Pamoja na kwamba nimesoma mtandaoni lakini pia mimi nilisoma Biology o- level, ninafahamu kazi ya nyongo kwa ujumla wake na hakuna utofauti kati ya mnyama na mnyama, yaani nyongo ya kuku, mbuzi, ng'ombe, chui, simba, mtu, nyani nk, kazi yake ni moja tu nayo ni kusaga au kuyeyesha mafuta yanayoingia tumboni kwa njia ya chakula, nyongo inazalishwa na Ini na kuhifadhiwa kwenye kifuko kinachoitwa "gall bladder" ambacho kimeungana na ini, chakula kinapoingia katika utumbo mdogo ndipo gall blader humimina hiyo nyongo ili ikasage mafuta yaliyoambatana na chakula na mafuta yakisagwa ndipo hufyonzwa na vifyonzeo (olveollis kama sijasahau) ambavyo vimeungana na mishipa ya damu na hivyo mafuta yaliyoisha sagwa pamoja na chakula kilichosagwa ndani ya utumbo mdogo husafirishwa na damu katika sehemu mbalimbali za mwili, sasa kwa akili ya kawaida haiwezekani sumu itumike katika usagaji wa chakula tena itumike sehemu ambayo chakula kilichoyuyuka huwa kinafyonzwa kuingia kwenye damu ili kisambae mwili mzima ndiyo maana nikasema hata nyama ya mamba ingekuwa ni sumu pia na hata kinyesi cha mamba kingekuwa ni sumu pia kwasababu baada ya usagaji wa chakula mabaki ndiyo huwa ni kinyesi na kwa namna hiyo viboko wengi wangekufa kwasababu maisha ya viboko na mamba huwa ya ujirani kwa kiasi fulani na hata samaki na viumbe wengine wa majini wangekufa pia.
Hadithi ya Nyongo ya Mamba kuwa Sumu ipo huku kwetu sana, Afrika ya kati, mashariki na kusini lakini huwezi kusikia hadithi hizi huko Asia ambapo pia wapo mamba, huwezi kusikia hadithi hizi huko Canada na USA ambapo pia kuna mamba wakubwa kama hawa wetu wajulikanao kama Alligators, huko Brazili na maeneo ya mto Amazon kuna mamba wengi sana Wanaitwa Caiman crocodile, huko huwezi sikia kwamba nyongo ya mamba hao ni sumu na hao mamba wanakula vyakula vilevile wanavyokula mamba wetu (Nile crocs).
Ni hivi; Kuna baadhi ya mimea ni sumu sana na inakuwa ni sumu kali sana pale inapochanganywa na nyongo, nyongo yoyote ya mnyama yeyote na mamba anayo nyongo nyingi na anaweza kupatikana kirahisi ndipo Waganga wa kienyeji huchukua hiyo nyongo na kuchanganya na hiyo miti-sumu kupata matokeo bora zaidi ya hizo sumu.
Na watu wanasema ukichukua kiasi kidogo tu ndani ya ukucha na kumuwekea mtu ndani ya glasi ya maji au pombe basi huyo mtu ni baibai!!, ni uwezo wa nyongo ya mamba kusaidia kuipa nguvu miti-sumu hiyo.
Kifupi ni kwamba Nyongo ya Mamba kama ilivyo (per se) siyo sumu bali ni kiungo kizuri sana cha kufanya miti-sumu (toxic herbs) ziwe na nguvu kubwa sana ya kuua. Na hii ni lazima iwe ni miti-sumu na siyo synthetic toxin sumu za kutengeneza viwandani.
Na imani hii utaikuta kwa waganga wa kienyeji wanaotengeneza sumu za miti shamba wakichanganya na nyongo ya mamba na hivyo kuwadanganya watu kwa kujua au kutokujua kwamba Nyongo ya Mamba yenyewe kama yenyewe ni Sumu.