Nyongo ya Mamba siyo sumu, ni uzushi na uongo uliozoeleka miongoni mwa jamii za kishirikina, sio kweli hata kidogo kwamba Nyongo iwe sumu.
Sasa wewe niambie kazi ya hiyo nyongo ya mamba mwilini mwa mamba ni ipi???
Nyongo ipo kwa binadamu, kwa kuku, mbuzi nk, kazi yake ni kumeng'enya mafuta ndani ya utumbo mwembamba, ndani ya utumbo mwemba ndimo usagaji wa chakula hufanyika.
Mamba hula vyakula vyenye protein na mafuta hivyo nyongo inamsaidia kuyeyusha mafuta yatokanayo na vyakula anavyokula.
Nyongo (bile) ni digestive juice.
Watu wengi wenye imani kwamba nyongo ya mamba ni sumu hao utakuta wamekulia katika imani za kishirikina na uchawi.
Kama nyongo hiyo ingekuwa ni sumu mbona yeye mwenyewe mamba si angekufa kabla ya kuua watu wengine au hata nyama yake isingekuwa inaliwa au hata kinyesi chake kingekuwa ni hatari na sumu kubwa.
Tumieni akili kuliko kupinga kijinga kwa kufuata mkumbo tu.
Angalia ndani ya Google uone watu waliofanya hizo tafiti.
Crocodile bile lethal poison??