoa yao au kuamuru jambo lolote.

Sio kwenye issue ya COVID19, hata mambo ya kimaendeleo hakuna mkoa sasa unamamlaka ya kujipangia mambo yake.

Nyerere ulijilimbikizia nguvu kama mkoloni, ile nguvu umeirithisha kwa wengine nao wengine wamejiongezea nguvu zaidi.
Sikupendi Nyerere.
Pumbaf kabisa wewe, ndug Issa Hamdun, mbona mwinyi na kikwete hawakufanya kitu>
SEMA CCM ina matatizo ni ya kuitoa madarakani
 
Wahenga husema siyo vizuri kumsema marehemu. Tuanzie pale tulipoishia! Kati ya mwaka 2010 - 2013 tulifanikiwa kuanzisha Mchakato wa Katiba Mpya! Ndani ya ile Rasimu ya Katiba iliyosimamiwa na Tume ya Jaji Warioba, kulikuwa kuna mambo mengi tu mazuri;

likiwemo la kupunguza mamlaka ya Rais katika mambo mbalimbali, kuondoa vyeo kama vya Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kupunguza idadi ya Wabunge na watendaji wengine wa Serikali, nk

Sijui ni kwa bahati mbaya au makusudi! Rais wa wakati ule (JK) aliamua kujaza wanasiasa wengi na wataalamu wachache kwenye lile Bunge la Katiba. Baada ya hapo tunakumbuka mvutano uliokuja kujitokeza mwanzoni kabisa mwa mjadala kuhusu mfumo wa serikali, aidha uwe wa Serikali mbili kama zamani au uwe Serikali Tatu kama Rasimu ilivyopendekeza.

Hivyo basi kumlaumu Mwalimu Nyerere wakati huu ni kutafuta tu sababu nyepesi (ingawa hawezi kukwepa lawama hata hivyo) maana nafasi muhimu ya kurekebisha yale madudu ya Katiba ya mwaka 1977 tuliipata, ila mwisho wa siku JK, Ccm na Ukawa walitusababishia tuikose Katiba Mpya ya Wananchi kwa sababu zao tu binafsi.
Kwani ukawa ndio waliopendekeza kujazwe wanasiasa? Au ccm ndio tatizo iliyotaka kujaza wabunge wake ikiamini ndio wengi hivyo wataliteka bunge la katiba na kuwa la ccm ili ajenda zao za chama zipite?
 
Nyerere si Mkwawa,wala si Kimweri ,wala si Bushiri -Hawa ndio waliopambana na wakoloni.

Nyerere alikuwa pandikizi la wakoloni ili awe mkuu wa nchi baada ya wakoloni kuondoka.

Hta hivyo, Hakuwa smart sana kuongoza nchi kiuchumi,bali alijikita zaidi kwenye Mfumo wa kimasikini wa siasa za kijamaa ambao ulimfia mikononi mwaka mwaka 1983 hivi.

Sijui ni kwa vipi watu walimwita Baba wa Taifa, wakati Waislamu wa Tanzania wanayo malalamiko yao mingi tuu ya kukandamizwa kielimu na kupewa fevar wakiristo kinyemela hadi leo serikalini waislamu ni chini ya 20%.

Kulikuwa na Taasisi endelevu ya kiislamu iliyoitwa EAWMS ambayo ilikuwa inamiliki mashule ,vyuo vya elimu mbali mbali na

ilikuwa na Mpango wa kujenga vyuo vikuu nchini ili kuwasaidia waislamu ambao walikuwa nyuma sana kielimu kutokana na figisu za mkoloni.
-Mwalimu aliiua tasisi hii na kuunda Bakwata ambayo imekuwa jinamizi kwa waislamu wa Tanzania.

Nyerere Si Mchumi na ndo maana taifa hili limezama kwenye umasikini hadi leo.
Alikuwa mwana Historia na mambo ya Propaganda na hotuba tamu tamu za kuwalaza watu kifikra.Hilo alifanikiwa.
Nyerere hana udini acha uzushi hatari huo wa kidini, Rashid Kawawa katibu wake na pia alikuwa waziri mkuu ni muislam. Kweli hujui historia ya nchi jinsi Nyerere alivyopambana, hili ni juu yako kujifunza. Pia ujifunze jinsi uchumu wetu ulivyokuwa baada ya Azimio la Arusha mpaka wakati wa vita vya Uganda vilivyoua uchumi wetu.

Pia ujifunze vikwazo vya uchumi tulivyowekewa na Ulaya na Marekani baada ya Azimio la Arusha na kwa sababu ya kuisaidia ANC ya Afrika Kusini.

Inabidi ujifunze kwa nini Afrika ni masikini sio Tanzania tu, sababu kuu na mojawapo nitakupa. Hatuna teknolojia ya kutumia malighafi zetu kuunda wanayoounda Ulaya na Marekani. Mfano dhahabu, kwetu siye ni ya kuvaa tu wakati magharibi ni ya kutengenezea machine mbalimbali hata magari na ndege sio simu na computer tu. Hivyo wanatupangia bei ya kuuza mali zetu, tukisema hapana wanakataa kununua na kubaki nazo wenyewe bila matumizi makubwa nayo hivyo inatupasa tuuziane wenyewe kwa bei ndogo sana.

Waislamu wengi hawakuwa na elimu ya shule ila ya dini, hii ni kwa sababu wakoloni walisomesha wakristo tu, na waislamu wako busy na Kuran mpaka leo, zaidi ya masomo ya shule. Hata kwenye shule za kiislamu ni kuran inayotiliwa mkazo zaidi ya masomo mengine.
 
Back
Top Bottom