Kitaalam sqm 1 ya nyumba bei yake ni 500,000 mpk 750,000 sasa piga hesabu nyumba yako ina ukubwa gani kwa sqm kisha zidisha. Hizo bei imewekwa range kuzingatia maeneo na tofauti ya bei ya materials. Kwa hiyo kama unauziwa nyumba angalia bei ya viwanja maeneo hayo kwa sqm kisha angalia ukubwa wa nyumba kisha zidisha.
Hizo bei nilizotaja ni kwa nyumba standard iliyojengwa na materials imara na ni mpaka finishing zote.
Sio unaenda tu unaambiwa kijumba kinauzwa 180m kwa kuwa kiko Mbweni wewe unatoa bila kufanya tathmini ya kitaalam. Utaishia kupigwa mara mbili ya bei ya kawaida.
Tatizo Bongo nyumba zinauzwa na madalali kwa ufundi wa kuongea na sio kutumia valuers wenye weledi na waliosomea hayo mambo.
Mwisho wa siku kijana unaogopa kujenga wakati ungeanza at your 20s ungekuwa na nyumba 10 ukifika 40 au 50yrs.
Amkeni watanzania halafu mtu anajitolea kuwaelekeza tena bure mnaleta ubishi wa kijinga sijui fundi Michael sijui kila mtu ana ghorofa. Soma between lines hata kama kichwa chako ni maji utaokota kitu kikusaidie maishani mwako.