Maulaga59
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 2,984
- 2,971
Wandugu,
Wakati serikaki ikiongeza mshahara kwa shilingi 10,000.00 serikali hyo mshahara ukifika benk baada ya kulipa kodi ya PAYE, huko benki serikali inatoza kodi tena.
Huu ni uonevu ulopitiliza, ni unyonyaji kwa wafanyakazi na ushamba kwa viongozi walobuni hiyo tozo bila kutafakari.
Mtu unaweza kuwa na Phd ila usiwe na akili TIMILIFU yenye ubingwa katika kufanya kwa busara.
Tuipinge kodi hyo kila kona na ikiwezekana mshahara ukiingia toa zote ukaweke vikoba
Lete habari nyingine, mambo ya mishahara tulishafunga last month, hatujadili tena hadi mwaka mwingine wa fedha. Afterall hata ukipewa hiyo elfu 10 nzima nzima itakuwa imetatua nini kwenye maisha yako ya kila siku. Fuga kuku, sungura , bata nakadhika ili vi-boost kipato chako. Mshahara ni kichocheo tu cha wewe kufanya mambo makubwa! Kuna watu huku mitaani hata laki moja kwa mwezi hajawahi kuiona lakini wanadunda mitaani! Funguka, tafuta njia ya kupandisha hicho kidogo ulichonacho! Usitulilie hapa, wengine hatuna hiyo mishahara!