Kama wanawake wanapenda sana quarrels ndio maana mnaenda nyumba ndogo, hizo nyumba ndogo siyo wanawake?
Kama ni wanawake, je kuna kozi maalum ya kusomea kuwa nyumba ndogo - in other words is NN a profession, kama ndio basi mjue mnaibiwa tu.Its a matter of time jamani.
Nitamalizia hivi, binadamu kwa hulka aliyoumbwa nayo, anayo tabia ya kupenda mabadiliko. Na hii ni kwa wote wanawake na wanaume.Tofauti iko kwenye mifumo ya maisha,mila, desturi na imani za kidini zenye kutuwekea mipaka.Mipaka hii inafanya watu wawe na kiasi, wajizuie kufanya mambo fulani kwa kuogopa Mungu, jamii, serikali n.k.
Hii mipaka isingekuwepo, basi si ajabu hakuna mwanaume wala mwanamke angebakia na ndoa yake kwa vile kungekuwepo na alternatives za kukimbia kero na kutafuta furaha na faraja.
Inashangaza kuona ati akina kaka walio wengi wanadhani wao wanayo haki kukiuka mipaka lakini wanaamini kabisa kuwa wanawake wao hawapaswi kukiuka. Wanasahau hakuna binadamu mwenye roho y achuma na mwingine ya sufi. Kumbuka usitende usichopenda kutendewa na hii ndio golden rule.Ukijua kuwa kitu fulani kinakuumiza wewe ujue ukimfanyia mwenzio naye utamuumiza. Je ni sawa?