Nyongo ya mamba ni sumu kali inayouwa kwa haraka zaidi

Acha kubisha usicho kijua Mzee baba,hii ni uhalisia kabisa inatokea kila siku maeneo husika fika siku moja use shuhuda kwa wabishi wenzako.
 
Ushawahi itumia?au unafuata upepo unapovuma?
 
Acha kubisha usicho kijua Mzee baba,hii ni uhalisia kabisa inatokea kila siku maeneo husika fika siku moja use shuhuda kwa wabishi wenzako.
Naongelea utafiti wa kisayansi na si ubishi au uzushi potofu unaoeneze wewe. Naongelea wataalam waliofanya research kwa kuwalisha panya na nyani nyongo ya mamba na haikuwa na matokeo yoyote mabaya. Naongelea scientific facts na siyo mapokeo ya simulizi za mababu kama unavyofanya wewe! Naongelea mambo yaliyofanywa maabara na siyo bla blah za mtaani kama wewe!
 
Ushawahi itumia?au unafuata upepo unapovuma?


Na wewe nikuulize swali hilohilo, je umeshaonja nyongo ya mamba kuthibitisha kwamba ni sumu??.

Matumizi ya Nyongo ya mamba kama kiungo (additive) katika miti-sumu ili kufanya sumu hizo ziwe kali na kuua kwa haraka ni Elimu au sayansi inayopatikana katika maeneo yetu ya Afrika mashariki na kati, kusini na magharibi, ni elimu inayotumiwa hasa na Waganga na wachawi katika kutengeneza hizo sumu ili kudhuru watu. Ni elimu inayohusikana na mambo ya kichawi.
 
Nishashudia watu wameathirika kwa kutumia ikichanganywa na dawa za kienyeji au kichawi.
 
Nahitaji hii sumu naipataje? Mwenye kujua jinsi naweza kuipata naomba msaada?
 
Sisi ambao sio wa wabishi na ambao tunapenda kujifunza tunashukuru kwa taarifa.
 
Tunaenda kuwashika ziwani au mto ruaha ile nyongo tunatoa ile sumu kwa ajili ya mishale yetu ya kuwindia tunachanganya namiti pori fulani mizizi yake basi hata tembo ukimpiga mshale ule au nyati mita 5 tu mbele hapo hapo ganzi anadondoka
Kumbe wewe ni Jangili
 
Nyongo ya Mamba ni sumu kali mno

Hata ikitokea mamba amekufa mtoni, serikali ikifahamu inaweza kuwazuia watumiaji wa maji ya mto huo wasitumie maji kwa siku nzima

Watu wa Maliasili na wanajeshi huwa wanachinja mamba wakubwa waliozeeka na kuchukua nyongo na magamba TU, nyama wanaweza kuwaachia wananchi mle mpaka muache.

Kwa aliyekula nyama au mafuta ya mamba anajua ni jinsi gani inavyoleta KIU, unaweza kunywa maji Lita 5 kwa siku na bado kiu isiishe.

Babu yangu alikuwa na mkuki na nyongo ya mamba kidogo kwenye kikopo cha Kiwi, lakini alikuwa anaficha darini.
 
Kweli, hayo maeneo hakuna Mambo hayo. Hata mtoa maada anasema, eti Kigoma mjini, mwanga, Ujiji? Mzushi tu. Huku Kuna ustaarabu bwana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…