Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Kuna mambo mengi mno KWENYE SIASA yanayohitaji utulivu wa kutosha kuyaelewa
Dk Slaa katika hatua za awali alikubaliana na wazo la LOWASA kujiunga na CHADEMA
Tulipomuuliza kwenye kamati kuu kwanini alikubali kujiunga kwa Lowasa kwenye chama, akatujibu kwamba Lowasa alisema atakuja na mtaji ambao kwa wakati ule Dk alisema hakuuona
Pili alisema alidhani Lowasa atakuwa mwanachama tu lakini hatakuwa mgombea urais
Tatu ,alisema Lowasa atoke hadhani kwa watanzania ajisafishe kwanza kuhusu tuhuma za ufusadi ambazo yeye(Dk slaa)ana ushahidi nazo.
Sisi tulimuita Lowasa mbele ya Dk slaa( katibu mkuu) wetu kipindi hicho na Lowasa akatolea ufafanuzi kila jambo kwa ufasa.
Katika hatua hiyo Dk Slaa akaridhika lakini baadaye hatukumuona bali tulichoona ni barua ya kumkaimisha Salum Mwalimu nafasi yake.
Maoni yangu ya ujumla ni kwamba Dk Slaa alikuwa sahihi kusimamia kile alichokiamini lakini alichoghafilika kidogo ni kuharibu kazi kubwa aliyoipigania kwa miongo miwili mizima yaani robo ya umri wake kwa kukwazwa tu kwa mara moja.
Lazima katika haya mapambano tupime baina ya masilahi mslapana ya jamii na taasisi tunazozisimamia ukilinganisha na masilahi yetu. Nadhani Dk amesimamia masilahi yake zaidi kuliko masilahi mapana ya jamii ya wapenda mageuzi makububwa ya mfumo wa kiutawala.
Kitabu cha Dk mambo mengi ameyasema kwa ukweli kufurahisha watu fulani wa makundi fulani na ndio maana nasema ni wakati wa watanzani kupima wanasisa vizuri bila kujali vyama vyao.
Dk Slaa hawezi kuwaona viongozi wa CHADEMA kama viongozi waliodalalia chama chao. Mwanzoni
kiongozi kama Mbowe,Tindu Lisu,Mnyika walikuwa hawkubaliani kabisa na swala la LOWASA kujiunga na CHADEMA lakini sisi wajumbe wa Kamati kuu ndio tuliowalazimisha baada ya kuona uwezo na nafasi ya Lowasa kukiletea chama ushindi
Hatukukjbsliana kirahisi ila tulipata nguvu ya kuwashawishi baada yakuona kwamba katika hatua za awali Dk Slaa aliunga wazo hilo mkono.
Kwahiyo Dk kushutumu vio gozi wenzake ni kujitetea kusiko na mashiko yoyote.
Lakini mwisho wa siku yote ni historia CHADEMA ipo na itaendelea kuwepo bila kujali mawimbi yanayoikumba,
tukumbuke dr Slaa anatumiwa na chama chake kipya, ccm kuiua CHADEMA.
uchaguzi mwakani atarudishwa kukitetea chama cha ccm,
Moja ya Mjumbe wa kamati kuu aliyekwenda na ujumbe wa kamati ndogo ya kamati kuu kwenda kuongea na Dk Slaa kuhusu uamuzi wake huo.
Jambo kubwa alilolalamika ni kwamba hamkubali LOWASA lakini tatizo kubwa lilokuwa dhahiri ni kwamba alishafanyiwa maandalizi yote ya kuwa mgombea Urais kwanini ghfla tu Kamati kuu inafanya mabadiko ya mgombea.
Tulimpa facts zote lakini hakutaka kutuelewa.
Katika kikao Cha kamati kuu alipewa facts zote kwanini ni muhimu kumkubali Lowasa licha ya upungufu ambao uitajwa kwa LOWASA na kwamba yeye hawezi kukipa chama ushindi au upinzani ambao ungefanana na wa LOWASA pamoja na upungufu ambao LOWASA alisemekana anao.
Kamati kuu ilimuambia Demokrasu ni kuhusu watu na watu wanasema nini kwa wakati huo.
