NYUMA YA PAZIA: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015 - Dkt. Slaa


Nimependa ulichoongea kwani una uwezo mkubwa wa kujieleza na una mtiririko mzuri wa uandishi. Kwa hiki ulichoongea ni dhahiri ww ulikuwa mmoja ya watu mlioshiriki mchakato wa kumpatia Lowassa nafasi adhimu ya kugombea urais kupitia cdm.

Kwa mtazamo wangu kama kuna kosa kubwa mlifanya viongozi wa cdm, ni kumpa Lowassa nafasi ya kugombea urais. Pangeni sifa vyovyote mtakavyo lakini uamuzi ule ni wa kihuni kama uhuni mwingine, Lowassa alikuwa hafanyi siasa wala hawezi siasa bali alikuwa anafanyiwa na wapambe kutokana na hela yake. Ww kama ww ni lini uliwahi kumuona Lowassa akiongea kwenye jukwaa la siasa zaidi ya nusu saa, zaidi ya wapambe kumsifia? Ni nani ambaye hakujua watu walijiandikisha kwa hasira maana walijua Lowassa ndio chaguo la ccm, na kitambulisho cha kura kiliitwa kichinjio kwa ajili ya kumchinjia Lowassa iwapo angekuwa mgombea wa ccm?

Magufuli alipewa nafasi na ccm sio kwakuwa alikuwa anakubalika na wanaccm, bali ndio pekee aliyekuwa amebaki wangalau angekuwa na nguvu ya kupambana na Dr. Slaa, na hii ni kutokana na rekodi yake ya utendaji hasa kwenye miundombinu. Iwapo sio hofu ya Dr. Slaa, Leo hii Membe ndio angekuwa rais kupitia ccm iwapo ingeshinda na wala asingekuwa Magufuli. Msituone hatujui lolote, kama kuna sifa kubwa alikuwa nayo na ndio hasa ilimpa nafasi ni pesa yake na sio zaidi ya hapo. Slaa kama Slaa kilichomfanya aondoke cdm, ni kuzira na shinikizo la mkewe kwa kukosa nafasi ya kugombea urais ambayo walikuwa wamejiandaa nayo. Ila sababu ya kuwa aliondoka kwakuwa Lowassa sio msafi ilikuwa ni kisingizio tu, japo katika mazingira yale sababu hiyo inambeba, lakini ukweli ni kuwa alizira baada ya yeye kukosa nafasi ile.

Halafu napenda muelewe wala msitake kupotosha, cdm ilivyokuwa iko kwenye damu za wananchi hiyo 2015, ingepata kura nyingi sana iwapo Dr. Slaa angekuwa mgombea, na hata kama asingekuwa rais kutokana na mfumo wa uchaguzi ulivyo, bado cdm ingebaki na haiba yake, kuliko ilivyokuwa baada ya Lowassa kuingia.
 
Umewasilisha mawazo yangu kwa asilimia tisini...

Heshimu yako mkuu.
 
Dkt. Slaa alihamia lini na Wapi CCM? Nina uhakika wa asilimia mia moja hutarudi na jibu la tarehe wala mahali.

Ni kweli hayuko ccm, lakini unapokuwa balozi kwa uteuzi wa mwenyekiti wa ccm, hasa mwenyekiti mwenyewe akiwa ni Magufuli, automatically ww ni mwanaccm. Kama Magufuli alipokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huku jeshi likiwa limetengwa na siasa kikatiba itakuwa ubalozi wa Slaa? Jaribu kuangalia alichoongea juzi Dr. Slaa alipokuja kwenye mkutano wa SADC, ni wapi Slaa aliongelea demokrasia? Je aliposema kwamba yote wapinzani waliyopigia kelele yamefanyiwa kazi na Magufuli, ni nani asiyejua kilio namba moja cha Slaa na wapinzani ilikuwa katiba mpya?Je katiba mpya imepatikana? Kama Slaa aliongoza maandamano zaidi ya mara moja enzi JK kuwa haheshimu demokrasia, je hivi sasa demokrasia iko kwenye hali gani? Kama Slaa hakuwahi kuamini kwamba hamna ushindi wa ccm bila wizi wa kura enzi za JK, je sasa hivi box la kura linapobakwa kiwaziwazi, ndio Magufuli alipofanyia kazi hicho kilio cha wapinzani?

Namuheshimu Dr.Slaa, na natambua mchango wake kwenye siasa za nchi hii, lakini siwezi kutoa 20,000 yangu kwenda kununua kitabu cha mtu mwenye unafiki wa wazi. Mkitaka kigaweni bure ili watu wakisome
 
Pascal.. kama mtu kauoa na asimfanye mkewe kuwa kila kitu hiyo siyo ndoa tena. Unamnyoshea kidole Dkt. Slaa kwa vile kampa kipaumbele mkewe na watoto wake? Mwanamme usipompa nafasi ya kwanza mkeo.. unampa nani?
Mzee mwenzangu , inategemea ''situation''
Nafasi ya kwanza haina maana unayosema. Kuna nyakati unampa mkeo nafasi ya pili kwasababu ''mkeo ni kila kitu'', kwa kufanya hivyo ndivyo ''ndoa inapokuwepo''
 
Mimi hata bure hicho kijitabu sichukui, anayaka ajisafishe ajifanye kuwa hakufanya mistake 2015??
 
Safi sana mkuu!
 
Hiki kitabu hakifai hata kuwa "toilet paper" ya vichaa majalalani! Doctoral rubbish...
 
