OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Sikuandika kitu mara baada ya uchaguzi japo nilishuhudia kilichotokea. Kuna makosa kadhaa ambayo CCM wanayafanya ili ku-justify yaliyotokea niwaambie vijana wa CCM Mkae kimya maana mnajiharibia katika siasa za kimataifa. Na ninaamini wengi mnapenda kuja baadae kufanya siasa za kimataifa ili kuiwakilisha Tanzania katika majukwaa makubwa. Hali ya kutetea uvunjaji wa haki za binaadamu ambayo zinakemewa na taasisi za ndani na nje ni upuuzi sio siasa.
Mathalani, kwa wanaosema waandamanaji walikuwa wezi au vibaka, hii ni hoja mbovu kwa kuwa wote tunajua mtuhumiwa wa wizi hupelekwa kwenye vyombo vya sheria. Kutetea watu kuuawa kwa tuhuma za wizi hata kwa "Mob justice" ni kutoelewa haki ya kuishi na usawa kabla ya sheria. Aidha! Uko ushahidi wa watu kuuawa wakiwa nyumbani kwao suala ambalo linaleta maswali mengi zaidi kwa hao wanaotetea waandamanaji kupigwa risasi za moto.
Ni busara kukubali kuwa ni makosa yametendeka na kuwaomba radhi watanganyika badala ya kukaza shingo kipindi hiki. Huu ni wito kwa vijana wote ambao naona ufahamu wao kuhusu HAKI unaathiriwa na siasa chafu.
Nimeona video kadhaa za watu wakiwazika wapendwa wao huku wakiimba nyimbo za kishujaa. Hii ni tofauti sana na tabia za watanganyika za kulia wakati wa kuzika. Hii ni ishara ya maumivu yaliyopita ukomo. Pia zimeshaibuka ishara ya watu walioumizwa kuwa tayari kufanya lolote ili kupunguza maumivu. Hili suala la watu kutaka kufanya lolote likikutana na vijana wa CCM ambao wanaona sahihi watu kuuawa litaleta shida. Watu wanaweza kufuatwa na wakakumbwa na Mob Justice ambayo haitakuwa nzuri kwa ustawi wa nchi.
Huu sio wakati wa kutumia vijana wenye maneno machafu, bali muda wa kutumia busara. Wala sio muda wa kuona chama kinalinda mtu kwa kuwa nyumbani kwako uko mwenyewe na mobb justice inaweza kukufanyia jambo baya. Hat hili suala la Desemba 9, linaweza zimwa kwa busara na sio kutumia vijana wa ovyo.
Huu ni wito wa kuangalia mtukio na kuamua kwa busara.
Nawasilisha