Nyerere tutakukumbuka na kuenzi kila kitu isipokuwa CCM!

Kwa Faiza Foxy unalisakama kanisa katoliki na Nyerere sujui kwa nini? Kifupi ni kwamba kanisa katoliki si tu kwamba ina rasilimali nyingi hapa TZ bali ni duni nzima nenda hata Marekani Shule na Hospital zote nzuri zinamilikiwa na kanisa hili,kwa hiyo si sahihi kusema Nyerere alipendelea kanisa katoliki. Je miaka yote hiyo baada ya yeye kutoka mbona bado kanisa katoliki lipo juu tena zaidi kulipo alipokuwepo???
Kifupi ni kwamba we unachuki binafsi na kanisa na Nyerere vitu ambavyo havitakusaidi hata ungefanya nini kanisa katoliki lipo juu tena zaidi ya unavyofikiri
All BEST form four results from ROMAN CATHOLIC
ALL BEST HOSPITALS FROM RC N.K
MTAJIJU!!!@@@
 
Hizo sifa za Nyerere ulizompa zote za uongo.

Amani na upendo ulikuwepo kabla ya ujio wake na hata alipotoka kwao kuja Dar alikaribishwa kwa amani na upendo na akapewa chumba, kula, kulala na akina Sykes, vijana wa mjini Dar enzi hizo.

Kuhusu Ukombozi wa Afrika Kusini, hilo ni changa la macho, si yeye, ilimbidi awepo kwenye mkumbo akipenda asipende. Wakimbizi kutokea Kusini kwenda Kaskazini wakimbilie wapi bila ya kuja Tanzania na kabla ya hapo Tanganyika?

Ni mfano wa Kenya na Somalia leo hii, Wasomali wengi wapo Kenya leo hii kuliko nchi nyingine yeyote duniani baada ya Somalia kwenyewe, kwa kuwa ndio wa karibu na ndipo kwenye ndipo kimbilio la karibu.

Kuhusu Ujamaa, atakumbukwa sana kwa kuwa huo ujamaa wake ndiyo uliifanya hii nchi kuwa masikini kukliko wote duniani.

Kiswahili, alikikuta kikiongewa Afrika Mashariki nzima, na yeye mwenyewe kakiri kuwa alikuwa hakijui vizuri akafundishwa na vijana wa Dar wa enzi hizo, kwa sasa tunawaita wazee wa Dar.

Umoja wa Kitaifa, Tanganyika ilikuwa na umoja wa Kitaifa toka enzi hizo, ndiyo maana Mzanaki akaweza kuja Dar na kupokelewa na kuishi bila bughdha.

La Idi Amin, hili lina mjadala mrefu sana wa kiitikadi za kidini.

Kwa kifupi sikioni cha maana cha kumsifia Nyerere ispokuwa kimoja tu, ni kweli kabisa anastahili kila sifa kwa kulikuza Kanisa Katoliki Tanzania na kulifanya ndiyo lenye kuhodhi ardhi kubwa Tanzania baada ya Serikali na kulifanya kanisa katoliki na wakatoliki kuwa wa mwanzo kwa kila jambo katika Tanzania. Kwa hili sibishi, ambalo wewe umelisahau hujaliweka kwenye sifa zake.
Kwa maandishi uliyoandika hapa umethibitisha bila shaka wewe ni mdini!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hata wewe na mchama wako msipomkumbuka heshima ya Nyerere (R.I.P) iko pale pale
kitaifa na kimataifa.
 
Dhambi za ccm ni nyingi sana goja nipite tu
 
Wanaomchukia Nyerere kwa chuki za kidini kama FaizaFox hawana hoja kabisa. Anasema wakimbizi wa kusini mwa Afrika walitakwa waje Tanzania kwani ni karibu. Yaani mtu aruke Namibia, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Botswana aje Tanzania alafu useme Tanzania ndo karibu???

Kuhusu Amin sijui mna hoja gani kwamba kuna suala la udini, mi natokea Kagera na nina ndugu Uganda. Sitaki mkaririshwe vitu vya ajabu! Uganda ni moja ya nchi ambazo watu wake hawabaguani kidini kama ilivyo kwetu, waislamu Uganda ni chini ya asilimia 15 lakini wanaheshimika sana. Ukatoriki ni dini kuu kule kwa sababu ya historia ya mashaidi wa Uganda lakini kuna umoja wa hali ya juu.

Baada ya kupinduliwa Amini nchi alipewa Prof Yusuf Rule ambaye ni mwislamu ingawa waliokuwa wanaoongoza mapambano ni wakristo akina Milton Obote na Yoweri Mseveni! Katika matukio makubwa ya kikatiri kufanya Amin aliwahi kumuua kwa mkono wake Askofu Luwumu. Pamoja na umaarufu wake mpaka kuna mtaa unaitwa Luwumu Street haikuwahi kuchukuliwa mauaji hayo kama ya kidini nchini Uganda.

