Nyie madogo mnaofaulu mitihani acheni kuwadanganya wenzenu kuwa mnamtegemea Mungu

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
2,395
Reaction score
2,391
Ukisikiliza vijana wengi waliofanya vizuri kwenye mitihani yao wanadai ni Mungu tu.

Maswali ya kujiuliza
1. Swali linakuja je waliofeli wao hawakumtegemea?
2. Hawakusoma ila Mungu ndio aliwapa majibu au?
3. Kuna wasioamini Mungu lakini wanafanya makubwa,wao wanamtegea nani?

Ushauri wangu kwao. Kabla hujasema ni Mungu, anza kutaja jitihada/mbinu ulizotumia kusoma na kufaulu alafu Mungu akakusaidia na sio kuwaingiza choo wengine.

Hakuna Mungu anaeweza kumsaidia mjinga. Madhara ya kauli hizi ni kuathirika kwa vijana wengine ambao bado hawajamaliza,wanaweza kuamua kuacha kusoma na kushinda makanisani kumsubiri Mungu afanye miujiza kwenye mitahani yao.
 
Nadhani ulimuelewa vibaya, anamtanguliza Mungu katika masomo yake, kama Rais wetu anavyosisitiza, kwamba tumtangulize Mungu kwa kila jambo (la heri) tufanyalo. Hata Mungu mwenyewe amesema jisaidie (jitahidi) nami nitakusaidia.
 
Sasa umeajiriwa,kazi uliomba mwenyewe,ukakubali ofa ya mshahara na mkataba ukasaini mwenyewe kwa akili zako timamu,unanyonywa wapi mkuu.Fanya ile kazi ambayo hunyonywi.
 
Habari za Mungu ni kama kibwagizo tu mzee usichukulie serious..
Watu wanatoa rushwa za ngono wapande vyeo, wanahonga wapate kazi, mwingine kapata kazi kwa connection tu ila utasikia ni Mungu tu, Omba Mungu.

Ni moja ya kauli inayodumaza akili za waafrika, hata watu wenye pesa/mafanikio wanaamini Mungu ndo kawapa!
 
Nadhani ulimuelewa vibaya, anamtanguliza Mungu katika masomo yake, kama Rais wetu anavyosisitiza, kwamba tumtangulize Mungu kwa kila jambo (la heri) tufanyalo. Hata Mungu mwenyewe amesema jisaidie (jitahidi) nami nitakusaidia.
Sasa wao hawasemi mbinu walizotumia kufaulu,kitu ambacho ni kibaya kwa vijana wajao
 
Kwa mtu yoyote mwenye kumuamini Mungu lazima atamuweka Mungu mbele kwa chochote hata kama ni kidogo maana anajua juhudi zake zimefanikiwa kwa msaada wa Mungu.

Na ikumbukwe tu katika kufanikiwa kila mtu ana njia zake na bahati yake. Tunaweza wote kwenda njia sawa ila mwisho wa siku matokeo yakaja tofauti.
 
Sio hao madogo tu, hata matajiri wengi waliopata utajiri wao kwa dhulma na unyonyaji wa wafanyakazi wao hupenda sana kuanza na huo msemo.
Ndio mana unakuta mijitu imekopa badala ya kufanya kazi yalipe yanaenda kukesha makanisani yakisubiri Mungu awafutie madeni yao
 
Habari za Mungu ni kama kibwagizo tu mzee usichukulie serious..
Watu wanatoa rushwa za ngono wapande vyeo, wanahonga wapate kazi, mwingine kapata kazi kwa connection tu ila utasikia ni Mungu tu, Omba Mungu.

Ni moja ya kauli inayodumaza akili za waafrika, hata watu wenye pesa/mafanikio wanaamini Mungu ndo kawapa!
Kabisa mkuu,usipokuwa makini utadumaa kwa kuamini
 
Habari za Mungu ni kama kibwagizo tu mzee usichukulie serious..
Watu wanatoa rushwa za ngono wapande vyeo, wanahonga wapate kazi, mwingine kapata kazi kwa connection tu ila utasikia ni Mungu tu, Omba Mungu.

Ni moja ya kauli inayodumaza akili za waafrika, hata watu wenye pesa/mafanikio wanaamini Mungu ndo kawapa!
Hahahaaa
 
Kwa mtu yoyote mwenye kumuamini Mungu lazima atamuweka Mungu mbele kwa chochote hata kama ni kidogo maana anajua juhudi zake zimefanikiwa kwa msaada wa Mungu.

Na ikumbukwe tu katika kufanikiwa kila mtu ana njia zake na bahati yake. Tunaweza wote kwenda njia sawa ila mwisho wa siku matokeo yakaja tofauti.
Kwa hiyo ukienda kuiba na kufanikiwa bila kuonekana napo ni Mungu kakusaidia?
 
lazima atamuweka Mungu mbele kwa chochote hata kama ni kidogo maana anajua juhudi zake zimefanikiwa kwa msaada wa Mungu.
Nimenukuu hapo☝️. Ila tambua sio mafanikio yote yanatokana na Mungu
 
Sijaona ulipopinga kwamba huyo aliyefauru hayupo sahihi bali nimeona umekubali kuwa yupo sahihi ila aongeze maneno kuwa alifanyajefanyaje pia.
 
Nimenukuu hapo☝️. Ila tambua sio mafanikio yote yanatokana na Mungu
Wapo wanaotumia nguvu za giza katika kufanikiwa. Ndio maana mwanzo nimesema kwa wanaomuamini Mungu.
Hao wanaotumia njia zingine siwezi kuwaongelea.
 
Nadhani ulimuelewa vibaya, anamtanguliza Mungu katika masomo yake, kama Rais wetu anavyosisitiza, kwamba tumtangulize Mungu kwa kila jambo (la heri) tufanyalo. Hata Mungu mwenyewe amesema jisaidie (jitahidi) nami nitakusaidia.
Wewe ndy umeelewa vibaya, soma alichosema yule dogo Tanzania one harafu soma thread vizuri.
 
Back
Top Bottom