Anyway,
Naona wadada wengi humu wanasema wana cheat kwa sababu waume zao wamekua wavivu kwenye kuwahudumia!
Lakini wanawake mnajisahau sana. Msianze tu kulaumu kuwa wanaume ni vilaza, hawajui mapenzi n.k. Embu tafakari, kabla hamjaanza kuishi pamoja ni vitu gani mwanaume wako alikua anavutiwa navyo kwako? Ulikua unaongea vipi na yeye? Vitu gani alikua hapendi? Vitu gani alikua anapenda? Na je bado unavifanya?
Hivi vitu vidogo vidogo ambavyo mnapuuzia huwa vina matter sana na huenda ndio vilifanya hata akaamua kuishi na wewe.
Ili mahaba yadumu kwa muda mrefu, yanahitaji wote wawili mjijali, muweke jitihada kwenye mapenzi yenu bila kukata tamaa, tofauti na hapo kama hakuna uvumilivu, mtachokana tu, na mambo ya kuchepuka yataanza. Na hata huko kwenye michepuko kuna deadline pia, so it's just a short time relief, not a long term solution!
Ni hayo tu.
#laskaboza