Yaani ninachosema ni hakuna general fomula ya haya mambo. Kuna mwanamke anadeserve asitoke hata na mia sababu ni muhuni tu amejiingiza hapo kuvuna. Tangu mwanzo alipanga avune kupitia viungo vyake na mayai yake. Na hawa huwa hawadumu zaidi ya 5 years, mara nyingi ni below that.
Ila kuna mwanamke kama usemavyo, amekaa na mwanaume tangu ana miaka 20 leo ana miaka 39, amekufulia, amekuzalia, amekulelea wanao, amekupikia halafu amekufumania unamjibu hovyo na unaanza visa mara leo hili kesho lile, anaamua imetosha muachane sasa halafu aondoke kama alivyokuja?
Alikuja akiwa na chuchu saa sita, alikuja pengine bikra, alikuja hana stress, alikuja akiwa na afya pengine umempa magonjwa, anastahili fadhila, anastahili haki. Sheria lazima zimlinde.
NDO MAANA NASEMA HAKUNA GENERAL WAY YA HAYA MAMBO, INATEGEMEANA NA MAZINGIRA HALISI.