Ukisikiliza vijana wengi waliofanya vizuri kwenye mitihani yao wanadai ni Mungu tu.
Maswali ya kujiuliza
1.Swali linakuja je waliofeli wao hawakumtegemea?
2. Hawakusoma ila Mungu ndio aliwapa majibu au?
3. Kuna wasioamini Mungu lakini wanafanya makubwa,wao wanamtegea nani?
Ushauri wangu kwao. Kabla hujasema ni Mungu,anza kutaja jitihada/mbinu ulizotumia kusoma na kufaulu alafu Mungu akakusaidia na sio kuwaingiza choo wengine.
Hakuna Mungu anaeweza kumsaidia mjinga. Madhara ya kauli hizi ni kuathirika kwa vijana wengine ambao bado hawajamaliza,wanaweza kuamua kuacha kusoma na kushinda makanisani kumsubiri Mungu afanye miujiza kwenye mitahani yao.