Kuhusu kiswahili sikusema Nyerere alileta kiswahili, namaanisha alikifanya kuwa lugha ya taifa. Kwa kauli yake umesema alikuwa hajiu kiswahili, ndiyo! kama angetaka lugha ya kiswahili iwe kizanaki nani angekataa? Ndugu zetu mmeaminshwa kwamba Nyerere alikuwa mbaguzi na aliukuza ukatoriki! Kama kweli angetaka alikuwa na nafasi hiyo na saa hizi mgekuwa mnalia na kusaga meno!
 
Hizo sifa za Nyerere ulizompa zote za uongo.

Amani na upendo ulikuwepo kabla ya ujio wake na hata alipotoka kwao kuja Dar alikaribishwa kwa amani na upendo na akapewa chumba, kula, kulala na akina Sykes, vijana wa mjini Dar enzi hizo.

Kuhusu Ukombozi wa Afrika Kusini, hilo ni changa la macho, si yeye, ilimbidi awepo kwenye mkumbo akipenda asipende. Wakimbizi kutokea Kusini kwenda Kaskazini wakimbilie wapi bila ya kuja Tanzania na kabla ya hapo Tanganyika?

Ni mfano wa Kenya na Somalia leo hii, Wasomali wengi wapo Kenya leo hii kuliko nchi nyingine yeyote duniani baada ya Somalia kwenyewe, kwa kuwa ndio wa karibu na ndipo kwenye ndipo kimbilio la karibu.

Kuhusu Ujamaa, atakumbukwa sana kwa kuwa huo ujamaa wake ndiyo uliifanya hii nchi kuwa masikini kukliko wote duniani.

Kiswahili, alikikuta kikiongewa Afrika Mashariki nzima, na yeye mwenyewe kakiri kuwa alikuwa hakijui vizuri akafundishwa na vijana wa Dar wa enzi hizo, kwa sasa tunawaita wazee wa Dar.

Umoja wa Kitaifa, Tanganyika ilikuwa na umoja wa Kitaifa toka enzi hizo, ndiyo maana Mzanaki akaweza kuja Dar na kupokelewa na kuishi bila bughdha.

La Idi Amin, hili lina mjadala mrefu sana wa kiitikadi za kidini.

Kwa kifupi sikioni cha maana cha kumsifia Nyerere ispokuwa kimoja tu, ni kweli kabisa anastahili kila sifa kwa kulikuza Kanisa Katoliki Tanzania na kulifanya ndiyo lenye kuhodhi ardhi kubwa Tanzania baada ya Serikali na kulifanya kanisa katoliki na wakatoliki kuwa wa mwanzo kwa kila jambo katika Tanzania. Kwa hili sibishi, ambalo wewe umelisahau hujaliweka kwenye sifa zake.
umerogwa si bure na mganga wako kafa!!!! apo upo kwenye siku zako
 
Kwa Faiza Foxy unalisakama kanisa katoliki na Nyerere sujui kwa nini? Kifupi ni kwamba kanisa katoliki si tu kwamba ina rasilimali nyingi hapa TZ bali ni duni nzima nenda hata Marekani Shule na Hospital zote nzuri zinamilikiwa na kanisa hili,kwa hiyo si sahihi kusema Nyerere alipendelea kanisa katoliki. Je miaka yote hiyo baada ya yeye kutoka mbona bado kanisa katoliki lipo juu tena zaidi kulipo alipokuwepo???
Kifupi ni kwamba we unachuki binafsi na kanisa na Nyerere vitu ambavyo havitakusaidi hata ungefanya nini kanisa katoliki lipo juu tena zaidi ya unavyofikiri
All BEST form four results from ROMAN CATHOLIC
ALL BEST HOSPITALS FROM RC N.K
MTAJIJU!!!@@@
Nyerere asingepokonya shule za wakatoliki na kuwa za serikali leo hii asingeweza hata kuandika humu jamvinii, .. basi niseme tuwasamehe hawajui watendalo
 
Tuwe na utamaduni wa kukubali watu wenye uwezo hata kama tunatofautiana nao kiimani.
 
Kuna watu wanausongo na Nyerere,jina lake likitajwa wanakosa raha na kuonyesha chuki zao binafsi dhidi yake.
Ukweli utabaki hivyo hivyo Nyerere anastahili sifa kwa mazuri aliyoyafanya,ambayo yanazidi mabaya yake.
Kwa kauli yake alisema kwamba wao hawakuwa malaika kama binadamu kuna mabaya waliyafanya,na mazuri yapo lakini kilicho mshangaza waliofatia,badala ya kuendeleza mazuri walishikilia mabaya.
 
Nyerere, mwenyewe kakiri mara nyingi kuwa hajui kiswahili vizuri kafundishwa hao Wazee.

