Nyongeza ya mshahara Tsh 10,000 nayo inatozwa kodi ukiitoa benki au ATM

Nyongeza ya mshahara Tsh 10,000 nayo inatozwa kodi ukiitoa benki au ATM

Wandugu,

Wakati serikaki ikiongeza mshahara kwa shilingi 10,000.00 serikali hyo mshahara ukifika benk baada ya kulipa kodi ya payee, huko benki serikali inatoza kodi tena.

Huu ni uonevu ulopitiliza, ni unyonyaji kwa wafanyakazi na ushamba kwa viongozi walobuni hiyo tozo bila kutafakari.
Mtu unaweza kuwa na Phd ila usiwe na akili TIMILIFU yenye ubingwa katika kufanya kwa busara.

Tuipinge kodi hyo kila kona na ikiwezekana mshahara ukiingia toa zote ukaweke vikoba
Mwigulu Mchemba huyo !!! Laana ya Mungu imshukie yeye na familia yake kafanya hivyo ili apate kuiba akafadhili timu yake ya mpira
 
I wish Mheshimiwa Phillipo Mpango angeendelea kuhudumu kwenye Wizara ya Fedha! Alikuwa ni mbunifu sana kwenye kodi. Na kodi zake nyingi zilikuwa hazina athari ya moja kwa moja wananchi wa kawaida.

Ila huyu jamaa wa sasa! Kiukweli ni janga. Amejawa tu ujivuni na dharau.
Ndio haohao wezi wenyewe CCM ni wezi Hali ngumu kama hizi kweli leo hii tunakuja kuumizana kiasi hicho
 
I wish Mheshimiwa Phillipo Mpango angeendelea kuhudumu kwenye Wizara ya Fedha! Alikuwa ni mbunifu sana kwenye kodi. Na kodi zake nyingi zilikuwa hazina athari ya moja kwa moja wananchi wa kawaida.

Ila huyu jamaa wa sasa! Kiukweli ni janga. Amejawa tu ujivuni na dharau.
Sasa yeye si makamu wa rais kama akishindwa akiwa hapo hawezi hata ukimrudisha

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Halafu tozo zina accumulate, siku wakiamua wanakwangua akiba yako.......huyo ndo madelu mchumi daraja la kwanza.
 
Wabongo acheni kulalamika fanyeni kaZi mimi niko uku cambodia maisha yako juu acha mchezo uku hata kudeposit fedha bank kuna makato , gb moja ni sawa Na elfu kumi za kibongo halafu hali ya mtaani ni mbaya mnoo yani watu tunashindia ugali Na uji acheni kulalamika

Mbona wewe ndio unalalalmika Sasa. Kama wewe kuishi Maisha magumu Cambodia unaona sawa usilazimishe wengine huku Tanzania. Wewe ridhika huko Cambodia achana na sisi Tanzania tulalamike.
 
Maandiko yanatimia sasa,yaani hata kile kidogo unacho dhani unacho kitachukuliwa,ni maandiko hayo ,,in nabii tito voice.
 
Halafu tozo zina accumulate, siku wakiamua wanakwangua akiba yako.......huyo ndo madelu mchumi daraja la kwanza.
Halafu yeye anajinunulia Shangingi la LC300 ambalo hata waziri mkuu wa Japani hatembelei.
Msafara mmoja yanakuwepo hayo madude kama mia hivi!!! Hii nchi sio maskini ila imejaa wabadhirifu.
 
2025 Kuna jipya gani? nani kakwambia ccm inategemea Sanduku la kura! umemsikia aliesema Kenya ije kujifunza kwetu mbinu za uchaguzi
Hizo mbinu za kipumbavu tunazojivunia alikuwa anazifanya Moi na KANU miaka ya 90.. Wakenya walishavuka kwenye huo ujinga wa kuibiana kura kitoto na kimabavu.

Sisi bado tuko usingizini, tunaibiwa na kuteswa lakini hakuna yeyote anayeweza kufanya au kuzuia kinachoamuliwa.

Kenya upumbavu kama huu tunaofanyiwa tayari Mawakili na Law Society yao ingeshaenda High Court kuzuia huo ujinga.

Sisi mawakili wetu na chama chao wako kimya tu kama hakuna manung'uniko huko mitaani.
 
Hivi Mwigilu amesomea mambo ya fedha kweli?! Now mpaka ukituma pesa benki inakatwa,ukitoa inakatwa.

Tuna serikali isiyojua wajibu wake katika kujenga uchumi,yaani wanafikiri kuongeza kodi tuuu,Ila awaangalii kupunguzq matumizi Yao ya anasa na safari za kipuuzi.
Inakera mnoo
Labda PhD ya betting !!
 
Back
Top Bottom