Anataarifa kuwa Yule aliemkimbia sasa amerudi nyumbani?😁😁😁
 
Haya uliyoyasema ndio ukweli Wenyewe, sijui shetani gani alimpitia huyu Dr Slaa, alipambana miaka mingi kuleta mabadiliko yenye tija ktk nchi hii lakini alishindwa maamuzi ya muda mfupi tu 2015 na kupotexa mwelekeo mazima.
Chama ndo kilipoteza mwelekeo hadi sasa hakijulikani kinasimamia nini.
 
Dr. Slaa ni mtu mzuri aliyeshaushiwa na shetani kama ilivyokuwa kwa Adamu na Hawa!
Tumsamehe tu bali kitabu chake msikisome kwani kina uwongo mwingi wa kisisiem! Tangu aingie huko anachokisema hakieleweki tena! Mwacheni babu huyo!
 
"tindo, post: 32922226, member: 55693"]
Ni kweli hayuko ccm, lakini unapokuwa balozi kwa uteuzi wa mwenyekiti wa ccm, hasa mwenyekiti mwenyewe akiwa ni Magufuli, automatically ww ni mwanaccm.
Kuna wakati aliyekuwa Jaji Mkuu aligombea Urais kupitia CCM. Nani alijua kuwa Jaji alikuwa na kadi ya CCM!!
Jaribu kuangalia alichoongea juzi Dr. Slaa alipokuja kwenye mkutano wa SADC, ni wapi Slaa aliongelea demokrasia?
Hakuna
Je aliposema kwamba yote wapinzani waliyopigia kelele yamefanyiwa kazi na Magufuli, ni nani asiyejua kilio namba moja cha Slaa na wapinzani ilikuwa katiba mpya?
Inashangaza! Kwamba katiba aliyoilalamikiwa leo anaaminisha umma'' imefanyiwa kazi ''
JKama Slaa aliongoza maandamano zaidi ya mara moja enzi JK kuwa haheshimu demokrasia, je hivi sasa demokrasia iko kwenye hali gani?
Hata kuizungumzia katika ''uzuri' aliouona hakuthubutu
Kama Slaa hakuwahi kuamini kwamba hamna ushindi wa ccm bila wizi wa kura enzi za JK, je sasa hivi box la kura linapobakwa kiwaziwazi, ndio Magufuli alipofanyia kazi hicho kilio cha wapinzani?
!
Namuheshimu Dr.Slaa, natambua mchango wake kwenye siasa za nchi hii, lakini siwezi kutoa 20,000 yangu kwenda kununua kitabu cha mtu mwenye unafiki wa wazi. Mkitaka kigaweni bure ili watu wakisome
Hili nalirudia tena, ni mmoja wa walioamsha hamasa ya wananchi kushiriki siasa na kuhoji serikali bila woga.

Niliwahi kuandika hapa JF, uamuzi wa kuachana na Chadema kwa kutokubaliana na yanayoendelea ulikuwa ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu sana na mfano kwa vijana

Kwamba, kama kuna asiyeridhika na maamuzi ni vema akaheshimu msimamo wake na kusimama na kile anachoamini. Nilimpongeza

Baada ya hapo, Dr akaungana na akina Mwaky kwenda Sheraton kuzungumzia mambo tofauti na yale yaliyosababisha akaachia ngazi, hatua mbaya na mbovu sana.

Nilimweleza, heshima aliyoijenga kwa miaka na gharama kubwa itaporomoka.
Ni vema angetulia ili historia imhukumu.

Leo maneno yale yale yanamrudi kuliko mazuri mengi aliyofanya.

Kwa bahati mbaya hakujifunza kutokana na kosa la awali.
Dr Slaa aliwahi lalamikia vinasa sauti ktk godoro kule Dodoma. Umma ulilaani kitendo hicho.

Dr Slaa yule yule anaona kupigwa risasi ni jambo la kawaida kuliko vinasa sauti alivyowekewa. Akaogopa hata kusema ' si sawa''. Akausaliti umma uliosimama naye kulaani vinasa sauti. Hapa heshima yake ilifika 'rock bottom' na kugeuka kuwa coward

Kuandika kitabu kwa rekodi sioni tatizo ikiwa kufanya hivyo kutakuwa na tija katika jamii

Kama ni kwa biashara, timing ni mbaya.Hali ya kisiasa inakifanya kionekana ''uchochezi'' !!

Pili, akiwa na magwanda ya kijani kinachoeleza magwanda ya khaki si mkakati mzuri.

Tatu, kauli zake za hivi karibuni zinazopingana na kile alichosimamia hazisaidiii mauzo.

Nne, title ya kitabu ni nyuma ya pazia(behind the scene). Kwanini isiwe ''Memoir''
Behind the scene ni tangazo la shari dhidi ya mahasimu wake. Wateja ni akina nani?

Kama ''abstract'' ni hiyo ya MM, nachelea kusema kitabu kitaongelea migogoro zaidi kuliko demokrasia aliyosimamia kwa nguvu. Tuna migogoro ya kutosha! Nahitaji kusoma kitu tofauti.
 
Nyuma ya Pazia, kumbukumbu zitabaki kuwa mahala pake. Usipisoma watoto Wako watakuja kukisoma. Tena watasoma na mchango wako hapa.
 
mkuu!
umejibu maswali yote niliyokuwa najiuliza kuhusu sakata la slaa na chadema!
kwa Maelezo hayo sina kiu ya kununua hicho kitabu!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…