Wanawake waomba msamaha wapo bado.
Hapa kwenye kuombwa msamaha na kukiri makosa ndipo ulipo wa wanaume Wengi. Yaani mwanamke wangu hata awe amenikosea kosa kubwa namna gani nikisikia tu kakiri kosa na kuamba samahani dah najikuta nampenda mara 100 zaidi.
Kuna kibinti cha kichaga tuna-ukaribu wa kama wiki mbili ivii tuu, juzi ktk stori stori tulitofautiana kidogo, mimi nikaona miyeyusho nikasepa, ajabu kumbe akawaza kuwa nimeondoka kwa shari na hasira. Aisee kalinitumia texts za samahani ilihali mimi sioni hata kosa kabisa. Mimi nikajibu tu "OK" nikijua ni hali ya kawaida tu walaa hajanikosea kitu. Ajabu leo nikampigia simu kwa ajili ya stori stori zingine tu, si kakakumbushia kuhusu tukio la nyuma kuwa eti msamaha wa meseji hautoshi anataka kuomba msamaha wa mdomo, msamaha wa sauti.