Nyongeza ya mshahara Tsh 10,000 nayo inatozwa kodi ukiitoa benki au ATM

Nyongeza ya mshahara Tsh 10,000 nayo inatozwa kodi ukiitoa benki au ATM

shinyangakwetu

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2015
Posts
2,487
Reaction score
2,394
Wandugu,

Wakati serikaki ikiongeza mshahara kwa shilingi 10,000.00 serikali hyo mshahara ukifika benk baada ya kulipa kodi ya PAYE, huko benki serikali inatoza kodi tena.

Huu ni uonevu ulopitiliza, ni unyonyaji kwa wafanyakazi na ushamba kwa viongozi walobuni hiyo tozo bila kutafakari.

Mtu unaweza kuwa na Phd ila usiwe na akili TIMILIFU yenye ubingwa katika kufanya kwa busara.

Tuipinge kodi hyo kila kona na ikiwezekana mshahara ukiingia toa zote ukaweke vikoba
 
Hivi Mwigilu amesomea mambo ya fedha kweli?! Now mpaka ukituma pesa benki inakatwa,ukitoa inakatwa.

Tuna serikali isiyojua wajibu wake katika kujenga uchumi,yaani wanafikiri kuongeza kodi tuuu,Ila awaangalii kupunguzq matumizi Yao ya anasa na safari za kipuuzi.
Inakera mnoo
 
Wewe bado unatunza fedha zako bank? Kalakabaho!!
 
Kwa hali hii ni upuuzi wa mtu mmoja mwenye phd za majalalani
I wish Mheshimiwa Phillipo Mpango angeendelea kuhudumu kwenye Wizara ya Fedha! Alikuwa ni mbunifu sana kwenye kodi. Na kodi zake nyingi zilikuwa hazina athari ya moja kwa moja wananchi wa kawaida.

Ila huyu jamaa wa sasa! Kiukweli ni janga. Amejawa tu ujivuni na dharau.
 
Wandugu,

Wakati serikaki ikiongeza mshahara kwa shilingi 10,000.00 serikali hyo mshahara ukifika benk baada ya kulipa kodi ya payee, huko benki serikali inatoza kodi tena...
MLIICHAGUA CCM KWA KISHINDO HAYO NDIO MALIPO YAKE
 
Wandugu,

Wakati serikaki ikiongeza mshahara kwa shilingi 10,000.00 serikali hyo mshahara ukifika benk baada ya kulipa kodi ya payee, huko benki serikali inatoza kodi tena...
Wanakuongeza 8,000/- halafu wanakata 9,000/- kwa wewe kuitoa hela hiyo toka benki.. Ni sawa na kukupunguzia 1000/- toka kwenye mshahara
 
Hivi Mwigilu amesomea mambo ya fedha kweli?! Now mpaka ukituma pesa benki inakatwa,ukitoa inakatwa...
Labda sijakuelewa,, yaan nikienda kwa nmb wakala nikaweka pesa yangu bank inamaana hapo pia wanakata
 
Wakati Rais anatangaza Jambo letu WATUMISHI wa Umma waliruka ruka kwa Shangwe huku Wakisikika wakisema MAMA ANAUPIGA MWINGI,

Mshahara ilipoingia BENKI Nyongeza walioongezewa ni Sh.10,000/= na Ukitaka kuitoa BENKI au kwenye ATM kuna TOZO JIPYA la SERIKALI limewekwa lazima liikate hiyo NYONGEZA hakika huu ni Unyonyaji wa Kiwango cha Juu na ni kweli MAMA anaupiga Mwingi.

Watumishi TUJIPONGEZE kwa kuweka CCM Madarakani.
 
Anza kuipinga ccm kwanza miTOZO ya ovyo ovyo ni matokeo ya ccm
 
Back
Top Bottom