Walianza kukata siku nyingi mfano NMB Walikuwa hawajaweka officialy. Ila ilikuwa ukitoa kiasi fulani makato ni tofauti na hapo kabla.
Inakera sana. Yaani mshahara unakatwa kodi, na bado unakatwa tozo ya kutoa na makato mengine kama service charge nk.
Hivi kama serikali ina hali mbaya,si wauze v8 zao na kupunguza ziara na misafara mingi ya viongozi?
Yaani wanaona njia rahisi ni kukomaa na wananchi. Wao ziara za kila mara ambazo kiuhalisia nyingi hazina tija.
Kuweka mawe ya msingi hata mkuu wa mkoa anaweka kwa niaba.
Aisee, inaumiza sana tena sana!