Nyerere kaja Dar es Salaam mwaka 1952 kawakuta watu wanaongea kiswahili leo mnakuja na drama zenu za kumsifia Nyerere kila kitu.

Yaani mtu atoke Butiama aje kuwafundisha kiswahili wakazi wa ukanda wa Pwani.

Ni kweli Kiswahili ni lugha ya PWANI ikiwa ni mchanganyiko wa kibantu na kiarabu. Ni kweli Nyerere alikuja mjini Dar akiwakuta watu wa PWANI wakizungumza kiswahili lakini mchango wa Nyerere kukipaisha Kiswahili haupingiki hata kidogo.
Nyerere baada ya kuchukua nchi akatangaza Kiswahili iwe lugha rasmi ya nchi, hata sisi wa vijijini tukalazimishwa kutumia lugha rasmi ya Kiswahili, tulishaandika vitabu kwa lugha zetu lakini Nyerere akatupiga stop, ndio maana anabidi apewe sifa kwa kuwafanya mamilioni ya watu waishio mbali na PWANI ya Tanzania kuzungumza Kiswahili. Asilingelifanya hili labda Kiswahili kisingekuwa maarufu kama kilivyo leo hii

Rekebisha, Nyerere alikuja Dar es salaam (Mzizima) akitokea Edinburg University sio Butiama.
 
Kwa hayo, mfahamishe mleta mada kuwa anapotosha anapoweka Kiswahili kama kama moja ya sifa za Nyerere.

Kwani mtoa mada kasema kimeletwa na Nyerere? Au amesema tutamkumbuka kwa mengi ikiwamo kiswahili? Kubali au ukatae Nyerere anao mchango wake hasa kisera kwenye kukifanya kiswahili kutumika kama lugha rasmi Tanzania
 
Ni kweli Kiswahili ni lugha ya PWANI ikiwa ni mchanganyiko wa kibantu na kiarabu. Ni kweli Nyerere alikuja mjini Dar akiwakuta watu wa PWANI wakizungumza kiswahili lakini mchango wa Nyerere kukipaisha Kiswahili haupingiki hata kidogo.
Nyerere baada ya kuchukua nchi akatangaza Kiswahili iwe lugha rasmi ya nchi, hata sisi wa vijijini tukalazimishwa kutumia lugha rasmi ya Kiswahili, tulishaandika vitabu kwa lugha zetu lakini Nyerere akatupiga stop, ndio maana anabidi apewe sifa kwa kuwafanya mamilioni ya watu waishio mbali na PWANI ya Tanzania kuzungumza Kiswahili. Asilingelifanya hili labda Kiswahili kisingekuwa maarufu kama kilivyo leo hii

Rekebisha, Nyerere alikuja Dar es salaam (Mzizima) akitokea Edinburg University sio Butiama.

Huyu jamaa na dada ake Faizafoxy hata historia inawapiga chenga, kwanza mtoa mada hakusema kiswahili kimeletwa na nyerere
 
kosa kubwa sana ambalo nyerere alifanya na bila shaka anaadhibiwa nalo mpaka sasa ni kutuachia ccm , maana sasa ni dhahiri kwamba SHETANI NI BORA KULIKO CCM !
 
Kwani mtoa mada kasema kimeletwa na Nyerere? Au amesema tutamkumbuka kwa mengi ikiwamo kiswahili? Kubali au ukatae Nyerere anao mchango wake hasa kisera kwenye kukifanya kiswahili kutumika kama lugha rasmi Tanzania

ubarikiwe sana .
 
Ni kweli Kiswahili ni lugha ya PWANI ikiwa ni mchanganyiko wa kibantu na kiarabu. Ni kweli Nyerere alikuja mjini Dar akiwakuta watu wa PWANI wakizungumza kiswahili lakini mchango wa Nyerere kukipaisha Kiswahili haupingiki hata kidogo.
Nyerere baada ya kuchukua nchi akatangaza Kiswahili iwe lugha rasmi ya nchi, hata sisi wa vijijini tukalazimishwa kutumia lugha rasmi ya Kiswahili, tulishaandika vitabu kwa lugha zetu lakini Nyerere akatupiga stop, ndio maana anabidi apewe sifa kwa kuwafanya mamilioni ya watu waishio mbali na PWANI ya Tanzania kuzungumza Kiswahili. Asilingelifanya hili labda Kiswahili kisingekuwa maarufu kama kilivyo leo hii

Rekebisha, Nyerere alikuja Dar es salaam (Mzizima) akitokea Edinburg University sio Butiama.

Nyerere kazaliwa EDINBURG?
 
pamoja na kwamba nimemsamehe NDUGU NYERERE makosa yake mengine yote , lakini naapa kwamba HILI LA KUTUACHIA CCM SITAMSAMEHE MILELE !
 
Back
Top Bottom