Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Hahahahaahha.... I Kanti You!! Mimi mvivu wa kucheza toka utotoni nitakuwa nawashangalia wewe na kaka B hapo mkiingia Kati....

Hahahahaa wala usijali tutawaburudisha vya kutosha. Muwe na mbavu za ziada tuu na muandae noti za kututunza looh heheheheheh
 
Ha ha ha ha hapo una paka mate mkononi ......ile ya kuimba mko mduara (kama una wako mshike kiuno chini kwa chini ehee chini kwa chini)

Nimekumbuka huu wimbo.....

Mnara Mnara Mnara njiwa, akija baba ntamwambia kitanda chako kimelaliwa...
Kunguru mweupee kakosa mkia..
Mnara Mnara. .
Ukitaka kwenda moshi... moshi kuna umandee moshi
Ukitaka kwenda Tanga? Tanga kuna umandee Tanga ukitaka kwenda lindi lindi kuna umandee lindii
Mnaaara Mnaaara Mnaaara


cc: RRONDO
 
Kuna huu pia....
Kanadianii eeehh wa Upanga eeeh
Mzuri sana eeeh ana akili eeeh
Chumaa kinalia aaaahh acha aaah chumba ssshhh
Chumaa kinalia aah aah aaah chumba ssshh

Safari ya shule naiombea baraka
Safari ya shule naiombea barakaa
Nikamwambia mama eeh
Kwaheri nakwendaa
Kusoma masomo yangu ya leeooo
Nikamwambia baba eeh
Kwaheri nakwenda
Kusoma masomo yangu ya leo

Oohh mama kwaheri mama nakwenda zangu shule oooh oohh kwaheri mama nakwenda zangu shule
Ooh mamaa furaha mama nakwenda zangu shule ooh oooh kwaheri mama nakwenda zangu shule..

Nakwenda Upanga kwaheri mama nakwenda zangu shule
Nakwenda olimpio kwaheri mama nakwenda zangu shule
Nakwenda mzizima kwaheri mama nakwenda zangu shule...
Ooh mama mama furaha mamaa.......

cc: RRONDO
 
yai bovu yai bovu linanuka linanuka linanukaje linanukae pwii pwii sembwela
 
Aaahahahahahhahahahahahaaa aahahahahahhaahahhaahhahahahaa eehehehehehehehehheheheeeee yaani weweee umenifanya nicheke kwanguvu hapa nilipo loooh
Nimevuta taswira jinsi ulivokuwa unaimba huo wimbo kwanguvu bila wasiwasi unashangaa unavutwa ndani paaah paaah kichapo loooh.

Pole mwaya looh nimecheka hadi machozi looh.
Hahahaaa hahaha du sio kwa kichapo kile maana nilihisi naishiwa damu asingekuwa bibi kusema nmetosha ningekufa wallah
 
Mtu mmoja ana kidendele,
Keshokutwa tutamnyoa nywele.

Hehehehehehehehee haki ya nanihii
Huu ilikuwa unamuwekea mtu kitu chochote mfano ganda la nyanya kichwani bila yeye kujua halafu unaanza kuimba .......

Mtu wangu ana kideengeelee
Kesho kutwa nitamnyoa nyweleee
Hahahahahahhaaa basi ukisikia hivyo unaanza kujipukuta kama umewekewa kitu mwilini au kwenye nguo looh.

Halafu hiyo ID yako nakumbuka zamani enzi zile maikalus bado yapo mjini, kulikuwa na daladala moja linaitwa Chakochangu.
 
Moja chama chetu cha umoja
Mbili macho kama pilipili
Tatu, Tatu mwizi wa mapera
Nne:mwanne acha uhuni
Tano, kwa mchuzi wa manjano
Sita,baharini kuna vita
Saba,sabasaba imefika
Nane,zunguruka tuonane
Tisa,kwa Mzungu kunatisha
Kumi, kwa magumi na mateke

Huu wimbo sisi tulikuwa tunaimba hivi
Moja ........(nimesahau)
Mbili, taa ya kandili
Tatu, mwali kaliwa na chatu
Nne, tumpate tumchune
Tano ,kapika wali manjano
Sita, waarabu waenda vita
Saba, ndiyo siku ya mahaba
Nane, ingia ndani tuagane
Tisa,tisatisa ya tisini
Kumi,kwa mateke na magumi.
Ukifika hiyo kumi unampiga aliye karibu yako ngumi au teke.
 
Hehehehehehehehee haki ya nanihii
Huu ilikuwa unamuwekea mtu kitu chochote mfano ganda la nyanya kichwani bila yeye kujua halafu unaanza kuimba .......

Mtu wangu ana kideengeelee
Kesho kutwa nitamnyoa nyweleee
Hahahahahahhaaa basi ukisikia hivyo unaanza kujipukuta kama umewekewa kitu mwilini au kwenye nguo looh.

Halafu hiyo ID yako nakumbuka zamani enzi zile maikalus bado yapo mjini, kulikuwa na daladala moja linaitwa Chakochangu.

Kweli mtu wangu,huu utandawazi umebadili mifumo yetu ya maisha.
 
Mama wa kambo, mbo
Mbona wanitesa sa
Sasa naondoka ka
Kaa peke yako ko
Koti la babu bu
Bubu asemi mi
Mimi nasema ma

Mwengine aendelee..

Hizi nyimbo hata origin haijulikan..!
bubu hasemi ,,mi
mimi na wewe,, we
wembe wa kucha,, cha
chakula kitamu,, mu
mungu mkubwa,, bwa
bwawa la samaki,, ki
king majto,, to
tone la maji,, ji
jitu la kale,, le
lenye midevu,, vu
vumbua samaki

inaendaa mwisho tausiii ndege wangu ndege wangu wa thamani

dah kumbe nna kumbukumbu bado aiser
 
Ana Ana Ana do,
Kachanika basto,
ispiringi matingo,
kajamba, ushuzi unanuka, tena sana, sana kabisa.
Nadhani huu wimbo ulikuwa wa kizungu ukaswahilishwa, kama kuna mtu anaujua asili yake anaweza kutuhabarisha.
Hahahahahaaa!!! Hapa, nipo kwenye kikao. Nimecheka kimya kimya baada ya kuona huu wimbo.
 
Namtafuta mke wangu X2
Hapa hayupo X2
Kaenda wapi X2
Kaenda kusuka X2
Chanuo kampa nani X2
Kampa msusi X2
Pesa kampa naniX2
Kampa msusi X2

Nina ndoo yangu
Eeeeh
Yakuteka maji
Eeeeh
Maji ya dhahabu
Eeeeh
Watoto msitizame nyuma X2
Yai bovu linapita X2
 
Vipi yange yange walishawahi kukupa kucha nyeupe? Wakipita juu tulikuwa tubaimba
Yange yange nipe kucha nyeupeee....
Cha ajabu kweli kwenye kucha kunatokea vidoa vyeupe!
Aisee..! Hii mechanism yake sikuielewa kabisaa..! Yaani vinatokea kabisa vidoa vyeupe hasa kidole cha kati..!
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Back
Top Bottom