Nyongeza ya mshahara Tsh 10,000 nayo inatozwa kodi ukiitoa benki au ATM

Nyongeza ya mshahara Tsh 10,000 nayo inatozwa kodi ukiitoa benki au ATM

Hizo mbinu za kipumbavu tunazojivunia alikuwa anazifanya Moi na KANU miaka ya 90.. Wakenya walishavuka kwenye huo ujinga wa kuibiana kura kitoto na kimabavu.

Sisi bado tuko usingizini, tunaibiwa na kuteswa lakini hakuna yeyote anayeweza kufanya au kuzuia kinachoamuliwa.

Kenya upumbavu kama huu tunaofanyiwa tayari Mawakili na Law Society yao ingeshaenda High Court kuzuia huo ujinga.

Sisi mawakili wetu na chama chao wako kimya tu kama hakuna manung'uniko huko mitaani.

Wakenya hawajavuka popote ndugu yangu. Africa usanii upo damuni.
 
Binadamu ndiye kiumbe pekee anayelipia kuishi kwenye sayari yake....
 
Lipa tozo wewe acha kupenda buree.
Lipa tozo kwa maendeleo yako na wajukuu zako
 
Pongezi kwa Mwigulu kwa kazi nzuri.
Hakika nchi haiwezi kusonga mbele bila kulipa kodi/tozo lazima tulipe tozo.
 
Lete habari nyingine, mambo ya mishahara tulishafunga last month, hatujadili tena hadi mwaka mwingine wa fedha. Afterall hata ukipewa hiyo elfu 10 nzima nzima itakuwa imetatua nini kwenye maisha yako ya kila siku. Fuga kuku, sungura , bata nakadhika ili vi-boost kipato chako. Mshahara ni kichocheo tu cha wewe kufanya mambo makubwa! Kuna watu huku mitaani hata laki moja kwa mwezi hajawahi kuiona lakini wanadunda mitaani! Funguka, tafuta njia ya kupandisha hicho kidogo ulichonacho! Usitulilie hapa, wengine hatuna hiyo mishahara!
👏🏾🔊
 
Back
Top Bottom