Nyoka Mwenye Kichwa Kidogo sana umbo kubwa eneo la katikati na Mkia Mwembamba

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,600
Reaction score
59,760
Wakuu, kwamba naomba msinichoke hapa kuna kitu kinaniumiza kichwa sana sielewi. Hapa majuzi katika pitapita zangu za hapa na pale humu nyumbani ndani nimepishana na nyoka ana kichwa kidogo sana ila katikati ni mnene balaa na ana mkia mdogo. Kwanza najua wapo wadau watasema leta picha, sikia wakuu nyoka huyu ni moja ya nyoka wanaokimbia sio kawaida.

Nilipomuona nikajaribu kumfuata ili nimtulize hata kwa fimbo na mawe ili asilete madhara au vinginevyo ila alikimbia vibaya sana ni moja kati ya nyoka niliowashuhudia wakikimbia kwa kasi ya ajabu hatimae alitoweka ghafla sikumuona tena. Lakini huyu nyoka yupo humu humu tunamoishi hajawahi kumdhuru mtu nadhani anaogopa watu ila ninahofia siku mtu akikosea bahati mbaya mguu hauna macho na nyoka katoka kwenye harakati zake bahati mbaya akamkanyaga itakuaje?

Humu najua wapo wadau wanajua mambo mengi ya wanyama km hawa, hivi kwa nyoka km huyu ambae anazunguka tu eneo hili hili hamdhuru mtu ila anazunguka tu, tunafanyaje ili aondoke? Utauliza kwanini usimtafute? Anajificha na hakuna mtu mwingine amemuona zaidi yangu. Nimemuona mara ya kwanza akakimbia, nikamuona mara ya pili akakimbia na mara zote aliponiona alijihami kwa kukimbia ni anakimbia vibaya mno, huwezi hata kumkimbiza kwa miguu mpaka nikawa najisemea huyu kwa hii kasi angekua anadhuru humu angekua ameshatudhuru wote humu ndani. Watu ambao hawajamuona wananiuliza ni nyoka gani Cobra mimi sijui kuhusu nyoka ila nimeona tu ana kichwa kidogo eneo la kati ni mnene kisha ana mkia mdogo. Nimejaribu hadi ku-Google simuoni nyoka km yule niliemuona.

Nawasilisha wakuu. Nasubiri maelezo yenu hapo chini.

Nime-Google ni km huyu hapa aisee sema huyu naona km hana kichwa kidogo
Screenshot_20250821_054259.jpg
 
download.jpeg

@zerominus10 nadhani unamuelezea huyu
 
Kabla ya kumkimbiza nyoka yoyote ni vizuri tujue unamkimbiza nyoka gani. Kuna wengine kuwakimbiza ni kukikimbilia Kifo chako hata kama anakukimbia.

HIki ndicho nilipewa tahadhari kuhusu nyoka
 
View attachment 3447688

@zerominus10 nadhani unamuelezea huyu
Hapana sio huyo ni km huyu hapa
Screenshot_20250821_054513.jpg

Huyo nyoka ni anakimbia hatari aisee akishapata sehemu ya kujificha ndio anakua ameyeyuka humuoni tena
 
Kwenye mambo ya kiasili labda ni mizimu ya kwenu kwanini unamuona ww peke yako?
USHAURI WANGU
Jaribu kuongea na wazee wa kwenu huenda kuna mambo wanayafahamu
 
Wakuu, kwamba naomba msinichoke hapa kuna kitu kinaniumiza kichwa sana sielewi. Hapa majuzi katika pitapita zangu za hapa na pale humu nyumbani ndani nimepishana na nyoka ana kichwa kidogo sana ila katikati ni mnene balaa na ana mkia mdogo. Kwanza najua wapo wadau watasema leta picha, sikia wakuu nyoka huyu ni moja ya nyoka wanaokimbia sio kawaida.

Nilipomuona nikajaribu kumfuata ili nimtulize hata kwa fimbo na mawe ili asilete madhara au vinginevyo ila alikimbia vibaya sana ni moja kati ya nyoka niliowashuhudia wakikimbia kwa kasi ya ajabu hatimae alitoweka ghafla sikumuona tena. Lakini huyu nyoka yupo humu humu tunamoishi hajawahi kumdhuru mtu nadhani anaogopa watu ila ninahofia siku mtu akikosea bahati mbaya mguu hauna macho na nyoka katoka kwenye harakati zake bahati mbaya akamkanyaga itakuaje?

Humu najua wapo wadau wanajua mambo mengi ya wanyama km hawa, hivi kwa nyoka km huyu ambae anazunguka tu eneo hili hili hamdhuru mtu ila anazunguka tu, tunafanyaje ili aondoke? Utauliza kwanini usimtafute? Anajificha na hakuna mtu mwingine amemuona zaidi yangu. Nimemuona mara ya kwanza akakimbia, nikamuona mara ya pili akakimbia na mara zote aliponiona alijihami kwa kukimbia ni anakimbia vibaya mno, huwezi hata kumkimbiza kwa miguu mpaka nikawa najisemea huyu kwa hii kasi angekua anadhuru humu angekua ameshatudhuru wote humu ndani. Watu ambao hawajamuona wananiuliza ni nyoka gani Cobra mimi sijui kuhusu nyoka ila nimeona tu ana kichwa kidogo eneo la kati ni mnene kisha ana mkia mdogo. Nimejaribu hadi ku-Google simuoni nyoka km yule niliemuona.

Nawasilisha wakuu. Nasubiri maelezo yenu hapo chini.

Nime-Google ni km huyu hapa aisee sema huyu naona km hana kichwa kidogo
View attachment 3447689Jamii ya mamba.
 
Humu najua wapo wadau wanajua mambo mengi ya wanyama km hawa, hivi kwa nyoka km huyu ambae anazunguka tu eneo hili hili hamdhuru mtu ila anazunguka tu, tunafanyaje ili aondoke? Utauliza kwanini usimtafute?

Huenda ana watoto hapo au kuna upatikanaji wa misosi maeneo hayo...

Fanyeni usafi mkubwa, mwaga mafuta ya taa au oil chafu maeneo fiche yote...
 
Back
Top Bottom