Nyimbo ya Lil' Wayne "Mirror" ina ujumbe mkubwa sana

So Lil Wayne anamaanisha unabidi kumpenda Sana rafiki yako ambaye huwa ukijitazama kwenye kioo unamuona ambaye ndo wewe
Sio hio tu, tafuta nyimbo inaitwa 'Abortion' au huko mbali tafuta 'Sweetest Girl' kisha sikiliza lines za Wayne mule uelewe, anakwambia 'and then she runs to the pastor, and she feels no different after, and then she ask him (where my money at)?'

Hii kawaimbia Malaya wanaotaka kuokoka Ila still bado wanahitaji Pesa ili waishi amekimbilia kanisani kwa Mchungaji ila baadae anaona hakuna kinachobadirika anamuuliza Mchungaji wewe unaingiza Pesa za sadaka Mimi Pesa yangu ipo wapi? Yaan Mchungaji kapita nae
 
lil Tunech ni mkali ya Commercial
Tafuta ngoma yake moja inaitwa 'I am Me' utamuelewa, nyingi ya nyimbo zake zina ujumbe mahususi

Kuna lines anasema:

And we hold court and take your life for a settlement
Yes, I'm the best
And no, I ain't positive, I'm definite
I know the game like I'm reffin' it
This is Tha Carter, Tha Carter 3, the New Testament
And I'm the God
And this is what I bless 'em with
 
Huyo nyimbo zake nyingi zimebeba jumbe Kali sana hajawahi Tunga wimbo pasi na ujumbe
Na ni bright Carter 111
 
Mimi mbona nikijiangalia kwenye kioo namuona mtu mwingine?
Huyo ndio namuamini, kwamba hatoweza kuniacha ktk nyakati zote.
Sio kwamba sijiamini, lah! Peke yangu siwezi.

Lakini, huo wimbo naupenda na hata Wayne nampenda pia.
Kila unapojiangalia na kujiona kwenye kioo kwa nyakati zote unazopitia mbaya, ngumu za hatari na nyakati nzuri zote unajiona kiutofauti kulingana na huo wakati. Na always unapopitia magumu ww pekee ndoo wakujipa moyo kwanza. Hii nyimbo binafsi nailewa na kwa playlist yangu ipo
 
Kwa sababu ulikuwa haujazaliwa au ulikuwa mdogo wakati Tupac Amar Shakur anatema madini ya kibabe.
Lets play a game, taja wimbo mmoja wa Tupac wenye madini then nakujibu kwa wimbo wa wayne hadi mmoja wetu atakapoishia njiani.

Tupac mwana harakati tu yule, ni kama hapa Tz Ushindanishe fid q na roma
 
Huu wimbo✔️ (mmoja)
Wimbo wa...✔️ (mmoja)

Nyimbo hizi✔️ (nyingi)
Hizi nyimbo✔️ (nyingi)
Nyimbo za.....✔️ (nyingi)
Nyimbo hii..❌ (siyo Kiswahili sanifu)
Hii nyimbo...❌
Nyimbo ya....❌ (siyo Kiswahili sanifu)
 
Acha kutuharibia lugha yetu adhimu. Nyimbo ni kiti gani? WIMBO mmoja tu utauitaje NYIMBO? Bibi FaizaFoxy njoo huku uone kuna washenzy wanatuharibia lugha
 
Huu wimbo✔️ (mmoja)
Wimbo wa...✔️ (mmoja)

Nyimbo hizi✔️ (nyingi)
Hizi nyimbo✔️ (nyingi)
Nyimbo za.....✔️ (nyingi)
Nyimbo hii..❌ (siyo Kiswahili sanifu)
Hii nyimbo...❌
Bora umesema wewe mkuu maana ningesema mimi ingekuwa nongwa. Hawa vijana wanatuharibia sana lugha yetu adhimu ya Kiswahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…