Nyie madogo mnaofaulu mitihani acheni kuwadanganya wenzenu kuwa mnamtegemea Mungu

Nyie madogo mnaofaulu mitihani acheni kuwadanganya wenzenu kuwa mnamtegemea Mungu

Ukisikiliza vijana wengi waliofanya vizuri kwenye mitihani yao wanadai ni Mungu tu.

Maswali ya kujiuliza
1.Swali linakuja je waliofeli wao hawakumtegemea?
2. Hawakusoma ila Mungu ndio aliwapa majibu au?
3. Kuna wasioamini Mungu lakini wanafanya makubwa,wao wanamtegea nani?

Ushauri wangu kwao. Kabla hujasema ni Mungu,anza kutaja jitihada/mbinu ulizotumia kusoma na kufaulu alafu Mungu akakusaidia na sio kuwaingiza choo wengine.

Hakuna Mungu anaeweza kumsaidia mjinga. Madhara ya kauli hizi ni kuathirika kwa vijana wengine ambao bado hawajamaliza,wanaweza kuamua kuacha kusoma na kushinda makanisani kumsubiri Mungu afanye miujiza kwenye mitahani yao.
Hata kwenye soka hivyo hivyo,mambo ya imani kila mahali.Mungu ni wa wote na siyo kwa wanaofaulu tu.Waambie wajifunze,na hali hii ipo kwenye nchi za dunia ya tatu.
 
Kwa mtu yoyote mwenye kumuamini Mungu lazima atamuweka Mungu mbele kwa chochote hata kama ni kidogo maana anajua juhudi zake zimefanikiwa kwa msaada wa Mungu.

Na ikumbukwe tu katika kufanikiwa kila mtu ana njia zake na bahati yake. Tunaweza wote kwenda njia sawa ila mwisho wa siku matokeo yakaja tofauti.
Kuna jamaa ni jambazi sugu na ameshaua sana tuu, lakini ukiingia kwenye gari lake ni nyimbo za dini mwanzo mwisho, kiufupi wengine wanasema tuu Mungu kwa kumdhihaki na kuwaonyesha walimwengu but matendo yao mabaya tuu.
 
Sio hao madogo tu, hata matajiri wengi waliopata utajiri wao kwa dhulma na unyonyaji wa wafanyakazi wao hupenda sana kuanza na huo msemo.
mbona kama unamsema mwamedi kwani kakukosea nini?
 
Kuna jamaa ni jambazi sugu na ameshaua sana tuu, lakini ukiingia kwenye gari lake ni nyimbo za dini mwanzo mwisho, kiufupi wengine wanasema tuu Mungu kwa kumdhihaki na kuwaonyesha walimwengu but matendo yao mabaya tuu.
Wapo wa hivyo wengi, la muhimu mtu ni kutenda yaliyo mema ili mwisho wa siku uishi kwa amani
 
Hata kwenye soka hivyo hivyo,mambo ya imani kila mahali.Mungu ni wa wote na siyo kwa wanaofaulu tu.Waambie wajifunze,na hali hii ipo kwenye nchi za dunia ya tatu.
Ndio mana tunafeli mambo mengi sababu ya kauli hizo za kijinga. Sa kama wote mnamtegemea Mungu basi washinde wote
 
Unajua madhara yake? Kwani hakuna waliokuwa wanasoma na wamefeli?
Mkuu tujadiri vitu vilivyo na fact kuelewana

Mimi noseme Mungu ananipenda wewe useme kauri yangu nimemaanisha wewe upendwi na Mungu Huu si udikteta kabisa tena wakidini na kiimani

Ok jirani yangu kafeli nilovyomuuliza kasema yote ni mapenzi ya Mungu mimi nataka nimshitaki kwanini aseme hivyo kwahiyo anamaanisha mdogo wangu aliyefauru Mungu hana mapenzi nae.
 
Nadhani ulimuelewa vibaya, anamtanguliza Mungu katika masomo yake, kama Rais wetu anavyosisitiza, kwamba tumtangulize Mungu kwa kila jambo (la heri) tufanyalo. Hata Mungu mwenyewe amesema jisaidie (jitahidi) nami nitakusaidia.
Hili andiko lipo kwenye kitabu gani
 
Mkuu tujadiri vitu vilivyo na fact kuelewana

Mimi noseme Mungu ananipenda wewe useme kauri yangu nimemaanisha wewe upendwi na Mungu Huu si udikteta kabisa tena wakidini na kiimani

Ok jirani yangu kafeli nilovyomuuliza kasema yote ni mapenzi ya Mungu mimi nataka nimshitaki kwanini aseme hivyo kwahiyo anamaanisha mdogo wangu hana Mungu hampendi ndio maana kafauru
Ww sikuelewi kabisa,nyie ndio mnamuona Mungu mbaya
 
Unachomaanisha ni kuwa mungu mbaguzi? Kwamba dogo huyu amefaulu na huyu amefeli yote ni mapenzi ya mungu!!!🤔🤔🤔 Dah!!
wewe jamaa ni mweupe sana kichwani

Again

wewe una ubongo mdogo Sana, umeshindwa kuelewa nilichoandika aisee sichangii tena hii mada.
 
Ukisikiliza vijana wengi waliofanya vizuri kwenye mitihani yao wanadai ni Mungu tu.

Maswali ya kujiuliza
1.Swali linakuja je waliofeli wao hawakumtegemea?
2. Hawakusoma ila Mungu ndio aliwapa majibu au?
3. Kuna wasioamini Mungu lakini wanafanya makubwa,wao wanamtegea nani?

Ushauri wangu kwao. Kabla hujasema ni Mungu,anza kutaja jitihada/mbinu ulizotumia kusoma na kufaulu alafu Mungu akakusaidia na sio kuwaingiza choo wengine.

Hakuna Mungu anaeweza kumsaidia mjinga. Madhara ya kauli hizi ni kuathirika kwa vijana wengine ambao bado hawajamaliza,wanaweza kuamua kuacha kusoma na kushinda makanisani kumsubiri Mungu afanye miujiza kwenye mitahani yao.
Ndugu mbona kama vile una Jazba nao sana hivi? au labda Wewe Mwenyewe enzi zako pamoja na Wanao wa sasa hamjawahi hata Kufaulu Shule?
 
Mkuu serious kabisa??
Ok jirani yangu kafeli nilovyomuuliza kasema yote ni mapenzi ya Mungu
Kufeli kwa jirani yako ni mapenzi ya Mungu? Na yule aliefaulu? Mbona kama mungu anabagua wakufaulu na wakufeli sasa? Huyo mungu gani?
 
Back
Top Bottom