Nyumba ya Polepole kuvunjwa haijalishi iwe ya kibunge au ya kiraia huo ni uhalifu na unatakiwa kufanyiwa kazi na jeshi la polisi bila kujali chochote.
Kusema Polepole anajikweza kisa nyumba yake haikuwa na mali nao ni ushamba tu, ingekuwa na mali nyingi naamini pia ungesema Polepole fisadi, kuwa na mali nyingi au chache ni life style ya mtu yeyote anajiamulia, sio kigezo cha uzalendo, na sio kila mwenye mali nyingi au chache ni mwizi au mtakatifu, hizi sababu nyepesi ulizo leta hapa hazina mashiko.
Kuhusu majirani sidhani kama Polepole ameajiri majirani zake wawe walinzi wake, nao wanakazi zao, una hakika wakati wa tukio hao majirani walikuwepo nyumbani? na kama walikuwepo hawakuwa na shughuli nyingine wakawa wametega macho na masikio yao kwa Polepole tu?
"Ushuani" ni tofauti na "uswahilini" ambapo kila anaeingia na kutoka huonekana, hata ukila maharage kwako majirani wote wanajua, usikariri maisha yako ukayahamishia kwa mwenzako.
Siku hizi watu wanapanda ndege wanazunguka karibia nchi nzima kwa siku moja, wewe unashangaa umbali kati ya Manyara na Dodoma ambao hata kwa gari mtu anafika? hizi mindset zenu....
Hicho kikao walichokaa Polepole na CCM wenzake ili watuondoe kwenye lengo la msingi [Katiba Mpya] kilifanyika lini na wapi? Kila siku mnalilia mikutano ya kisiasa irudishwe kwa wote, ila Polepole kutoa maoni yake apuuzwe!, hamkumbuki anayemnyima Polepole ndie anaewanyima nyie.
Sio kwasababu Polepole ni mwanasiasa mwenye mawazo tofauti na kambi yake ndio aanze kutengwa na kutafutiwa sababu za kila aina, ajibiwe hoja zake maisha yaendelee, kwasababu ni haki yake kutoa maoni na wanaoulizwa sharti wamjibu wasimtishe, kumkejeli, au vyovyote vingine.
Haiwezekani leo kutaka Polepole apuuzwe kwa kutoa hoja zake, ila nyie "wana demokrasia" mkitoa hoja zenu mtake zijibiwe, hii ni double standard, haki haina mipaka na haichagui sura, kama mnaona Polepole ana makosa nendeni mahakamani na hao wenzenu mliowaunga mkono bila kujitambua, opposition is an art.