Nyufa ni kubwa sana hata mfiche vipi, CCM matatani

Nyufa ni kubwa sana hata mfiche vipi, CCM matatani

Foffana

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2022
Posts
3,240
Reaction score
5,625
Anaandika Kigogo

NYUFA NI KUBWA SANA HATA MFICHE VIPI ,BASHE AMEITIA CCM MATATANI

Kitendo cha kuahirishwa vikao vya juu kabisa vya CCM kwenye kufanya uteuzi wa wagombea wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025 ni jambo zito na gumu sana kuwahi kutokea kwenye uhai wa CCM.

Sababu za kitoto anazotoa Amos Makalla ni kwa ajili ya watu wajinga ambao hawana uelewa wa mambo haya na hawataki kujishughulisha na mambo ya nchi hii ndiyo wanaweza kuamini sababu zake za kijingajinga alizozitoa.

Sababu hizi ni nyepesi na naziita za kitoto kwa kuwa huwezi kutaka kuaminisha watu wenye akili timamu kabisa waelewe na kukubali kuwa eti wagombea wengi sana ndiyo maana kazi ya kupitisha majina iliyokuwa ifanywe na kamati kuu imeahirishwa.

Sawa tuchukulie kuwa ni kweli wagombea ni wengi sana na mlishindwa kumaliza kuwachambua. Sasa kulikuwa na haja gani kuacha wajumbe wafike Dodoma na kazi ya kuchambua hamjamaliza? Kulikuwa kuna haya gani kuacha wajumbe wafike mpaka ukumbini na Mwenyekiti kulazimika kuahirisha kikao wakati kulikuwa hakujakamilika kwa kazi ya kuchambua majina?

Amos Makalla anajitahidi sana kuficha nyufa zilizosababishwa na Bashe na wanamtandao wenzake ambao wamefanikiwa kujenga mtandao uleule kama waliojenga wakati wa Lowassa na kukaribia kabisa kuipasua CCM. Awamu hii wamefanikiwa vilevile na wamejenga mtandao mpana sana ndiyo maana Bashe alikuwa anaweza kupigia simu makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa na kuwapa maelekezo nani apite nai asipite !

Maeneo yote nchi nzima Bashe na wana mtatandao wenzake wamepandikiza watu wao na shida imekuja baada ya kugundulika kuwa majina yaliyotoka wilayani na mikoani kwa maksi siyo yaliyopelekwa kwenye vikao vya juu kwa ajili ya maamuzi ya mwisho. Kwa kifupi majiba yamechakachuliwa vibaya sana!

Walianza toka wakati wa uchukuaji fomu ,watu waliokuwa hawawataki waliwatishia kwa kutumia vyombo vya usalama wasigombee kwa kusingizia ni maagizo ya wakubwa ,waliposhindwa hapo Bashe alipigia simu makatibu wa wilaya na mikoa na kuwapa maelekezo kuwa yametoka juu na waliposhindwa huko sasa wamechakachua majina na ndiyo sasa imeleta shida kubwa kiasi hiki.

Haijaleta shida Tanganyika tu bali kote mpaka Zanzibar imeleta shida kubwa sana kwa sababu Bashe bado anaota kuwa wanapaswa kujenga kuweka mtandao na Zanzibar ili mgombea wao wa 2020 bwana Masauni awe Rais ifikapo 2030😁

CCM isingejikuta kwenye mikingamo hii mikubwa kuwahi kutokea kama ingalikuwa makini na kusikiliza maonyo yaliyokuwa yanatolewa kuhusu Bashe na watu wake. Alianza haya mambo zamani sana na tulikuwa tunasema anagawia watu hela bungeni kwa ajili ya kufanya mambo haya watu hawakuwa wanasiakia. Tulisema anapigia simu makatibu wa CCM huko mikoani na wilayani na kusema katumwa na mwenyekiti na katibu mkuu bado watu walikuwa hawataki kusikia sasa yamewakuta mambo ya aibu kubwa sana.

CCM haijajifunza shida iliyoletwa na wanamtandao miaka ile ya 1995 na madahara yake yalikwenda na kukiharibu chama mpaka 2015 .. Madhara makubwa yaliyoipata CCM kwenye mbio za urais mwaka 2015 ilikuwa ni madhara ya kuwa na mtandao ndani ya CCM. Mtandano ni kansa na kitu kibaya sana kuachwa kukue ndani ya nchi au serikali au chama cha siasa. Ni kikundi cha watu wenye ulafi wa kutaka kushika madaraka na wanatumia kila aina ya mbinu kuhakikisha wanaingia madarakani na madhara yake wote mnayajua na shida ambayo Tanzania iliingia kama matokeo ya mtandao na watu wake.

Bashe na kikundi chake wametumia fomula ile ile ya wakati wa Lowassa na wamei apply na imefanyakazi vizuri sana ndiyo maana wameweza kuweka wagombea wao wa ubunge na udiwani karibia 95% nchi nzima. Hili kitu wanalolijenga sana ni jinamizi na litakuja kuipasua hii nchi vipande vipande kwa kuwa tunapokuwa tunasema haya mambo watu wanakuwa hawataki kusikia

Leo mchakato umevurugika Dodoma kwa kuwa Bashe na kundi lake wameharibu uchaguzi ndani ya chama na ndani ya CCM.

NI AIBU KUBWA SANA KUTOKEA NA NYUFA NI KUBWA SANA HATUWEZI KUZIZIBA KWA MAELEZO YA MAKALLA

CCM IKO NJIA PANDA NA IMEKWAMA SANA
 
Kwamba swala la kizimkazi kususa kununa na kwenda kupunga upepo HOME halihusiani na kuahirisha kikao?

Kumbe ni Bashe? Huyu Bashe ana nguvu kasi gani? Amezitoa wapi? Ni nani kwenye siasa za tz?
 
Kwamba swala la kizimkazi kususa kununa na kwenda kupunga upepo HOME halihusiani na kuahirisha kikao?

Kumbe ni Bashe? Huyu Bashe ana nguvu kasi gani? Amezitoa wapi? Ni nani kwenye siasa za tz?
Yaan ukisoma andiko la mtoa mada hupati chochote cha maana, unapata maswali kama yako. Ukute ni watu wanachafuana tu.
 
"Bila CCM imara Nchi itayumba" MWALIMU NYERERE"

Vikao vimeahirishwa kutokana na "kasoro za kiufundi". Ni budi zishihulikiwe Ili mchakato salama uendelee. Vyama vyoote vinaweza kuvurunda na Nchi ukabaki salama, ila sio CCM.
 
Back
Top Bottom