Mwaka 2015 LOWASA alikuwa ni mwanasiasa anayekubalika kwa jamii ya makundi yote kuliko mwanasiasa yoyote kwa kipindi kile hususani kwa wagombea Urais waliokuwa wametia nia.
Tulimueleza Dk kuanza kutafakarifu udhaifu wa Lowasa ambao kwa maeneo mengine umeongezewa chumvi ilihali wananchi wanampenda hakutusaidii kupata ushindi au kutoa upinzani wa kutosha kwa mgombea wa CCM.
Na mimi binafsi nilimuambia Dk Slaa hata kama LOWASA hatashinda Urais lakini atakuwa Katibu mkuu wa Chama kikibwa sana nchini.
Naamini uwezo wa Dk Slaa ni Mkubwa sana kwahiyo angesimama kwenye nafasi ya ukatibu mkuu kipindi kile cha uchaguzi tungepata idadi kubwa ya wabunge na madiwani kuliko tuliopata sasa
Lakuni hata kura za uais huenda zingekuwa nyingi kuliko zilizopatikana kwa matangazo ya Tume ya Uchaguzi
Kwahiyo nadhani kitabu chake anataka tu kuwaaminisha wananchi kuhusu uhalali wa uamuzi wake lakini kama hakuwa na mbegu ya ubinafsi hakupaswa kufanya uamuzi ule aliofanya.
Yote yamepita ,
CHADEMA tunapaswa kusonga mbele kwani haya tunayopitia ndio kanuni za mchakato wa safari tunayotaka kwenda
Kwavyovyote vile safari lazima ifike mwisho
Nimependa ulichoongea kwani una uwezo mkubwa wa kujieleza na una mtiririko mzuri wa uandishi. Kwa hiki ulichoongea ni dhahiri ww ulikuwa mmoja ya watu mlioshiriki mchakato wa kumpatia Lowassa nafasi adhimu ya kugombea urais kupitia cdm.
Kwa mtazamo wangu kama kuna kosa kubwa mlifanya viongozi wa cdm, ni kumpa Lowassa nafasi ya kugombea urais. Pangeni sifa vyovyote mtakavyo lakini uamuzi ule ni wa kihuni kama uhuni mwingine, Lowassa alikuwa hafanyi siasa wala hawezi siasa bali alikuwa anafanyiwa na wapambe kutokana na hela yake. Ww kama ww ni lini uliwahi kumuona Lowassa akiongea kwenye jukwaa la siasa zaidi ya nusu saa, zaidi ya wapambe kumsifia? Ni nani ambaye hakujua watu walijiandikisha kwa hasira maana walijua Lowassa ndio chaguo la ccm, na kitambulisho cha kura kiliitwa kichinjio kwa ajili ya kumchinjia Lowassa iwapo angekuwa mgombea wa ccm?
Magufuli alipewa nafasi na ccm sio kwakuwa alikuwa anakubalika na wanaccm, bali ndio pekee aliyekuwa amebaki wangalau angekuwa na nguvu ya kupambana na Dr. Slaa, na hii ni kutokana na rekodi yake ya utendaji hasa kwenye miundombinu. Iwapo sio hofu ya Dr. Slaa, Leo hii Membe ndio angekuwa rais kupitia ccm iwapo ingeshinda na wala asingekuwa Magufuli. Msituone hatujui lolote, kama kuna sifa kubwa alikuwa nayo na ndio hasa ilimpa nafasi ni pesa yake na sio zaidi ya hapo. Slaa kama Slaa kilichomfanya aondoke cdm, ni kuzira na shinikizo la mkewe kwa kukosa nafasi ya kugombea urais ambayo walikuwa wamejiandaa nayo. Ila sababu ya kuwa aliondoka kwakuwa Lowassa sio msafi ilikuwa ni kisingizio tu, japo katika mazingira yale sababu hiyo inambeba, lakini ukweli ni kuwa alizira baada ya yeye kukosa nafasi ile.
Halafu napenda muelewe wala msitake kupotosha, cdm ilivyokuwa iko kwenye damu za wananchi hiyo 2015, ingepata kura nyingi sana iwapo Dr. Slaa angekuwa mgombea, na hata kama asingekuwa rais kutokana na mfumo wa uchaguzi ulivyo, bado cdm ingebaki na haiba yake, kuliko ilivyokuwa baada ya Lowassa kuingia.