Nyimbo gani umekua nazo na ukizisikia zinakukumbusha utoto au ujana wako?

Wataalam wanasema muziki uliousikiliza ukiwa na takribani miaka 13 ndio huwa taste yako ya muziki. Muziki wa kikongo ndio muziki ambao nimekuwa nao nyumbani kwetu miaka ya 1990 akisikiliza mzee. Pia Chaka Chaka, Whitney, Abba zilikuwa ni ngoma za mama yangu. Braza wangu mmoja ndiye aliyenitambulisha kwenye hip hop ya Tupac. Uncle wangu yeye alikuwa ni mzee wa reggae. No wonder hadi leo, Reggae, Rhumba Congolese na Rap ndio miziki niipendayo.

Hii album ya Koffi ya V12 ndio album naisikiliza toka niko Primary School Tabora 1990s hadi leo hii, 2025, March 06 saa 5 na dakika 48 usiku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…