Wahenga husema siyo vizuri kumsema marehemu. Tuanzie pale tulipoishia! Kati ya mwaka 2010 - 2013 tulifanikiwa kuanzisha Mchakato wa Katiba Mpya! Ndani ya ile Rasimu ya Katiba iliyosimamiwa na Tume ya Jaji Warioba, kulikuwa kuna mambo mengi tu mazuri;
likiwemo la kupunguza mamlaka ya Rais katika mambo mbalimbali, kuondoa vyeo kama vya Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kupunguza idadi ya Wabunge na watendaji wengine wa Serikali, nk
Sijui ni kwa bahati mbaya au makusudi! Rais wa wakati ule (JK) aliamua kujaza wanasiasa wengi na wataalamu wachache kwenye lile Bunge la Katiba. Baada ya hapo tunakumbuka mvutano uliokuja kujitokeza mwanzoni kabisa mwa mjadala kuhusu mfumo wa serikali, aidha uwe wa Serikali mbili kama zamani au uwe Serikali Tatu kama Rasimu ilivyopendekeza.
Hivyo basi kumlaumu Mwalimu Nyerere wakati huu ni kutafuta tu sababu nyepesi (ingawa hawezi kukwepa lawama hata hivyo) maana nafasi muhimu ya kurekebisha yale madudu ya Katiba ya mwaka 1977 tuliipata, ila mwisho wa siku JK, Ccm na Ukawa walitusababishia tuikose Katiba Mpya ya Wananchi kwa sababu zao tu binafsi.